Geita: Wazee wa mkoa wawataka vijana kuchangamka na kuacha kuilaumu serikali

Geita: Wazee wa mkoa wawataka vijana kuchangamka na kuacha kuilaumu serikali

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Ikiwa leo Tanzania Bara inaadhimisha miaka 63 ya Uhuru wazee waliozaliwa kabla ya uhuru mkoani Geita wamewataka vijana kuacha kuilalamikia serikali kwamba haileti maendeleo kwenye jamii zao

Badala yake waiunge mkono izidi kuleta maendeleo kwani mpaka sasa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali.

Wakizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru kimkoa, wazee hao wamesema miaka 1960 Geita haikuwa na shule hata moja badala yake walilazimika kwenda Mwanza na enzi hizo waliokuwa wanasomea kwenye shule hizo ni wale wenye familia zilizokuwa na uwezo wa kifedha



Lakini kwa sasa kila kata ina shule ya sekondani hivyo ni maendeleo makubwa yaliyopatikana kipindi hiki cha miaka 63 ya Uhuru.
 
Back
Top Bottom