Gen Z wa Tanzania wapewe ajira maana ukosefu wa ajira ni chanzo cha maandamano tunayoshuhudia Kenya na sasa Uganda

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
Wadau Asalam aleykum.

Wanasema mwenzako akinyolewa zako tia maji.

Nawashauri viongozi wangu mlioko kwenye vyombo vya kutunga sera, mfanye kuwaajiri vijana walioko mtaani wenye ujuzi na wasio na ujuzi pia watafutiwe kazi za kufanya.

Hii itawafanya kuwa bize na hivyo kuwasahaulisha na ugumu wa maisha wanaokabiliana nao sasa.

Viongozi wangu, msijiamini kupitiliza kwamba nyinyi mna mifumo imara kuliko huko kunakofuka moto sasa.

Wanasema mwenye njaa mara zote huwa na hasira.

Pia wanasema kama huna kazi ya kufanya, basi chochote kinachokuja mbele yako unaweza kujikuta unakifanya! Shetani huwatumia sana wasio na kazi kutimiza agenda zake ovu.

Maandamano ni kama ugonjwa wa kuambukiza. Mara nyingi nchi nyingi zenye matatizo kama vile Libya, Tunisia, Misri, Sudan, na sasa Kenya na Uganda, maandamano huwa yanaanza kidogo kidogo na baadaye kusambaa nchi nzima!

Kama hali ikiendelea hivi ilivyo, basi tusishangae kuwaona Gen Z wetu nao wakiingia barabarani kuandamana.
Naomba kuwasilisha.
 
hakuna kijana wa bongo atakayeandamana sisi ni maiti toka enzi za nyerere ova
 
Siyo ajira . Watumie vyema tu kodi zetu waache wizi. Magufuli hakuajili mtu ila maemdeleo.ya nchi tuliyaona
 
Kama zile Taarifa zinazotolewa za Kiserikali kutoka Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji; Serikali kuu; Idara na Taasisi mbalimbali ni za kweli kuhusu Ikama; nadhani ipo haja ya kuwaajiri vijana kwani kila mwaka utakuta Taarifa inasema: Idadi ya Watumishi Hitajika ni X, waliopo ni Y kwa hiyo pungufu (X-Y) = Z. Manake ili kusiwe na Uhaba wa Watumishi natakiwa X-Y iwe ni 0. Lakini haijawahi kutokea X-Y ikawa ni 0.
Kila mwishoni mwa mwaka (June/July) maombi ya Ajira mpya huwasilishwa Serikalini na wanaohitaji Watumishi hao ili kuondoa Upungufu(Z) uliopo na Huwekwa katika Bajeti kwa shughuli hiyo ya kuajiri (Ajira zinazoombewa).
Sasa inakuwaje Serikali haikubali kutoa hizo Ajira?? Ufinyu wa Bajeti unakuwaje /unatoka wapi ilhali bajeti zinakuwa zimepitishwa Bungeni? Kama Bunge limeridhia Bajeti manake fedha zipo na zimeruhusiwa kutumika kama zilivyoombwa. Mbona kipengele cha Ajira ndo kipengele kinaleta shida kiutekelezaji tofauti na vipengele vya Miradi na Kile cha Gharama za Uendeshaji (OC)??
Ni kweli ifike mahali tusipuuze lisemwalo - kwani hatujui huko mbeleni kitatokea nini. Serikali yetu sikivu ichukue Tahadhari.
 
Mambo hubadilika Mkuu.
Tusiishi kwa mazoea.
mkuu angalia kizazi kilichopo na miaingi tuliyowekewa.... ogopa sana nchi ya waoganikapewa jina la nchi ya amani.... ogopa sana jamii inayokuzwa ikiamini pesa na mali ndizo huleta maana ya maisha.... uchawa kusifia na kutozingatia mambo ya muhimu ndivyo vimejaza akili za vijana wengi....

niwe mkweli leo watu wakiamua kuandamana mimi nitageuka nyuma kuangalia nina familia nina majukumu alafu nitaishia kusema sijihusishi kwakua nayahofia maisha kulingana na misingi iliyowekwa toka enzi za uhuru...

ni mtazamo tu japo kweli wanaweza badilika ila sio hii gen singeli ya kweli
 
Kenya kuna sababu lukuki nje ya ajira zinazofanya kuandamana.
 
mkuu ajira hazitoki kwakua serikali yetu haina hela.... na kwanini haina hela ni matumizi makubwa ya fedha kwenye uendeshaji wake...

mfano swala kama mwenge lingeweza kulipa watumishi wangapi? japo watumishi hao hao hulazimishwa kuuchangia mwenge kwenye wilaya husika.
ununuzi wa magari ya viongozi unashuhudia msafara wa lc 300 kama 30 zinampitisha kiongozi.
unadhani haya matumizi ni lazima au viongozi wanataka kutuonyesha kwamba hatuna la kufanya?

leo tunakopa nje na bado tumewekwa kwenye nchi maskini zaidi na sio kuwekwa ndio uhalisia

ogopa nchi ambayo wanatenga bajeti ya kununua magari mapya wakati yaliyopo bado yanalipa vizuri tu ninkamfumo ka kujimilikisha kanatafutwa
 
Kenya kuna sababu lukuki nje ya ajira zinazofanya kuandamana.
Ni sahihi kwani Kenya ukiondoa tatizo la Ajira, kuna Siasa, kuna Fitina za ukabila, kuna husda(Chuki binafsi) bila kusahau Ubabe (Mimi ni Mimi; mtafanyaje).
 
Wasingoje ajira za serikali tu, waingie mitaani kwenye sekta binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…