Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,125
- 7,373
Acha kilitex mkuu kuna baby biscut kuna kiwanda cha kutengeneza sillingboard, camartec, tanzania litho, nmc kiwanda cha maziwa aisee jamani..!!
MASTER PLAN unaufunga mjadala huu wa viwanda km NANIKwa sababu mdau kauliza na majibu yametolewa hivyo mjadala unafungwa rasmi. Kuna mwenye swali la nyongeza?
Ngongo hivi mtu akitaka kuifufua general tyres anahitaji mtaji arround kiasi gani? Na aangalie nini hasa ili apate faida?
Nimewaza nikinunue siku moja
Mkuu Bavaria ukitaka kuifufua General Tyre mambo yafuatayo ni lazima yafanyike.
Mosi,Utahitaji kuwarejesha wafanyakazi hasa wa kitengo cha uzalisha kwa 90%
Pili,Utatakiwa kuandaa fedha kwaajili ya ununuzi wa raw material si chini 1 billion.
Tatu mashamba ya mpira moja ya raw material muhimu ambayo yalikuwa yakihudumiwa na GT yatatakiwa kurejeshwa chini ya kiwanda ili kupunguza gharama za kununua mpira nje.Hivi sasa Yana ya Kenya wananunua mpira karibu na bure.
Nne,Serekali lazima ianze kuzuia matairi kuingia soko la Tanzania holela.Hichi ndio kizungumkuti kwasababu utakuta GT inalipa kodi zote kuanzia raw material and etc lakini waagizaji & wasambazaji wanakwepa kodi matokeo yake tairi linalozalishwa ndani linakuwa na bei kubwa.
Kulikuwa na Coffee Curing pale Moshi na Tanalec kule Arusha, hivi navyo vinajikongoja au vilishakufa?
Kibo Match pale Moshi kipo mochwari sasa hivi.
Breweries aahh inauma ...
***2015 operation Delete CCM*** basi
Coffee Curing bado kipo kinajikongoja na mitambo yao iliyopitwa na wakati. Ila Kibo Match na Kibo Paper tayari tumeshavisahau, mwaka juzi katikati ndio walivifunga rasmi kama kumbukumbu zangu ziko poa mana walikua na deni kubwa sana kwenye benki moja hapa TZ na yote hayo yalisababishwa na ubovu wa Board members hasa mwenyekiti ambae alikua anachukua mafungu kuendeleza shule yake pale Moshi, yule Mnaijeria mwenye kiwanda alikua akituma pesa ila hazifanyi mambo ya maana na still walikua wanachukua mikopo isiyotumika ipasavyo mpaka hawakuweza kulipa wafanyakazi kuanzia hapo ndo ukawa mwisho wake.
Mkuu Mimi niliwahi kufanyakazi General Tyre so kila hatua ya kuifisadi na kuizika niliiona kwa macho yangu mawili.
Kwanza nakunusha kwa sauti kubwa hakuna mold (kinu) cha kupika tyre kilichohamishiwa Yana Kenya.Kilichofanyika ni kuhamisha technologia ya kutengeneza tyre baadhi ya sizes hasa 7.50 - 16 HCT 10 PLY ambayo ilikuwa na soko kubwa Tanzania,Congo DRC,Somalia na Kenya kwenyewe.
Kilichofanyika enzi za Mzee wa uwazi na ukweli ni kumruhusu aliyekuwa mkurugenzi mkuu Devendra Lohani kufanya anavyotaka ikiwa ni pamoja na kupewa mkopo mkubwa kutoka NSSF U$ 10 Million kwaajili ya kumodernise (mitambo ya kisasa) halikufanyika hata kidogo na bado maengineer & technician wakalazimishwa kuuza formula ya kutengeneza hiyo tyre ambayo msomali mpenda vita alikuwa akiifunga kwenye Land Cruiser p/u na mtutu wa bunduki kubwa alikuwa na uhakika na tyre za general tyre zitafanya kweli.
Enzi hizo hakuna gari iliyokwenda Manyara,Ngorongoro,serengeti bila kufunga 7.50 - 16 SHCT 12 PLY au 10PLY.Demand ilikuwa kubwa mno ikabidi General tyre mabor msumbiji watupatie mold za 7.50 - 16 HCT ili kukabiliana na mahitaji makubwa.Pamoja na kuzalishwa kwa siku zaidi ya 1,350 bado ilishindikana kukidhi mahitaji.
Kuona hivyo YANA wakatumia pengo la uongozi na uadilifu wakaanza kuzalisha 7.50 - 16 yenye profile sawa na General Tyre na wakati huo huo juhudi kubwa za kukifunga kiwanda cha General Tyre ambayo ilikuwa chini ya mwenyekiti wa bodi Shelukindo William zilikuwa zikipamba moto.
Mungu mkubwa 7.50 - 16 YANA siku hizi imekumbana na kichapo cha ukweli kutoka Goodride 235 / 85 R 16 tubeless kutoka China imeiondoa kwenye soko kiasi kikubwa.Magari mengi ya utalii siku hizi yameachakufunga YANA kutokana na kukosa ubora na bei yake kuwa juu.
Tanzania ya Mwl Nyerere tutaikumbuka sana.
Hii hatari sana na tukiwaachia utawala watauza hadi ikulu kama kigamboni wameshauza tayari