Geita: Mkoa "tajiiri" usiokuwa tajiri

Geita: Mkoa "tajiiri" usiokuwa tajiri

Kile unachokiona Geita (nimeishi pale Nyang'hwale) ni matokeo ya mikataba mibovu iliyoingiwa na viongozi wa nchi hii na wao kwenda kujineemesha.
Yote uliyosema ni kweli ukila nanasi la geita hutakula nanasi la mahali pengine uhisi umekula nanasi
Mikataba mikataba mikataba hiki ndio nira iliyoiba na kumaliza mali za watanzania na ndoto hata ya kuwa Gaborone haipo acha Jos
Geita mkoa mzima hauna Rami kilomita 10
(Usiniambie Ile ya highway ya mwanza bukoba) hakuna maji ya uhakika
Kweli kabisa
IMG_20230623_175759.jpg
 
Sijawahi kufika Geita lakini tatizo ni CCM, angalia Mirerani na utajiri uliyopo ni aibu tupu lami yenyewe ya mchongo tena ya juzi, Arusha na Moshi hakuna stand
Nasikia, Kenya ilishawahi kusifiwa kwa kusafieisha TANZANITE.

Inasemekana, South Africa walishawahi kupewa tuzo kwa kuuza TANZANITE.

Ajabu, nchi zote hizo mbili hazina "shamba" la Tanzanite.

Walizitoa wapi?

Ila nilisikia tu, sina uhakika kama ni taarifa ya kweli au ni porojo.
 
Nilikuwa nabeba ukifika dar ukiwapa kesho yake wakileta Yao nyumba nzima wanakataa kula nikaona ni kuwatesa Geita Kuna nanasi aisee na embe na samaki na Kila utajiri
Kwa utajiri uliopo Geita, ilistahili iwe na Airport kubwa na ya kisasa.

Kwa utajiri uliopo Geita, ilipaswa kuwa na miundombinu bora kabisa.

Kwa utajiri uliopo Geita, kulipaswa kuwepo na mijengo inayotambulisha kuwa ni mkoa tajiri.

Kwa utajiri uliopo Geita...
 
Uko sahihi kabisa lakini kinyume chake hali ni mbaya Sana mvua ikinyesha barabara hazipitiki kabisa
 
Tena Kama kipindi hik Kuna vumbi jaman geita duuh
Sikuwa na kawaida ya kuvaa kofia wala miwani, lakini kuna maeneo ukipita, inabidi uvae kofia na miwani ya kukukinga na vumbi. Vinginevyo, utafika uendako ukiwa umetapakaa vumbi kichwani na usoni. Ndivyo wengine tufanyavyo. Unavaa kofia na miwani, ukishapita eneo lenye vumbi sana, unazivua na kuzihifadhi kwenye begi.
 
Jamn tunaoshi Geita tunapata tabu some time
 
Vumbi jepesi linaingia hadi kwenye Koo dhahabu unaweza kuwa unachimba choo ukakutana na mkanda ila geita imebarikiwa aisee
Mimi ni mpitaji Geita, lakini kwa jinsi palivyo, nahisi kuwahurumia wenyeji wake na kuwakasirikia viongozi wake.

Geita inastahili kuwa duni kama ilivyo sasa, kweli?

Geita ni ya kuzidiwa na Kilimanjaro kimaendeleo, kweli?

Tatizo ni wananchi au viongozi?

Siyo haki kabisa.
 
Geita ni mkoa ambao kila ukitajwa mwili wangu unasisimka maana huwa nalikumbuka dikteta uchwara lililotoka mkoa huo.

Kwahiyo huwa siupendi kusikia wala sina mpango wa kutembelea mkoa huo wenye laana ya kumtoa dikteta aliyeitesa na kuinajisi nchi kiasi kile
 
Jamn tunaoshi Geita tunapata tabu some time
Kumbe ni wa Geita! Tuambie, kwa nini Geita, mkoa mzuri "mtajiri" uliojaliwa utajiri siyo tajiri?

Kwa nini Geita si tajiri kuizidi mikoa mingi Tanzania?

Sidhani kama nitakosea nikisema kwamba kwa utajiri uliopo Geita, ungeweza hata kuwa tajiri kuizidi Dar Es Salaam. Nimefikiri tu.
 
Geita ni mkoa ambao kila ukitajwa mwili wangu unasisimka maana huwa nalikumbuka dikteta uchwara lililotoka mkoa huo.

Kwahiyo huwa siupendi kusikia wala sina mpango wa kutembelea mkoa huo wenye laana ya kumtoa dikteta aliyeitesa na kuinajisi nchi kiasi kile
Lakini mkuu, Geita ni Tanzania pia. Na kama upo Dar Es Salaam au Dodoma, huenda unanufaika na "jasho" la Geita kuzidi wanaoishi Geita. Uupende tu, na uutetee ukiweza.

Geita, mkoa mzuri na tajiri, haupaswi kuwa choka mbaya kama ulivyo sasa.
 
na Mererani vumbi limepungua siku hizi? Kenya wanafaidika zaidi na tanzanite kuliko wenyewe.
Hakuna nchi iliyofaidika Kwa ku entertain wachimbaji wadogo...huu ndo ukweli....mchungu watu wakitaka mafanikio lazima tuambiane...
 
Hakuna nchi iliyofaidika Kwa ku entertain wachimbaji wadogo...huu ndo ukweli....mchungu watu wakitaka mafanikio lazima tuambiane...
Mkuu, kuna hoja hapo juu kuwa Kenya inanufaika zaidi na Tanzanite kuliko wenyewe. Kama ndivyo, Kenya inanufaika kupitia wachimbaji wakubwa au wadogo?

Kama ni kweli, kwa nini iwe Kenya na siyo Tanzania au Manyara au Arusha?
 
Back
Top Bottom