Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Siyo rahisi kuyafikia malengo na mahitaji yenu ya msingi mengi na yote kwa pamoja. Inahitaji muda na nafasi.
Inafahamika na Imebainika Africa na duniani nzima, mnatamani mahitaji yenu yote ya msingi yatimizwe. Serikali imekubali, na imewaalika mezani kuzungumza nanyi mnataka nini tena mtaani?
Katika kuyafikia hayo msipokua na nidhamu ya pamoja katika kuyafikia hayo malengo yenu, ni dhahiri mnaweza kuyakosa yote.
Isifikie mahali mkachokwa na mnaowashinikiza watimize mahitaji yenu, lakini pia jumuiya ya kimataifa inayowapongeza kwa kujitambua na kuwatetea, kupoteza imani nanyi, na kuamini kwamba hamkua na nia ya kutimiziwa mahitaji yenu bali kuleta fujo na uharibifu tu; na pengine kuna mipango na mashinikizo ya kisiasa nyuma yenu.
Uvumilivu wa utawala na vyombo vya ulinzi na usalama unaelekea ukomo. Nanyi taratibu mnapoteza uelekeo, mnapoteza malengo, mapoteza muda na mnapoteza maisha. hapatakua na faidi kwa yeyote miongoni mwenu.
Ni muhimu nidhamu ya pamoja ikajengwa miongoni mwenu. pupa ikawekwa kando, vinginevyo mtakosa na kupoteza yote.
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote. mihemko sio deal.
Pokeeni salamu nyingi sana kutoka Tripoli-Libya na Khatoom-Sudani🐒