Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu
Kumbe CCM wakiwatishia wapinzani ni sawa tu lakini Waoinzani wakiwatishia CCM, viongozi wake wanaenda hadi kwenye vyombo vya habari kulialia
Hivi karibuni nimemuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Yefred Myenzi, akieleza kuwa baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wameanza kutuma jumbe za vitisho kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.
Akizungumza kwenye kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Geita, Myenzi amesema vitisho hivyo vinaleta hofu kwa viongozi na kuwaathiri kisaikolojia, hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa uhuru.
Soma pia: Abdulrahman Kinana: Chaguzi za 2019 na 2020 zilileta hofu, Mwaka 2024 na 2025 zitakuwa za Huru na Haki
"Watendaji wangu ambao ni wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wanapokea meseji ambazo sio nzuri na kimsingi zinawaondoa kwenye reli ya kufanyakazi vizuri, maana inatakiwa uwe na utimamu wa akili bila hofu wala shinikizo unapofanya maamuzi lakini wakianza kutuma meseji za vitisho mara kuna maisha baada ya uchaguzi na meseji nyingine kama hizo tunawaondoa kwenye mudi ya kufanya kazi.
Wengi wanafanya kazi wakiwa na hofu ya kuogopa na kutishiwa sidhani kama anaweza kutoa maamuzi yaliyosahihi kwahiyo kama haujaridhika na mchakato nenda kwenye hatua inayofuata maana ofisi zetu zipo wazi"
Source: EATV