Gen. Makenga, kamanda mkuu wa M23 amerudi DRC kuongoza mashambulizi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
M23.JPG

Kamanda mkuu wa kundi la waasi la M23 Generali Sultani Makenga amerudi mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, akitokea nchi Jirani ambayo msemaji wa kundi hilo Maj. Willy Ngoma hakutaja.

Maj. Ngoma amesema kwamba tangu arudi DRC, Generali Sultani Makenga amekuwa akitembelea wapiganaji wake katika sehemu mbali mbali mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo katika mji wa Bunagana ambao sasa unadhibitiwa na waasi wa M23.

Makenga, mwenye umri wa miaka 50, anasemekana kujua vizuri nguvu na uwezo wa jeshi la DRC, na eneo zima la kivu kaskazini.

Wachambuzi wanasema kwamba lengo la Makenga ni kutoa maelezo Zaidi kwa wapiganaji wake namna ya kupambana na jeshi la DRC na wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki endapo wataingia Congo.

“Bila shaka Generali Sultani Makenga amerudi DRC kutoka kule amekuwa amejificha, ili kuongoza mashambulizi mwenyewe. Amekuwa akiongoza akiwa mbali na sasa yupo na makamanda wake na wapiganaji. Hii ni kuwapa motisha kuendelea kupigana Zaidi.” Amesema Nabende Wamoto mchambuzi wa siasa za maziwa makuu akiwa Kampala, Uganda, katika mahojiano kwenye kipindi cha radio cha kwa undani (saa tatu hadi saa tatu na nusu usiku, Afrika mashariki), idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, VOA.

M23 Wanadhibithi Bunagana, waliwahi kudhibithi Goma
Waasi wa M23 waliwahi kudhibithi mji wa Goma mnamo mwaka 2012 lakini wakalazimika kuondoka kutokana na shinkizo la aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Barack Obama.

Mkubwa wa General Makenga wakati huo, Generali Bosco Ntaganda, aliyejulikana kama Terminator, na ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa - ICC, alikuwa amekataa kuamuru wapiganaji wake kuondoka Goma kabla ya aliyekuwa rais wa DRC wakati huo Joseph Kabila, kukubali matakwa ya waasi wa M23.

Makenga, alikataa kumsikiliza Ntaganda na akaamurisha wapiganaji wa M23 kuondoka Goma, hatua ambayo ilimkasirisha Ntaganda.

Uhasama kati ya Generali Sultan Makenga na General Bosco Ntaganda ulipelekea mpasuko katika kundi hilo na kutokea mapigano makali kati ya wapiganaji watiifu kwa kila upande, yaliyopelekea vifo vya wapiganaji kadhaa.

Source: Chimpreports
 
Kuna mdau aliwahi kusema humu makenga amefariki, mimi nilimkatalia na nikasema kuwa

1. Ni dhahiri jeshi la Rwanda ndio wafadhili wa m23, miaka ile ya nyuma ya JK mpaka UN walilaani rwanda kwa kufadhili genge hilo.

2. Kwa kuwa rwanda hana jeshi kubwa na wala hana uchumi mkubwa. Sio rahisi Rwanda akubali kupoteza Askar na vifaa vyake vingi, hivyo basi, wakizidiwa mapambano hawa M23 huwa wanakimbilia kwao Rwanda.

Hii ndio maana ni rahisi wao kurudi Congo sababu hawakubali kufa, wakizidiwa tu wanarudi Congo. Nkisema hawakubali kufa haimaanishi kuwa hawafi kabisa.
 
View attachment 2281413

Nadhani alikuwa Rwanda. Kwa vuguvugu la Rwanda na Congo la hivi karibuni, lilikuwa swala la muda tu Rwanda kuanza kujibu mapigo.
 
Sijui hili jeshi la Afrika ya Mashariki litafanyaje kazi? Rwanda anashutumiwa kufadhili hao waasi, na yeye ni mwanachama wa EAC. Mbaya zaidi Afrika hatuwezi kuambiana ukweli. Tabia ya Rwanda na Uganda haikemewi waziwazi.

Sijui mtego huu utanasuliwa vipi.
 
Kuna mdau aliwahi kusema humu makenga amefariki, mimi nilimkatalia na nikasema kuwa

1. Ni dhahiri jeshi la Rwanda ndio wafadhili wa m23, miaka ile ya nyuma ya JK mpaka UN walilaani rwanda kwa kufadhili genge hilo.

2. Kwa kuwa rwanda hana jeshi kubwa na wala hana uchumi mkubwa. Sio rahisi Rwanda akubali kupoteza Askar na vifaa vyake vingi, hivyo basi, wakizidiwa mapambano hawa M23 huwa wanakimbilia kwao Rwanda.

Hii ndio maana ni rahisi wao kurudi Congo sababu hawakubali kufa, wakizidiwa tu wanarudi Congo. Nkisema hawakubali kufa haimaanishi kuwa hawafi kabisa.
Makenga yupo mzigoooni tokea kitambo alipumzisha akili tu.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Amekifuata kifo chake mtakumbuka haya maneno.
Hahahahaha huyu mwamba ameshutumiwa kufa toka enzi zile za JK akiwa madarakan ila bado anadunda.

Anaonekana mapambano yakianza tu huwa faster anasepa kurudi rwanda.
 
Nakuambia amefuata kifo chake and ths time huwenda ikawa inside job
 
Hahahahaha huyu mwamba ameshutumiwa kufa toka enzi zile za JK akiwa madarakan ila bado anadunda.

Anaonekana mapambano yakianza tu huwa faster anasepa kurudi rwanda.
Makenga hua anaishi Uganda na hata Ile 2013 M23 iliposepa yeye na wapiganaji wake walienda Uganda na kundi jingine lilienda Rwanda.
 
Back
Top Bottom