Lakini hii si slang iliyobuniwa tu mitaani. Ina mizizi katika historia ya fedha za Kenya wakati wa ukoloni wa Uingereza.
Kwa mujibu wa historia ya sarafu iliyochapishwa na Benki Kuu ya Kenya (CBK), shilingi 20 za Afrika Mashariki zilikuwa sawa na pound moja. Mfumo huo ulifanya jina “pound” kuendelea kutumika katika mazungumzo ya kila siku, hata baada ya Kenya kuanza kutumia sarafu yake ya kitaifa.
Mwaka 1949, noti ya shilingi 20 ya Afrika Mashariki ilikuwa na thamani sawa na pound moja. Baadaye, Kenya ilipoanza kutoa sarafu yake baada ya uhuru, jina hilo lilibaki kwenye lugha ya mtaani. Hivyo, mtu akikuambia “nipee pound,” huenda alikuwa anamaanisha shilingi 20, sio pauni za Uingereza unazozijua leo.
Leo hii, Gen Z wana Sheng yao, Millennials wana misemo yao, na wazee wana lugha zao za pesa. Lakini mifano kama hii inaonyesha jinsi historia ya nchi inavyoweza kuishi ndani ya maneno tunayotumia kila siku bila hata kufahamu asili yake.
Gen Z, mlikuwa mnajua hii historia ya “pound,” ama mmeisikia leo? Na Millennials, ni misemo gani mingine ya pesa ya enzi zenu ambayo Gen Z hawaielewi?