Geita: Mtoto achomwa na petroli kwa sababu ya kuiba Tsh. 800/=

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mtoto anayesoma Darasa la Tatu katika shule ya Msingi Kasota (9) Mkazi wa kijiji cha kasota Kata ya Bugulula Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo amejeruhiwa kwa kumwagiwa mafuta ya Petrol na kuwashwa moto mwilini mwake na Mama yake mzazi kwa kosa la kuiba Pesa.

Akizungumzia tukio hilo Mama mdogo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kama Siwema Kulwa amesema chanzo ni mtoto huyo anatuhumiwa kuiba pesa ya Mama yake kiasi cha shilingi 800 ndipo mama yake alipochukua uwamuzi wa kumchoma moto.

Soma pia: Mbeya: Mtoto wa miaka 8 achomwa moto na jirani kisa kupoteza sh 200

"Nilipigiwa simu nikiwa Geita na majirani nikaambiwa Dada wahi hapa kwa dada yako kuna tukio, nikauliza tukio gani nikaambiwa dada yako kachoma mtoto moto nikauliza kisa nini akasema kisa mtoto kaiba 800”alisema Mama mdogo Siwema Kulwa.

Mganga Mfawidhi kutoka Hospitali ya Wilaya Nzera Dkt.Shadrack Omega, amekiri kupokea Mtoto huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusema mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu huku akisema mtoto huyo amemwagiwa mafuta ya petrol na kuchomwa moto.

Attachments

  • Screenshot 2024-12-03 160654.png
    Screenshot 2024-12-03 160654.png
    509.8 KB · Views: 6
Nadhani umesahau sifuri zingine
 
Changamoto za maisha na ukosefu wa baba ni chanzo kikubwa cha MAMA KUWA KATILI
 
Hizo petrol wanazipatia wapi? Zinakuwa ndani kwao?
 
Mtoto anayesoma Darasa la Tatu katika shule ya Msingi Kasota (9) Mkazi wa kijiji cha kasota Kata ya Bugulula Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo amejeruhiwa kwa kumwagiwa mafuta ya Petrol na kuwashwa moto mwilini mwake na Mama yake mzazi kwa kosa la kuiba Pesa.

Akizungumzia tukio hilo Mama mdogo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kama Siwema Kulwa amesema chanzo ni mtoto huyo anatuhumiwa kuiba pesa ya Mama yake kiasi cha shilingi 800 ndipo mama yake alipochukua uwamuzi wa kumchoma moto.

Soma pia: Mbeya: Mtoto wa miaka 8 achomwa moto na jirani kisa kupoteza sh 200

"Nilipigiwa simu nikiwa Geita na majirani nikaambiwa Dada wahi hapa kwa dada yako kuna tukio, nikauliza tukio gani nikaambiwa dada yako kachoma mtoto moto nikauliza kisa nini akasema kisa mtoto kaiba 800”alisema Mama mdogo Siwema Kulwa.

Mganga Mfawidhi kutoka Hospitali ya Wilaya Nzera Dkt.Shadrack Omega, amekiri kupokea Mtoto huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusema mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu huku akisema mtoto huyo amemwagiwa mafuta ya petrol na kuchomwa moto.

View attachment 3168120
TOPIC YA ""MEASUREMENTS AND EVALUATION""

Ipelekwe mpaka kwenye ngazi ya Chini kabisa yaan NGAZI YA BALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI.

Ukatili uliopitiliza na unyama wa mwitunii
 
Back
Top Bottom