Geita: Mkoa "tajiiri" usiokuwa tajiri

Leo, ikiwa ni siku ya mapumziko, nimetembelela eneo lililoanzishwa machimbo mapya ya dhahabu hivi karibuni hapa Geita. Pichani ni mwanamke akiokota mawe anayodai yana dhahabu kwa lengo la kwenda kuyauza.
 

Attachments

  • IMG_20230629_131859.jpg
    1,016.3 KB · Views: 13
  • IMG_20230629_131851.jpg
    1.3 MB · Views: 13
  • IMG_20230629_131845.jpg
    1.3 MB · Views: 12
upo geita sehemu gani?? karibu uje uchome nyama hapa bever night club
 
Upo sahihi kabisa,halafu njoo shangaa Tanzania ilinganishae na Quatar,halafu baada ya hapo ishangae Africa,ilinganishe na Australia.
 
Leo, ikiwa ni siku ya mapumziko, nimetembelela eneo lililoanzishwa machimbo mapya ya dhahabu hivi karibuni hapa Geita. Pichani ni mwanamke akiokota mawe anayodai yana dhahabu kwa lengo la kwenda kuyauza.
Jirani na machimbo ya dhahabu yajulikanayo kama Tembo Mining, nimewakuta watoto wadogo wametoka kuvua samaki kwenye mto mdogo pembezoni mwa barabara. Walio hai wamewatengea kwa ajili ya kwenda kuwafuga na waliokufa wanaenda kuwatumia kwa mboga.

Ila nimeshangazwa pia kuwakuta wanaume watu wazima wakioga mtoni pembezoni mwa barabara Mchana kweupe bila kujali watoto na wanawake wanaopita jirani na wanakoogea. Kama huo ni ujasiri, basi wanastahili pongezi. Wengine wasingethubutu.
 

Attachments

  • VID_20230629_140553.mp4
    48.7 MB
Upo sahihi kabisa,halafu njoo shangaa Tanzania ilinganishae na Quatar,halafu baada ya hapo ishangae Africa,ilinganishe na Australia.
Nahisi Geita imeonewa ama imejionea. The region is so rich!

Kama dhahabu za kuokotwa zipo, zilizokwisha kuchimbwa, zinazochimbwa na zinazosubiri kuchimba ni nyingi kiasi gani?
 
Mkuu mikoa ya bara inasaidia kuijenga dar. Utaidharau Geita Leo lakini kutokana na mifumo yetu,kinachopatikana kinaingia serikali kuu kwenda kuijenga dar na Dodoma. Tukisema kila mkoa ujitegemee, ndani ya mwaka geita utaufuta huu Uzi.
Japo uzi una muda mrefu lakini hili ndiyo jawabu sahihi!.

Hii nchi kuna mikoa inanyonya rasilimali za maeneo mengine na kujisifu wana maendeleo huku mikoa inayotoa ikiwa kwenye hali mbaya

Mkoa wa Geita ukitoa hiyo highway ya Mwanza Bukoba hakuna barabara yoyote ya lami inayozidi 5km

Ukitaka kwenda mkoa wowote tofauti na Mwanza Musoma au Kagera unapita barabara ya Vumbi.
 
Kwa kuwa wewe mi mjanja kuliko wana Geita, njoo uchimbe utajirike uoneshe mfano.
 
sera ya majimbo ya chadema ilikuwa na maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…