Geita yatangaza uhaba mkubwa wa walimu hasa wa Sayansi na Hisabati

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tatizo la uhaba wa Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati kwa Shule za Sekondari mkoani Geita limefikia asilimia 56 hadi sasa, hali inayosababisha wanafunzi wengi kutofanya vizuri kwenye masomo hayo na kuathiri maendeleo ya elimu mkoani hapa.

Akitoa taarifa ya elimu mkoani hapa wiki iliyopita, Ofisa Elimu Mkoa wa Geita, Anton Mtweve alisema hadi mkoa huo una uhitaji mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi 1,715, huku waliopo ni 744 na upungufu ni walimu 972.

Alisema pia shule za sekondari mkoani hapa zinakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sanaa 430 ambapo kwa sasa kuna walimu wa masomo hayo 2,106 ikilinganishwa na mahitaji ya walimu 2,416.

Mtweve alisema kwa upande wa shule za msingi mkoani hapa nazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu 7,565 kwani waliopo ni 8,796 ikilinganishwa na mahitaji ya walimu 16,361 sawa na asilimia 46.2.

"Tofauti ya uwiano kati ya walimu na wanafunzi ni kubwa sana ikilinganishwa na mwaka jana, hali hiyo imesababishwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza mwaka huu," alisema.

Akitoa taarifa ya hali ya ufaulu kwa shule za msingi na sekondari mkoani hapa, Mtweve alisema ndani ya kipindi cha miaka mitatu (2018-2020), kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba na kidato cha nne umekuwa wa kupanda na kushuka.

"Kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 88.53, mwaka 2019 asilimia 79.12 na mwaka jana ulifikia asilimia 82.49, huku kwa mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 91.7, mwaka 2019 asilimia 87.13 na mwaka jana ufaulu ulifikia asilimia 89.15," alisema.

Akizungumzia changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo ya sanyansi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule aliziagiza halmashauri zote kuangalia namna ya kupata walimu wa muda wanaoweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo na kuinua ufaulu wa masomo hayo.
 
Ummy Mwalimu wazir wa Tamisemi zile ajira za juzi juzi tu hapa kautangazia umma wa watanzania kwamba hakuna shule iliyokosa mwalimu wa sayansi, ina maana kaliongea taifa sio?
 
Kama walimu wa sayansi wameisha si muwaajiri madaktari ma wafamasia wakafundishe
 
Hizi shule zina kiburi na ndiyo maana Maths na Science wanafunzi wataendelea kufeli kila mwaka.

Unaacha kumchukua engineer akusaidie kuokoa jahazi unang'ang'ania mwalimu ambaye Maths akipata D.

Hakuna siku Maths na Science ambapp secondari za Tanzania zilifaulisha.

Sijawahi kuina average ikivuka 45%.

Shule zibadili outdated mentality.

Bila kuishinikiza serikali kuajiri, suala la uhaba wa walimu wa sayansi litaendelea kuwa tatizo alafu kwanini tozo za miamala zinazokusanywa zisielekezwe kuondoa hili tatizo?
 
Uhaba wa walimu wa sayasi na hisabati imekua tatizo kwa muda mrefu sana sasa

Serikali ikae chini na kutafuta suluhu ya kudumu maslahi ya muda mrefu kwa taifa letu
 
Kwani mmesahau serikali walisema watatumia Tehama kufundishia shule zake ambapo itapunguza ukosefu wa walimu Nchini [emoji1787]

Vip kwani hawajaanza kutumia hizi TEHAMA BADO
 
Ajira za juzi tuliambiwa kila shule imepewa mwalimu wa sayansi na hesabu nchi nzima, huo upungufu unatoka wapi?
Kiongozi ..unawaamini wanasiasa !!?? Kosa kubwa tulilofanya kama Taifa Taaluma kuipa mgongo na siasa kuipa upendeleo.

Na bado tutaona mengi zaidi maana Dunia ipo kwenye Science and Technology sisi bado hata hatujaanza kuandaa wataalamu.
 
Hizi shule zina kiburi na ndiyo maana Maths na Science wanafunzi wataendelea kufeli kila mwaka.

Unaacha kumchukua engineer akusaidie kuokoa jahazi unang'ang'ania mwalimu ambaye Maths akipata D.

Hakuna siku Maths na Science ambapp secondari za Tanzania zilifaulisha.

Sijawahi kuina average ikivuka 45%.

Shule zibadili outdated mentality.
Acha mamb yako bhana sio kwel kuwa mwalimu alipata D pale DUCE tumesoma watu kibao wenye ufauli mzur tuu nikiwemo mimi na A
 
Angekuwepo ninae mfahamu waziri husika kibarua kinge ota nyasi yaani Geita kabisa.
 
Serikali haina uwezo wa kuajiri hiii porojo tupu
 
Hapohapo unaonyesha hukulielewa somo la Statistics. Tunapoongelea performance hatuongelei one variable iliyopata A kama wewe na kama kweli uliipata.

Average ya mnaoenda ualimu mlipata D tena ni chini ya hapo. Hata Magufuli alisema vilaza waende ualimu akawafukuza pale UDOM.

Na hii inawaumbua inapoonekana Maths na Physics hamjawahi kutoa performance nzuri nchini mkasababisha students wanayaogopa masomo hayo.

Acha mamb yako bhana sio kwel kuwa mwalimu alipata D pale DUCE tumesoma watu kibao wenye ufauli mzur tuu nikiwemo mimi na A
 
Tatizo la uhaba wa Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati kwa Shule za Sekondari mkoani Geita limefikia asilimia 56 hadi sasa, hali inayosababisha wanafunzi wengi kutofanya vizuri kwenye masomo hayo na kuathiri maendeleo ya elimu mkoani hapa.

Akitoa taarifa ya elimu mkoani hapa wiki iliyopita, Ofisa Elimu Mkoa wa Geita, Anton Mtweve alisema hadi mkoa huo una uhitaji mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi 1,715, huku waliopo ni 744 na upungufu ni walimu 972.

Alisema pia shule za sekondari mkoani hapa zinakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sanaa 430 ambapo kwa sasa kuna walimu wa masomo hayo 2,106 ikilinganishwa na mahitaji ya walimu 2,416.

Mtweve alisema kwa upande wa shule za msingi mkoani hapa nazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu 7,565 kwani waliopo ni 8,796 ikilinganishwa na mahitaji ya walimu 16,361 sawa na asilimia 46.2.

"Tofauti ya uwiano kati ya walimu na wanafunzi ni kubwa sana ikilinganishwa na mwaka jana, hali hiyo imesababishwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza mwaka huu," alisema.

Akitoa taarifa ya hali ya ufaulu kwa shule za msingi na sekondari mkoani hapa, Mtweve alisema ndani ya kipindi cha miaka mitatu (2018-2020), kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba na kidato cha nne umekuwa wa kupanda na kushuka.

"Kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 88.53, mwaka 2019 asilimia 79.12 na mwaka jana ulifikia asilimia 82.49, huku kwa mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 91.7, mwaka 2019 asilimia 87.13 na mwaka jana ufaulu ulifikia asilimia 89.15," alisema.

Akizungumzia changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo ya sanyansi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule aliziagiza halmashauri zote kuangalia namna ya kupata walimu wa muda wanaoweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo na kuinua ufaulu wa masomo hayo.
Halmashauri inakusanya pesa nyingi inashindwa kuajiri vijana kwa mkataba wawafundishe watoto badala ya kusubiria ajira kutoka Serikalini kuu.

Hao vijana wakipewa hata 200,000 kwa mwezi watafundisha vizuri tuu.
 
Back
Top Bottom