Gentamycine naomba kukuuliza kuhusu hili la Yanga, Coastal Union na GSM

Itovanilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
2,314
Reaction score
5,150
Wasalaam wanabodi

Sina neno, niseme tu kwamba Mimi ni shabiki na mwanachama halisi wa Dar es salaam Young African

Kuna uzi upo humu ambao umeanzishwa na member mwenzetu humu, akionekana kujua mengi kuhusu mpira wa kibongo kama si ujuaji tu.

Uzi unaituhumu timu ya Coastal union kwamba watafungwa tu, kwakuwa tayari GSM washatoa mlungula huko Tanga.

Maswali yangu,

Je, wewe Gentamycine umeangalia mechi kati ya Coastal union na Yanga?

Je, umeona na kujiridhisha aina ya magoli yaliyofungwa na wachezaji tegemeo na wenye kulazimisha matokeo?

Ushauri wangu kwako ni kwamba punguza ujuaji au jiongeze, siyo Kila habari unayoisikia unakimbilia kuileta humu.

Vinginevyo unajiaibisha tu,

Coast wamecheza vizuri tena walipania lakini ndio hivyo Tena,

Wamecheza lakini magoli kapata Yanga.
 
Mkuu, Binafsi nakupongeza sana kwa kwa huu ushauri wako juu ya Huyu bwana Mkubwa GENTAMYCINE, Nami niongeze kitu hapa. kwanza ni-declare my interest licha ya Mimi kuwa ni Shabiki wa Yanga mpaka rohoni Ila ukweli lazima usemwe, Huyu bwana Mkubwa amekuwa mstari wa mbele kila siku kuinanga Yanga au timu fulani tena kwa shutuma kwamba Yanga wamehonga timu pinzani ili iachiwe ishinde. Kuna nyuzi zake nyingi zenye maudhui Kama hayo kwa match karibia zote anazocheza Yanga.

Lakini licha ya propaganda zake zote hizo Yanga yetu inacheza kwa juhudi na kupata Matokeo mazuri kabisa, Mwanzo kabisa nilidhani Huyu bwana Mkubwa ni mtu anayeujua sana Mpira wa miguu Ila kwa sasa nimem-devalue kabisa na kumuona Shabiki maandazi na Asiyejua lolote kuhusu Mpira au Kama sivyo basi ana Chuki tu na Timu ya Wananchi.

Yanga hii kama mtu anaifuatilia vizuri iko na mapambano sana uwanjani na inatumia mbinu zote kupata Matokeo, Pia jitihada za Timu pinzani tunaziona namna wanavyopambana na Yanga, Rudi kwenye machi ya Yanga na Biashara, Dodoma Jiji, Mbeya kwanza, na Hii ya leo dhidi ya Coastal union.. hv kama kweli mtu unaangalia vizuri Mpira unaweza Kusema ety Yanga wanahonga Timu pinzani.? Ila tu ukubwa wa Yanga na jitihada zake ndo zinatoa Matokeo.

Kiupande wangu hata ni kama Shabiki wa Yanga Ila Simba ikipambana na kucheza vizuri uwanjani siwezi ku-undermine ety wamenunua match Hali ya kuwa mapambano nimeyaona maana hii michezo si uadui.

Sasa nami ni muambie tu bwana Mkubwa hii Tabia anayoiendekeza si Ushabiki kabisa, pia si utani Ila ni CHIKI NA NONGWA iliyokithiri, ifike kipindi kila mtu a-stick kwenye mechi zake yanini tufuatiliane.
 
Kaa tayari na makala refu la full pumba lililojaa ujuaji,majivuno na matusi juu dhidi yako
Sasa kama huna Akili, utaanze kuwa Mjuaji, Mjivuni na Mbobezi wa Matusi / Shombo?

Mimi ndiyo GENTAMYCINE ( alias ) Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer au Le Ange Adorable ( Malaika Ninayeabudiwa )

Na nitawakera mpaka mpasuke Mfariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…