Geita: Mkoa "tajiiri" usiokuwa tajiri

Unaposhangaa ya mkoa wa Geita unapaswa ushangae pia na ya mkoa wa Shinyanga wale Wana Almasi na Dhahabu pia lkn ni maskini wa kutupwa.
Hivi tatizo ni nini lakini? Uafrika?

Inasemekana, miaka kama kumi hivi baada ya mgodi wa Almasi kuanza kazi, Williamson alikuwa ameubadilisha sana mji wa Mwadui.

Vipi kama Williamson angeendelea na hiyo Kasi kwa miaka hamsini mfululizo?
 
Vumbi jepesi linaingia hadi kwenye Koo dhahabu unaweza kuwa unachimba choo ukakutana na mkanda ila geita imebarikiwa aisee
Ishatokea mara nyingi tu. Si ajabu mtu kuanza kuchimba shimo la choo lakini mpango ukabdailika baada ya muda mfupi, shimo lililotarajiwa liwe choo linakuwwa mgodi.
 
Viongozi bado nasema mikataba mingi haikulenga kuinufaisha geita na hii huenda kwa mikoa mingine pia yenye rasilimali
Nadhani angalau sehemu kubwa ya Pato ingerudi kuboresha miundombinu ya mahali husika.
 
Mwanzo kabisa geita iliijenga zaidi mwanza labda kwa Sasa itaanza kujenga Geita yenyewe kuzidi dar sio rahisi.
 
Kama ingelikuwa ni uamuzi wangu, ningeagiza asilimia sitini mpaka themanini ya mapato iwe inabaki kwenye mkoa husika kwa ajili ya maendeleo yake.

Iweje usaidie kulisha watoto wa jirani yako huku familia yako inalala njaa?

Naamini, hela ya Geita imesaidia kujenga flyover Dar Es Salaam.

Naamini, hala ya Geita inetumika kulijenga jiji la Dodoma.
 
Mwanzo kabisa geita iliijenga zaidi mwanza labda kwa Sasa itaanza kujenga Geita yenyewe kuzidi dar sio rahisi.
Siyo rahisi kuizidi Dar, lakini inaweza kuikaribia.

Dhahabu ina hela sana. Na asilimia arobaini ya dhahabu yote inayochimbwa Tanzania inapatikana Geita.
 
Mwanzo kabisa geita iliijenga zaidi mwanza labda kwa Sasa itaanza kujenga Geita yenyewe kuzidi dar sio rahisi.
Kwa mfano tu, Geita ikiachwa ijiendeshe yenyewe bila kuingiliwa na Serikali kuu, kwamba iwe kama kanchi ndani ya nchi ya Tanzania, kama Vatican ilivyo nchi ndani ya Italy, Geita ingeendelea kuwa duni kama ulivyo sasa?
 
Hapana lakini ili kufanikisha Hilo wangehitaji rasilimali watu ambayo ndio nyenzo muhimu sana kwa maendeleo ya mji
Watu ambao watawekeza ndani ya mkoa na watasimamia mapato kwa usahihi kwa mfano Leo TU nimeona hesabu za ndani zimetiliwa Mashaka na mara kadhaa wamekuwa wakipata hati chafu mwaka kama sikosei 2018 Nyang'hwale zililiwa zaidi ya bilioni 3 hela za miradi Sasa hii nayo ni shida ambayo hata mkiachwa wenyewe hamtaendelea
 
Ila sometimes Watanzania...
 
Mkuu mikoa ya bara inasaidia kuijenga dar. Utaidharau Geita Leo lakini kutokana na mifumo yetu,kinachopatikana kinaingia serikali kuu kwenda kuijenga dar na Dodoma. Tukisema kila mkoa ujitegemee, ndani ya mwaka geita utaufuta huu Uzi.
Hiyo ni sababu mojawapo inayonifanya niichukie sera ya ujamaa. Aliyetokwa na jasho anaweza asikifaidi ipasavyo alichokitolea jasho huku asiyejia jasho akineemeka na vya mvuja jasho..
 
Ahsante nakubaliana na wewe serikali majimbo ndio jibu haiwezekani Geita expolrts zahabu ni Usd bilioni 3 kwa maka yet hawana hata stendi ya basi ya kueleweka
 
Ahsante nakubaliana na wewe serikali majimbo ndio jibu haiwezekani Geita expolrts zahabu ni Usd bilioni 3 kwa maka yet hawana hata stendi ya basi ya kueleweka
Hawana stendi!

Hawana lami!

Hawana mijengo ya maana!

Kwetu si Geita, lakini nahisi Geita inapunjwa.

Ni aibu mkoa uliosheheni utajiri mkubwa kuwa maskini.
 
Mkuu, kuna hoja hapo juu kuwa Kenya inanufaika zaidi na Tanzanite kuliko wenyewe. Kama ndivyo, Kenya inanufaika kupitia wachimbaji wakubwa au wadogo?

Kama ni kweli, kwa nini iwe Kenya na siyo Tanzania au Manyara au Arusha?
Huwezi Ku control hawa wachimbaji wadogo.. Kenya inafaidika Kwa ulanguzi lakin haipati hasara ya mashimo..madini yakiisha
 
ila Mbona Mwendazake alijitahidi kukupambania hapakupanda kidogo ?
 
Mkuu, kuna hoja hapo juu kuwa Kenya inanufaika zaidi na Tanzanite kuliko wenyewe. Kama ndivyo, Kenya inanufaika kupitia wachimbaji wakubwa au wadogo?

Kama ni kweli, kwa nini iwe Kenya na siyo Tanzania au Manyara au Arusha?
Kenya inafaidika kwa vile kwa miaka mingi walikuwa wananunua kwa kimagendo, na wale wafanyabiashara wao wakitaka kusafirisha wanalipa kodi kwenye serikali yao.

Wale wauzaji Tanzanite wa kwetu wanauza kimagendo, serikali haipati faida yo yote na la kushangaza hata wao wafanyabiashara wenyewe sio matajiri kivile (at least huo utajiri wao hauonekani kuwa mkubwa sana)
 
Ni taarifa za kweli mkuu mpka leo India ndiyo muuzaji no 1 wa Tanzanite akifuatiwa na Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…