Devendra Lohani anatoka katika ukoo wa kifalme Nepal, alikwenda Marekani kwa ajili ya masomo lakini pia alikimbia vita vilivyokuwa vikiendelea nchini Nepal kwasababu kulikuwa na sheria iliyowalazimisha vijana kujiunga na jeshi ili kupambana na wapinga utawala wa kifalme wa Maoist.
Devendra Lohani alitumia fedha nyingi za GTEA {pamoja na fedha za mkopo wa NSSF $10,000,000} kumsaidia mfalme Gyanendra wa Nepal {Hindu kingdom} dhidi ya Maoist lakini hatimaye walifanikiwa kumaliza utawala wa kifalme may 2008.
Mwaka 2004 vijana 23 wa kinepal waliletwa Tanzania na mfalme Gyanendra kwaajili ya kupata mafunzo ya kijeshi TMA – Monduli, Rtd lt col Muro alipewa jukumu na Devendra kuandaa utaratibu wa kuwaingiza chuoni Monduli.
Kulikuwa na kila dalili ya mpango kushindwa kwasababu vijana wa kinepal hawakuwa wanajua lugha ya kiingereza pia taratibu za kiserekali hazikufuatwa kabisa, mipango ya kuwapatia ajira hapa Tanzania ikafanyika kwa kuwachomeka kwenye department mbali mbali GTEA na wengine wakapelekwa Clock Tower service center na Tanzanite One Mining kwa kazi za kuziba pancha na ulinzi respectively.
Wafanyakazi wa GTEA waliona ajira zao ziko mashakani wakaamua kutoa taarifa Uhamiaji, napenda kuwapongeza hawa jamaa wa uhamiaji kwa kazi nzuri kwasababu baada ya kupata taarifa wanepal walirejeshwa kwao baada ya muda mfupi lakini wanepal waliopelekwa Mererani {Tanzanite One Mining} mpaka leo wapo wanafanyakazi ya ulinzi.
Devendra Lohani aliwahi kututamkia wafanyakazi muda si mrefu Nepal ingefungua ubalozi Tanzania na yeye angekuwa balozi ,kwamaneno yake mwenyewe alitoa msaada kwa mfalme Gyanendra kwa matazamio ya kupewa ubalozi.
Inashangaza mtu wa aina ya Devendra Lohani pamoja na uovu wote mpaka leo anapata wapi uwezo wa kufanya mawasiliano na ofisi ya waziri mkuu,waziri wa fedha,waziri wa biashara, viwanda na masoko,ina maana idara ya usalama wa taifa imelala!
Usalama wa taifa inavyoonekana kazi yao ni ulinzi wa viongozi tu, ni vizuri usalama wa taifa wakaona umuhimu wa kulinda uchumi wetu pia kwasababu kufungwa kwa kiwanda cha General Tyre kumeambatana na athari kubwa kiuchumi.
Hakuna ubishi kwamba General Tyre ilikuwa ikilipa kodi VAT 150 milioni kwa mwezi, direct employment 400, indirect employment 1500, tumepoteza soko la matairi Kenya, Somalia, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi na Malawi