GEN Z kizazi kilichobarikiwa sana

GEN Z kizazi kilichobarikiwa sana

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2023
Posts
435
Reaction score
1,093
1996-2010.
Hichi kizazi kimebarikiwa sana,hakisubiri sijui serikali itoe ajira wanazama front wenyewe ni wapambanahi sana

Wengi wao wanajitegemea sio kama sisi kizazi cha millennium bado tupo kwa wazazi jitu lina miaka 36 bado lipo kwa mama.

Wengi wao wanapiga pesa simple sana sio mpaka watoe majasho.
Hawa jamaa wanajitambua sana

Wanaelewa duniani ni mapito kwa hiyo anatengeneza maisha fast
 
1996-2010.
Hichi kizazi kimebarikiwa sana,hakisubiri sijui serikali itoe ajira wanazama front wenyewe .
ni wapambanahi sana
Wengi wao wanajitegemea sio kama sisi kizazi cha millennium bado tupo kwa wazazi jitu lina miaka 36 bado lipo kwa mama.
Wengi wao wanapiga pesa simple sana sio mpaka watoe majasho.
Hawa jamaa wanajitambua sana
Wanaelewa duniani ni mapito kwa hiyo anatengeneza maisha fast

Hawa wanaibadili Africa sooner than we thought. Kuna wengine wanajidanganya wanachofanya hakionekani. Ila wajiandae. It the day will come if the necessary changes are delayed or overlooked.
Juzi kati General Mabeyo aligusia hatari tuliyonayo. Wenye masikio naamini walisikia
 
Sio kwamba ni special ila wamekua kwenye kipindi ambacho tatizo la ajira limekuwa kubwa na elimu imekuwa ya kuonekana kama si cha maana. Hii inawafanya waanze kutafuta alternatives mapema kuliko previous generations

Kingine ni internet, hii inawapa extra source of income, exposure ya dunia kupitia social media lakini pia uhuru wa kujielezea na kupata taarifa sahahi ambazo wasingezipata katika ulimwengu wa TV na radio ambazo zilikuwa controlled na serikali.

In short tunachokiona ni uhalisia wao kutokana na mazingira yao. Ila kuleta revolution nchini, Yes wana potential hiyo kwa sababu ni jeuri na wana mawazo huru
 
Hope unamaanisha wa nchi zingine so wabongo! Wetu hawana tofauti na boomers! Angalau boomers waligombea uhuru.

Hawa wabongo na milegezo hypnotized na uchawa? Wapo biz sn na kubet na visungura (hope watabadilika baada ya kodi kuongezwa mara 10)

Kwa sasa hawana mchango wowote kwa taifa, ni hasara tupu! Angalau millennials walichangamsha hakuna rais alilala bila kupata msukosuko! Mlimani ilikuwa mlimani kweli unasikia Nkhrumah hall imeitika na maazimio kila miezi michache. Siku hizi uchawa tangu maprof hadi watoto wao. UD imelala km uji wa mgonjwa ulioganda layer juu ya kupuliza, au mbege yenye kilemba. Tutazame tu kwa TV na Youtube mambo ya Gen kule nje then tukakope viroba tu sio daslam! Tusijidanganye.
 
Kenya kinachowasumbua ni ukabila hii ya finance bill Gen Z geresha Tu,nchi kama TZ watu wataandamana kama umoja na mshikamano wetu wa kitaifa utayumba ila tofauti na hapo sahau.Hiyo finance bill kila bajeti huwa naonaga zinapandaga tu hata TZ tumeongeza kodi hadi kwa Gen Z kwenye source zao za mapato huko kwenye mitandao.
 
Gen Z ndio watakuja kukitoa chama cha mapinduzi madarakani kupitia mitandao

Sooner than later. Kwanza wanashangaa inakuwaje likitu linaitwa fisiemu limekaa madarakani muda wote huo. Matatizo bado ni yaleyale.

Mfano mafisiemu yatakuja kwenye kampeni yatasema yataleta maji. Yatajenga Hospitali yatajenga barabara yataboresha huduma za afya.

Tunajiuliza kwani miaka yote nani anatawala?

Gen Z hawaelewagi hizo hesabu za kitwana
 
Hayo mambo ya Boomers, millenials na Gen Z ni huko US. Si huku wote bado tunajitafuta. Wote tunapigika, wote tunagombania fursa zilezile. Njaa tupu.
 
Back
Top Bottom