General OMEGA. Siri kubwa ya M23. Maandalizi ya kumkabidhi serikali ya Rwanda

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,692
Reaction score
5,647
Aliekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FDLR, General OMEGA, siku za nyuma, baada ya handaki aliyokuwemo na wenzake kulipuliwa na M23, na kusababisha vifo vya badhi ya walinzi wake, na kuhisiwa kuwa na yeye amefia katika shambulio hilo, alikamatwa na M23 na kuhifadhiwa kwa siri kubwa.

Msemaji mkuu(kaimu), Dr. Oscar Barinda, ametangaza kwamba, M23 inae, na wapo kwenye maandalizi ya kumkabidhi serikali ya Rwanda.
 
Na myaka ya nyuma General James Kabarebe ari mpigia simu na kumwambia hivi;

Omega,watoto wako wote wako hapa Rwanda na Serikali inawasomesha,Kijana wako mkubwa yuko China kwa sasa anasomea engineering, na wewe haujafanya mauaji ya kimbali,Wakati huo wewe ulikuwa Ubelgji unasomea upilot,kwa nini usitoke ndani ya hiyo misitu ukarundi tukasaidiana kujenga hii nchi?

Jibu la General Omega;

General, nakuapia ya kwamba mimi nitarudi Rwanda kukiwa hakuna Mtusi hata mmoja!.
Alikata simu.

Sasa swali watu wengi wanajiuliza; atajibu nini atakapo jikuta Kigali?!!
 
Story za kwenye kanga kuhalalisha wizi wa Rwanda congo
 
Story za kwenye kanga kuhalalisha wizi wa Rwanda congo
Hebu jaribu kuwafahamu FDLR, OMEGA Ndie alikuwa numba tegemezi kwenye uwanja wa mapambano akitegemewa sana na Kinshasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…