Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
- Thread starter
- #61
Mkuu MpendaTz nashukuru kwa maoni yako ingawa kwa sehemu kubwa sikubaliani nayo.
General Tyre iliomba mkopo wa dollar 10 milion kutoka NSSF kwaajili ya kuingiza teknolojia mpya [modernise].Chini ya mpango huo wataalamu walishauri mitambo ya kutengeneza matairi makubwa ilikuwa imepitwa na wakati mno.Basil Pesambili Mramba akatumia wadhifa wake wa waziri wa fedha akaiamuru BOT idhamini mkopo huo pamoja na kubainika wazi General Tyre isingeweza kurejesha mkopo kwa wakati uliokubaliwa kwasababu tayari ilikuwa ikidaiwa na mabank mengine mawili.
NSSF ilianza kutoa mkopo kwa awamu lakini hakuna mashine zilizonunuliwa hata moja badala yake mashine za zamani zikapakwa rangi.Safari za nje ya nchi kwa viongozi [management] zikaongezeka maradufu,wajumbe wa bodi nao wakatumbukia katika ufisadi wa kutisha.Wakopeshaji nao wakaonjeshwa utamu wa fedha badala ya kuingiza fedha kwenye a/c za General Tyre wakabuni utaratibu wa kujinyakua fedha juu kwa juu.Kampuni hewa zikaanzishwa kwaajili ya kutoa ushauri wa kitaalam zikachotewa dollar 1 milion.

Mkuu Ngogo, kwanza nitamke tu kuwa ni vizuri tukaipongeza serikali kwa kuona aibu hii kuwa ni yao na inawapasa kuishughulikia japo wamechelewa sana kuchukua hatua stahiki lakini bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa.
Serikali yetu inaonekana kujali sana siasa badala ya uchumi wa nchi, maana uchaguzi ukiitishwa mahali sasa hivi mf.huko Igunga Mawaziri wanafunga ofisi kwenda kubwabwaja uwongo, kupanga mikakati ya wizi wa kura nk. huku nchi ikididimia. Lakini jambo kama hili linawachukua miaka kumi kujua la kufanya! Hii ni aibu tena fedheha ya hali ya juu.
Kuhusu aliyesababisha kufa kwa GT, sikubali kutajwa mhusika mmoja na ninaomba katika mambo mazito kama haya watu wasiwe wanadanganya wananchi eti Waziri mmoja kaamua kuua shirika au kampuni muhimu kama hiyo yey peke yake. Yeye ni nani? Wala hakuwa Raisi wa nchi. Kuna baraza la Mawaziri linaloongozwa na Raisi, je maamuzi kama haya anaweza kuyafanya mwenyewe kweli? La hasha! na tuache mzaha kwenye mambo yanayolihusu Taifa. Huu unakuwa mzaha mwingine kama ule wa juzi hapa eti Raisi anasema mhasibu mmoja alifanya kosa katika ununuzi wa rada, eti mhasibu alikosea. Tafadhali sana sababu dhaifu kama hizi zisiletwe humu. Au wale waliotaka kuhamisha mabilioni kutoka hazina eti kwenye lori kwenda wizara ya mambo ya nje, eti walijiwekea saini na kuidhinisha kuondoa kiasi hicho bila kuwa na authority ya kufanya hivyo. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Serikali makini haiwezi kuwa inawapa wananchi wake sababu za kijinga jinga namna hii. Tunakuwa kama tunaongozwa na wapiga ramli na wacheza kamari?
Hivi visingizio uchwara lazima vikomeshwe na njia mahsusi ya kwanza ni kuhakikisha CCM inakaa benchi kwanza kwa miaka kadhaa, maana kwao limezoeleka ni kama utamaduni wa chama.
Last edited by a moderator: