Gen Z Mnakimbiza sana Magari!

Ulisha ambiwa Tanzania hatuna barabara za kuendesha 300kms.
Highway zetu ZIMEJAA MATUTA na hapo bado kona kila kms 2-5 hiyo 300 utaendeshea wapi labda angani...
Huijui Tanzania yote. Kama wewe hujawahi au huwezi usiseme haiwezekani. Na huu uzi nimefungua kuwatahadharisha wanaofanya hivyo ni hatari kwao na watumiaji mengine wa barabara.
 
Ilikuwa inasoma ngapi Mkuu?
 
Hio picha yako ni edited. Lakini wapo vijana wanaendesha gari mpaka 300kph hapa hapa Tz. Kwani wewe unafikiri inachukua sekunde ngapi BMW M3 au Golf 7/8 R au Audi S3 kufika 250 au 300kph? Zipo video sitaki kuziweka hapa zitawa expose wenyewe.
Na Mimi niliziona ila wapo sahihi mjerumani ni hatari
 
Huu Uzi kila nikiyasoma maoni ya wadau nasema ashukuriwe Mungu tu maana tulikuwa tunafia kwenye ile Harrier... Jamaa yuko tungi afu ni saa sita na madakikayake usiku ..akaenda kuvaa semi trailer kwa nyuma iliyokuwa imepaki road... Ashukuriwe Mungu kama sio ile trailer kwa nyuma pale kulikuwa na lile ngao la chuma , tulikuwa tunakusanywa wote pale chini ya tairi za nyuma za hiyo trailer
 
Duh bado kuna mambo mnatakiwa kutimiza hapa duniani.
Malori yaliyoachwa barabarani huwa yanaua watu wengi sana.
 
mbona hata ile vitz yang haikimbii labda hao crown
 
300kph kwa barabara zipi?
 
Nadhani kukimbiza gari inategemea na aina ya gari.
Kuna gari yani kuendesha spidi ya kawaida ni kuionea na kuna gari kuikimbiza pia unaionea.
Anyway mwendo mkali haufai.
 
Nadhani kukimbiza gari inategemea na aina ya gari.
Kuna gari yani kuendesha spidi ya kawaida ni kuionea na kuna gari kuikimbiza pia unaionea.
Anyway mwendo mkali haufai.
Upo mrembo? Itabidi nikutafute tupige road trip.
 
Nilitaka kushangaa gari gani 300km/h. Nyingi ni 180
Zingine 200/220 chache 260! Hilo dude la 300 ni kifo aise!
 
Nilikuwa navuka kwenye Zebra Pale Banda la ngozi jamaa Yuko na Ist kidogo anibutue na matusi juu akanitukana Yuko spidi 120.
Wenzie wote wamesimama ila yeye Sasa
hao ni kukariri tu plate number na kumsaka kimyakimya,....
sicheki na kima, nizingue hadharani , tutakutana sirini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…