Geita: Mwalimu ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia

Geita: Mwalimu ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia

Mwalimu wa shule ya msingi ng'weja mwalimu Nteba. M . Shija (36) ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia.
Tukio hilo limetokea juzi 13/3/2025.mwalimu huyo aliamka siku hiyo akiws salamq akaenda shule ila baada ya kutawanyisha watoto mida ya saa tano akawa amerudi nyumbani kwake muda huo mke wake alikuwa shambani muda huo ndio akautumia kujinyonga.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

View attachment 3271572
Siku hizi Hata Mimi Bushdokta Wakiniua wasiojulikana watasambaza habari za uongo kwamba nimejinyonga kwa matatizo ya kifamilia Mapenzi au Madeni.

Wasiojulikana wamebadili Mbinu.
 
Mwalimu wa shule ya msingi ng'weja mwalimu Nteba. M . Shija (36) ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia.
Tukio hilo limetokea juzi 13/3/2025.mwalimu huyo aliamka siku hiyo akiws salamq akaenda shule ila baada ya kutawanyisha watoto mida ya saa tano akawa amerudi nyumbani kwake muda huo mke wake alikuwa shambani muda huo ndio akautumia kujinyonga.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

View attachment 3271572
 
Itakuwa ni madeni

Matatizo gani hayo ya kifamilia mpaka nijiue
Mkuu; tema mate chini. Ndani ya familia au Ndoani yapo mengi tena ya siri kubwa hayasemwi wala kuandikwa.
Hapo teacher alifikiriaaa; akapiga taswiraa, akawaza na kuwazua lakini wapi; dah! akaona kete zake zote (michongo yote) hakuna hata kete moja walau ina dalili ya kuweza kuingia king.
Maswali ya kudhania:
1. Mke wake aliona bora aende shambani kuliko kumwandalia mme wake walau ka-chai ili jamaa akirudi apate cha kutia mdomoni. Kwa nini iwe hivyo?
2. Tarehe ya tukio i.e. 13/3/2025 ni kati ya zile tarehe ambazo waajiriwa wengi huwa hela ya mshahara zimeshaisha- Wenyewe wanaita "Tarehe Dume". Sasa kama alikuwa na madeni esp. ile mikopo ya kausha damu na hakumshirikisha Mke wake wakati wa kwuchukua mkopo; ndo kimbembe kinaanzia hapo.
 
Walimu inabidi wapewe posho kama ilivyo polisi ili kuounguza msongo wa mawazo na kuishi Kwa amani kama polisi
 
Watoto wanne ni familia iliyokaa muda mrefu pamoja.
Amemuacha mama wa watu na watoto.
Nani atawapambania dunia hii aisee.
Angalia maslahi yako hata wewe umezaliwa tu kwa maamuzi ya wengine.
 
Angalia maslahi yako hata wewe umezaliwa tu kwa maamuzi ya wengine.
Yaan kama swala ni kuangalia maslah yako hupaswi kuzaa.

Maendeleo ya Generation ni jukumu la Mkuu wa generation.

Inategemea na ukoo lakini, kwetu nikataka kuoa babà yangu lazima anipe N’gombe watatu, ni lazima sababu yeye alipewa na Babà yake.
 
Wanaume tujifunze kujipenda wakati mwingine

Kutokujipenda kunapelekea wakati mwingine kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kujiua kama hivi

Na takwimu zinaonesha Wanaume ndiyo wengi hufa Kwa kujiua kunaposababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo stress.

Studies mbalimbali zinasema, katika wanaume 10 wanaopanga kujiua, basi Wanaume 8 hufanikisha kujiua, wakati Wanaume 2 pekee ndiyo hughairi kujiua.

Upande wa Wanawake, katika Wanawake 10 wanaopanga kujiua, ni Mwanamke 1 pekee ndiyo hufanikiwa kujiua

Wakati Wanawake 9 kati ya 10 hughairi kujiua.

Wanaume tusiache kujipenda

Haijalishi unapitia mazito kiasi gani, tusiache kujipenda
 
Hili suala la watu kujinyonga limekuwa mtiti.

Mtaa fulani ndani ya wiki watu 2 wamejipiga kamba.
 
Yaan kama swala ni kuangalia maslah yako hupaswi kuzaa.

Maendeleo ya Generation ni jukumu la Mkuu wa generation.

Inategemea na ukoo lakini, kwetu nikataka kuoa babà yangu lazima anipe N’gombe watatu, ni lazima sababu yeye alipewa na Babà yake.
🤣Hapo kwenu ni bora kwa sababu mko kwenye mila za kiafrika ,huku kwingine ni ubepari wazee wanataka tu ujitafute kikubwa umesomeshwa..

Mila yenu ni nzuri sana kama jamii ya wasukumu na wamasai.
 
1000038395.jpg
 
Back
Top Bottom