Gen 'Z' (Vijana wa 90s na 2000s) nawakumbusha maisha hayasimami "Fainali Uzeeni"

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
🧵 1/ Ndugu zangu, vijana tuliozaliwa kati ya miaka ya 90s hadi 2000s, kuna jambo muhimu la kukumbushana: Maisha hayasimami, fainali uzeeni. Ujana ni kipindi cha misuli, ndoto na kelele—lakini kuna kesho ambayo lazima uiandae leo.

🧵 2/ Tulikulia kwenye vichochoro vya michezo ya kombolela aka uswazi, filamu za kina Van Damme, kuchomana na biki au korosho la moto, kuangalia katuni za benten na sasa tupo zama za mitandao kv Facebook, insta,TikTok nk. Tunapitia mengi na kwa sasa sisi ndo wajanja na tunafurahia—lakini kesho tukizeeka, dunia itatuuliza: una mchango gani? Umlilie nani!? Wifwa peke yako utajijuu!

đź§µ 3/ Maisha sio movie yenye part two. Ukitapanya ujana, hakuna kurudi ku-shoot tena. Usikubali kubaki ukisimulia "enzi zile" ilhali kesho yako haina dira. Tengeneza enzi mpya kwa vitendo vya leo vitendo halisi sio kujipa porojo. Kubeti au kujadili simba na yanga kila wakati na kuwalaumu wanasiasa hakutakusaidia. Mtapeana moyo kumlaumu mwanasiasa ila madhira ya leo na kesho ni ya peke yako. No one will cry with you.

đź§µ 4/ Kwa kila msanii uliyempenda, ulipenda bidii yake. Kwa kila mwanasoka uliyemshangilia, ulipenda mafanikio yake. Je, wewe unajenga mafanikio gani yanayoweza kushangiliwa? Au umebaki mtaani ukijadili maisha ya wengine?

🧵 5/ Sisi millennial ndio kizazi kilichoshuhudia mpito wa analogia kwenda digitali, kutoka kwenye magazeti hadi kwenye memes. Tuna akili ya jana na zana za leo—tusizichezee. Sisi nao tujionye na tujirekebishe bado muda na nguvu tunazo, tuweke uthubutu japo kidogo. Fanya kitu cha maana kabla nguvu haijaondoka kimyakimya.

🧵 6/ Uzee hauji kwa kelele. Utaamka siku moja ukute stamina imeanza kukusaliti, mawazo yana haribu mtiririko na risiti za miili zinaanza kuwasilishwa—bega linauma, mgongo unagoma, usingizi hauna mpangilio, nywele zinakuwa laini na kunyonyoka majukumu nayo yanakuwa mengi.

🧵 7/ Wakati huo utajiuliza: “Nilifanya nini na ujana wangu?” Usikubali jibu liwe “Nilicheka sana”, “Nililala sana”, au “Nilijifanya najua kila kitu”. Jitahidi ujibu, “Nilijituma. Nilijijenga. Nilijenga wengine.” "Ninacho" "nina nafuu"

đź§µ 8/ Hata kama huna kila kitu leo, anza. Soma vitabu. Tafuta maarifa. Wekeza hata kidogo. Omba kazi, anzisha wazo. Omba msamaha. Wekea msingi kesho yako. Uzee ni baraka, lakini unaweza kuwa laana kama haukuuandalia heshima. Mifano mingi ipo inakuzunguka.

🧵 9/ Vijana wa 90s na 2000s—hili ni wito: Tuamke. Usijifunze kupitia machungu yasiyo na ulazima. Usitumie
miaka yako ya 20s au 30s kupotea, halafu uanze kutafuta mwelekeo miaka ya 40 ukiwa umechoka. Kubeti siyo future. Bongo fleva sio future. Udaku wa insta sio future. Hivyo vyote ni "power suckers" yaani "vinyonya nguvu".

đź§µ 10/ Maisha hayasimami, na hakuna fainali ya maisha inachezwa ukiwa mzee. Kila siku ni sehemu ya mechi. Leo unacheza namba gani? Unapigania pointi zipi? Unawajibika kwa timu gani?

🚨 Hitimisho: Ujana si tiketi ya ujinga. Ni nafasi ya kuandika historia. Usikubali kuzeeka ukiwa na maneno, bali uzeeke ukiwa na matokeo. Chukua hatua. Fanya kazi. Jipange.Ukiubishia huu uzi hakikisha unajibishia mwenyewe na siyo mleta sledi pendwa N'yadikwa.

Sledi tayale, wahega!
 
🚨 Hitimisho: Ujana si tiketi ya ujinga. Ni nafasi ya kuandika historia. Usikubali kuzeeka ukiwa na maneno, bali uzeeke ukiwa na matokeo. Chukua hatua. Fanya kazi. Jipange.Ukiubishia huu uzi hakikisha unajibishia mwenye siyo N'yadikwa mleta sledi pendwa.

Sledi tayale
Asante kwa ujumbe, umetupiga kavukavu bila ganzi ila umenyooka sana mwana
 
Uzee unakuja fasta sana ukifika 30 years tu grafu yako inaanza kusoma kwenda chini
 
Moja ya Uzi bora kabisa kwa mwaka huu.

Kesho yetu inatengenezwa/kubomolewa na Tunayoyafanya Leo.

Hata kama unacho leo , usipokuwa nacho makini unaweza usiwe nacho kesho (kazi,afya, nguvu, nk).

Kama hauna Leo, ukifanya bidii na jitihada unaweza ukawa navyo kesho.

