DOKEZO Geita: Mkandarasi wa REA mtaa wa Nyantororo A juu (Msikitini) ameweka nguzo kwa watu waliotoa hongo na kuacha mamia

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mkandarasi wa huduma ya umeme REA mtaa wa Nyantorotoro A Geita Msikitini kwa juu ametufanyia hujuma sana wananchi. Nguzo za mradi wa umeme zimewekwa kwa kujuana sana kinyume na ramani ya mradi ilivyokuwa kabla ya yeye hajaanza kazi

Nguzo zilikuwa zinauzwa kwa watu bila kutoa hongo (rushwa) huwekewi nguzo, badala yake wananchi wengi wamekosa nguzo za umeme na mradi uko mwishoni

Idadi ya waliopewa nguzo hawafiki hata watu 20 lakini walionyimwa nguzo kwa sababu hawakutoa rushwa ni zaidi ya watu 100, hivyo tunaiomba Serikali iingilie suala hili kwani limeenda kinyume na utaratibu
 
TAKUKURU wako wapi
 
Kutoa rushwa ili kupata huduma za kijamii ambayo kimsingi inatakiwa kutolewa bure kunakwamisha maendeleo kwa kuzalisha ukosefu wa usawa. Wananchi wengi wanakosa huduma muhimu kwa sababu ya upendeleo, jambo linalozuia ustawi wa jamii kwa ujumla. Serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya rushwa hizi zinazolazimishwa na watendaji ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inanufaisha wote kwa haki.
 
Back
Top Bottom