Geita sasa ni kinara wa Matukio; RPC wa Geita Henry Mwaibambe Kazi unayo

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mkoa wa Geita sasa umekuwa na mfululizo wa matukio Hasa Matukio ya kujinyonga. Karibu kila siku RPC wa Geita Henry Mwaibambe amekuwa akitangaza Matukio hayo.

Matukio yanayo ukabili mkoa wa Geita ni Matukio ya vifo hasa kujinyonga na kuuliwa. Kwa mfano kwa Siku ya leo tu ni zaidi ya matukio Matatu ya vifo yameripotiwa na vituo tofauti tofauti kutoka mkoani Geita. Si kujinyonga tu na matukio Mengine kama ya Ubakaji na mengine.

Kwa tafiti zisizo rasmi Matukio mengi yanayo tokea mkoani Geita yanasababishwa na Mapenzi Huenda ukawa wivu wa mapenzi au ubakaji.

RPC wa Geita Henry Mwaibambe Pole kwa kazi ya kutangaza na kukemea kila siku unayo ifanya ila inatakiwa ushirikiane na Serikali ya Mkoa kutoa Elimu juu ya Matukio hayo.

Kwa leo ni hayo tu Wana Geita Sijui mmekubwa na nini.

Rejea Watu 28 wajinyonga Geita ndani ya miezi 6
 
Asikudanganye mtu mkuu wakazi wengi wa geita wana magonjwa ya akili japo hawajitambui....na hii imesababisha wengi kufanya matukio ya ajabu.

mkoa wa geita ni mkoa wenye migodi mikubwa na midogo ya dhahabu. huku geita kuna matajiri haswaaa lakini pia kuna masikini wa kutupwa.
 
Mbunge wa geita anasemaje huhusu hali hiyo? Na je hakuna nyumba za ibada geita ili watu wawe wacha Mungu?
 
asikudanganye mtu mkuu wakazi wengi wa geita wana magonjwa ya akili japo hawajitambui....na hii imesababisha wengi kufanya matukio ya ajabu.....mkoa wa geita ni mkoa wenye migodi mikubwa na midogo ya dhahabu...huku geita kuna matajiri haswaaa lakini pia kuna masikini wa kutupwa...
Basi counseling ya Akili inatakiwa kwa wakazi wa Geita
 
asikudanganye mtu mkuu wakazi wengi wa geita wana magonjwa ya akili japo hawajitambui....na hii imesababisha wengi kufanya matukio ya ajabu.....mkoa wa geita ni mkoa wenye migodi mikubwa na midogo ya dhahabu...huku geita kuna matajiri haswaaa lakini pia kuna masikini wa kutupwa...
... kama kuna kaukweli fulani hivi! mtukufu wetu naye si katokea pande hizo?
 
Mkoa wa Geita sasa umekuwa na mfululizo wa matukio Hasa Matukio ya kujinyonga. Karibu kila siku RPC wa Geita Henry Mwaibambe amekuwa akitangaza Matukio hayo.

Matukio yanayo ukabili mkoa wa Geita ni Matukio ya vifo hasa kujinyonga na kuuliwa. Kwa mfano kwa Siku ya leo tu ni zaidi ya matukio Matatu ya vifo yameripotiwa na vituo tofauti tofauti kutoka mkoani Geita. Si kujinyonga tu na matukio Mengine kama ya Ubakaji na mengine.

Kwa tafiti zisizo rasmi Matukio mengi yanayo tokea mkoani Geita yanasababishwa na Mapenzi Huenda ukawa wivu wa mapenzi au ubakaji.

RPC wa Geita Henry Mwaibambe Pole kwa kazi ya kutangaza na kukemea kila siku unayo ifanya ila inatakiwa ushirikiane na Serikali ya Mkoa kutoa Elimu juu ya Matukio hayo.

Kwa leo ni hayo tu Wana Geita Sijui mmekubwa na nini.

Rejea Watu 28 wajinyonga Geita ndani ya miezi 6
Huo mkoa unaongoza na matukio ya mauaji na kujiua,
 
Back
Top Bottom