Msisitizo ni kwenye Muda.
20's kwenda 40's .
tukifeli hapa. basi 50's tutaishi kwa tabu sana .

Mungu atubariki
 
Vijana ukipita kitaa wanapoteza sana muda kwa kupiga mbanga hazieleweki mtu anapiga mishe za bodaboda hela yote anampelekea muhindi nyingine anahonga mademu ale mbususu.
 
Usi
🧵 1/ Ndugu zangu, vijana tuliozaliwa kati ya miaka ya 90s hadi 2000s, kuna jambo muhimu la kukumbushana: Maisha hayasimami, fainali uzeeni. Ujana ni kipindi cha misuli, ndoto na kelele—lakini kuna kesho ambayo lazima uiandae leo.

🧵 2/ Tulikulia kwenye vichochoro vya michezo ya kombolela aka uswazi, filamu za kina Van Damme, kuchomana na biki au korosho la moto, kuangalia katuni za benten na sasa tupo zama za mitandao kv Facebook, insta,TikTok nk. Tunapitia mengi na kwa sasa sisi ndo wajanja na tunafurahia—lakini kesho tukizeeka, dunia itatuuliza: una mchango gani? Umlilie nani!? Wifwa peke yako utajijuu!

đź§µ 3/ Maisha sio movie yenye part two. Ukitapanya ujana, hakuna kurudi ku-shoot tena. Usikubali kubaki ukisimulia "enzi zile" ilhali kesho yako haina dira. Tengeneza enzi mpya kwa vitendo vya leo vitendo halisi sio kujipa porojo. Kubeti au kujadili simba na yanga kila wakati na kuwalaumu wanasiasa hakutakusaidia. Mtapeana moyo kumlaumu mwanasiasa ila madhira ya leo na kesho ni ya peke yako. No one will cry with you.

đź§µ 4/ Kwa kila msanii uliyempenda, ulipenda bidii yake. Kwa kila mwanasoka uliyemshangilia, ulipenda mafanikio yake. Je, wewe unajenga mafanikio gani yanayoweza kushangiliwa? Au umebaki mtaani ukijadili maisha ya wengine?

🧵 5/ Sisi millennial ndio kizazi kilichoshuhudia mpito wa analogia kwenda digitali, kutoka kwenye magazeti hadi kwenye memes. Tuna akili ya jana na zana za leo—tusizichezee. Sisi nao tujionye na tujirekebishe bado muda na nguvu tunazo, tuweke uthubutu japo kidogo. Fanya kitu cha maana kabla nguvu haijaondoka kimyakimya.

🧵 6/ Uzee hauji kwa kelele. Utaamka siku moja ukute stamina imeanza kukusaliti, mawazo yana haribu mtiririko na risiti za miili zinaanza kuwasilishwa—bega linauma, mgongo unagoma, usingizi hauna mpangilio, nywele zinakuwa laini na kunyonyoka majukumu nayo yanakuwa mengi.

🧵 7/ Wakati huo utajiuliza: “Nilifanya nini na ujana wangu?” Usikubali jibu liwe “Nilicheka sana”, “Nililala sana”, au “Nilijifanya najua kila kitu”. Jitahidi ujibu, “Nilijituma. Nilijijenga. Nilijenga wengine.” "Ninacho" "nina nafuu"

đź§µ 8/ Hata kama huna kila kitu leo, anza. Soma vitabu. Tafuta maarifa. Wekeza hata kidogo. Omba kazi, anzisha wazo. Omba msamaha. Wekea msingi kesho yako. Uzee ni baraka, lakini unaweza kuwa laana kama haukuuandalia heshima. Mifano mingi ipo inakuzunguka.

🧵 9/ Vijana wa 90s na 2000s—hili ni wito: Tuamke. Usijifunze kupitia machungu yasiyo na ulazima. Usitumie
miaka yako ya 20s au 30s kupotea, halafu uanze kutafuta mwelekeo miaka ya 40 ukiwa umechoka. Kubeti siyo future. Bongo fleva sio future. Udaku wa insta sio future. Hivyo vyote ni "power suckers" yaani "vinyonya nguvu".

đź§µ 10/ Maisha hayasimami, na hakuna fainali ya maisha inachezwa ukiwa mzee. Kila siku ni sehemu ya mechi. Leo unacheza namba gani? Unapigania pointi zipi? Unawajibika kwa timu gani?

🚨 Hitimisho: Ujana si tiketi ya ujinga. Ni nafasi ya kuandika historia. Usikubali kuzeeka ukiwa na maneno, bali uzeeke ukiwa na matokeo. Chukua hatua. Fanya kazi. Jipange.Ukiubishia huu uzi hakikisha unajibishia mwenyewe na siyo mleta sledi pendwa N'yadikwa.

Sledi tayale, wahega!
Usimwamshe aliyelala utalala wew hakika navyojua Mimi waandikaji Wengi wazuri na washauri Huwa sio wawekezaji wazuri kabisa utakuta una kanyumba tu kamoja Wenda na chakupangisha jitahidi upande miti hata eka 30 namana uwekezaji wa miti au matunda ni mrahisi sana ila baada ya Miaka 10 utakuwa vizuri
 
Hallucinations, amka, tenda, mada haimhusu mleta sledi, inakuhusu wewe. Hata hivyo unaonekana ushazeeka, huu ni ujumbe wa vijana wa 90s na 2000s wewe kikongwe tulia. Adios
 
Back
Top Bottom