Nitakuwa wa mwisho kutokuamini kuwa Mleta Uzi siyo ama Mmoja wa Watangazaji au Mchambuzi wa EFM Sports Headquarters.
Kuna mahala fulani hivi katika Maelezo yako umeshindwa Kujificha hasa uliposema kuwa Wenzake Studioni wanamchora tu, anajifanya ni Mtu wa Afrika Kusini na anajidai kuwa anajua mno Kiingereza.
Usichokijua tu ni kwamba huyu ( huyo ) Mchambuzi Geof Leah ni mwana Simba SC kindakindaki na Yeye ndiyo Mchambuzi wa Kwanza Tanzania nzima Kujiweka wazi ( Kujipambanua ) hivyo.
Kuhusu Maisha yake ni kwamba Geof Leah hatokei katika Familia Duni na ni Mtoto wa Kishua sana, akiishi Ushuani na ametembea, amesoma na kuishi nchi nyingi kutokana na Kazi ya Baba yake Mzazi hivyo kote huku kumemsaidia kumpa Exposure Kubwa ya mambo mengi ambayo kwa Waswahili baadhi msio na Upeo hili limekuwa ni Kero na Chukizo Kwenu.
Hoja yako kuwa anajifanya anajua sana Kiingereza imekaa Kipumbavu sana kwani hakuna aliyekuleta hata Wewe pia Kukijua vyema tena hata Kumzidi kama ukiamua Kujifunza na kila Siku Mwalimu Ras Simba anawatangazieni Redioni msiojua vyema Kiingereza akawafundisheni pamoja na wale wa British Council Posta.
Watanzania wengi mna Dhambi kubwa mno na iliyojaa Wivu na Chuki ndani yake hasa kwa Watu ambao huwa siyo Wanafiki kama huyo Mchambuzi Geof Leah, Wakweli na walio na Utajiri wa Knowledge na Exposure na sijui ni kwanini hambadiliki.
Hata hapa JamiiForums kuna Member Mmoja ( nimemsahau ila mnaomkumbuka mtamtaja kwani ni Maarufu sana ) na nasikia kapigwa BAN huwa ni Mtu mwenye Kuyajua mengi, huyasema mengi, hufafanua mengi, huchambua Masuala vyema na ana Maarifa mengi, Mjenga Hoja mzuri, Mchokoza Mada, ana Uwasilishaji wa Kipekee JamiiForums nzima ila cha Kushangaza badala ya Kumuelewa na hata ku appreciate tu Kipaji chake ( Talanta yake ) ndiyo amegeuka kuwa Chukizo kwa Wapumbavu wengi ( siyo Wote ) mpaka Wanamtukana, Wanamdhihaki na wanamtafutia BAN za Makusudi ili Kumzima na Kufifisha Umaarufu wake wakati kumbe ndiyo Kwanza anakuwa tu Kiumaarufu kiasi kwamba hata ID"s zingine hapa zinahusishwa / zinafananishwa nae.
Badilikeni.