Geita vs Yanga ,jicho la Mugah

Geita vs Yanga ,jicho la Mugah

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
It's wanderfull match.

Geita
Kocha minziro aliingia na plan nzuri na descpline nzuri huku akiwa na wachezaji wenye quality ya hali ya juu walifanikiwa kuizuia Yanga wasitengeneze nafasi za wazi .
Pia Geita kwenye kushambulia walifanikiwa Sana kutengeneza nafasi nyingi Ila umakini na labda Quality ya Mpole ili wahukumu

Defensi
Mabeki wageita walianza kwa kutoelewana lakini kadri muda ulivyoenda ndio walivyofanikiwa kuwa na chemistry nzuri kipindi Cha kwanza mchezaji ka Amos kadikilo alionesha kuwa ni miongoni mwa wachezaji 46 wa Tz waliowahi kucheza Afcon.
Duchu alikuwa bora Sana alitengeneza chance nyingi Sana na tuseme tu kuwa alimzidi Yasin Mstafaa

Yondani
Alicheza vizuri Ila alihukumiwa na kujulikana Sana madhaifu yake kwenye areal ball Ila Jana alicheza vizuri na kiwango Cha juu na nidhamu ya juu sana.

Viungo
Hapa Geita walianza na viungo wa 3 ,Kagoma ,Nashon na Abdalah ila walichokosea Sana ni Kelvin Nashon kucheza chini Sana ni Kama aliogopa mechi na hiki kilisababisha timu kuchelewa kufika eneo la kushambulia

Hasan Abdalah
Alitekeleza majukumu yake lakini Kuna kitu aliiangusha timu pasi zake nyingi zilikuwa ni square pass na hakuwa na dribling za kutosha labda kwakuwa minziro alipanga kutumia mafull backs wake kupush mashambulizi

Safu ya mbele
Hapa Geita walicheza vizuri na waligawana majukumu Ila Gorge Mpole aliwadissapoint wenzake na ndio hapo tulipoona Dan lyanga akiwa analalamika Sana maana kila mpira aliopewa Mpole alilazimisha kushoot na si kuangalia wenzake

Dan Lyanga
Alicheza vizuri kias Fulani Ila tulikosa kilichobora toka kwake kutokana na kupanic mapema mwanzo kulitokana na refa hasa wapembeni na badae akahamia kwa wenzake

Yanga
Kocha Nabi

Mohammed Nasreedin aliingia na plan ilifanikiwa hasa kutokana na kuwakosa aucho ,Djumaa na Saidoo alipanga kucheza kwa hadhari zaidi

Defensi
Kipa na Job mawasiliano yalikuwa chini Sana waliwapa Geita zawadi mbili ambazo hawakuzitumia vizuri hasa Mpole

Kiungo
Yanic alikuwa Bora Sana alicheza vizuri Ila wenzake walimuangusha Sana feisal Jana hakuwa Bora kiasi kile japo walidominate mchezo lakini walibaki kwenye eneo lao

Deus na Nkane walidhibitiwa ipasavyo Ila hata alipoingia Ambudo bado alidhibitiwa

Striker
Mayele

Dustin kalala mayele alitumia kosa moja la yondani kumwadhibu amekuwa striker Bora wanamna yake kwa ligi hasa ukilinganisha Tanzania mastraika wa aina hii hawajawahi kufanikiwa sana (Mavugo,Luizio na hata Vitalis Mayanga).
Anaonyesha kile alichokuwa anakifanya As Vita

Marefa
Big up Sana kayoko anajua kucontrol game bila kuangalia profile ya players
 
Safi umechambua bhuya,hila bwana Wallace karia wachambuzi wa mchongo kama nyie ndio anaowatafuta
 
Back
Top Bottom