KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Akiongea na AyoTV_ ambayo imefika nyumbani kwa Wazazi wa Theresia kupata undani wa kifo hicho, Mama Mzazi wa Mtoto huyo amesema wakati tukio linatokea Mwanae alikuwa ndani ya nyumba akiwa anachungulia dirishani ndipo risasi iliyofyatuliwa na Polisi ikapita dirishani na kumpiga sehemu za kifuani na akafariki.
Soma Pia: GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa
“Mwanangu alikuwa amekaa chumbani kwake kitandani (kabla ya kuchungulia dirishani), Mimi nikiwa sebuleni, baada ya vurugu Mwanangu akaja analia huku anavuja damu nikamwangalia nikaona kifua kimetoboka”