Katika maswala yanayotajwa sana midomoni mwa wafuatiliaji wa maswala ya kisiasa nchini, ni kwamba CCM wameamua kuongeza juhudi ili kuhakikisha jimbo la Kawe linarudi kwenye himaya yao na kuangusha "mbuyu" ,Halima Mdee.
Swala kubwa la kujadili baada ya hiyo arafa ni Nani atapewa dhamana ya kupeperusha bendera ya kijani yenye nembo ya jembe na nyundo.
Kwa mwenendo wa siasa za Kawe, anahitajika mtu mwenye mvuto, muadilifu, kijana na mwenye nia ya kuwatumikia wana Kawe. Na katika andiko hili nitawatajia mtu ambae ni "Dark Horse" of the race, yaani yule ambae atafanya makubwa na hakuna ambae anamtarajia. Ila kwanza tuanze na kwanini Kawe inaweza kurudi CCM?
Halima Mdee ni kiongozi hodari, thabiti na muhimu kwa taifa kwa ujumla. Ameshiriki katika kuibua majadiliano ya matukio makubwa kabisa kutikisa hii nchi na amekuwa mwiba mchungu kwa baadhi ya mafisadi wa nchi hii ambao hatuwezi kataa kuwa baadhi yao wako au wanahusiana moja kwa moja na chama tawala.
Lakini Halima akiwa anatumikia taifa kwa mawanda mapana, aliwasahau wananchi waliomuweka kwenye nafasi aliyopo. Citizens of Kawe missed their representative rights, they are sacrificed for other purposes.
Kama Mbunge ameshindwa kuwakilisha kero za wana Kawe za kila siku, Nani hajui kuhusu kadhia wanazopata wakaazi wa Makongo Juu? Nani afahamu kuhusu huduma mbovu za afya jimboni hapo? Najua itaibuliwa hoja ya "Hivi unajua kazi ya Mbunge?" Ndio naijua, ila apart from kusema tu pale Bungeni which apparently every one can do, which other initiatives alizochukua publicly kuonesha nia ya kutatua baadhi ya hizi kero? At least basi ile kuonesha ulijaribu kuchukua other counter measures? Mtauliza hizo counter measures ni zipi...sasa hio ndio kazi ya Mbunge.
Kawe missed Halima.
Sasa nani wa kumrithi Halima? Ofcourse atatoka Chama Cha Mapinduzi. Kumekuwa na majina mengi sana yanayotajwa tajwa midomoni mwa viongozi Chama wa Jimbo la Kawe. Nimesikia majina kama Nyambari Nyangwine, Faustine Mwenda, Kipi Warioba,Furaha Jacob ambae yeye alikuja kwa style ya kusema "ameagizwa na Mwenyekiti" na recently Bishop Gwajima who indeed inabidi tuanze kushangaa. Mwaka 2015 alifanya siasa chafu za kumchafua mwenyekiti na chama, alikuwa anasupport harakati za vyama vingine. Je ni lini aliitwa na kamati ya maadili kujibu makosa yake? Au hakuitwa kwa sababu Chama kilikuwa hakimtambui kama mwanachama? Yote haya tutapata majibu baadae.
Sasa nani unadhani ndie my "Dark Horse" of this race? .
Geofrey...Geofrey Timoth, Remember that name. Huyu jamaa anafanya calculated moves. Anajipambanua kiakili sana, hana haraka na mambo yake, kila jambo analofanya linaonekana ni limeamuliwa na timu yenye umakini mkubwa.
Geofrey Timoth, ama nimuite "Mjamaa Wa Kawe" kama anavojitambulisha sina details zake nyingi sana ila nafahamu amewah kuwa mtumishi wa Shirika la NSSF na sasa anajishugulisha na shughuli za ufugaji wa Kuku kupitia mradi wake wa "Timoo The Farmer"
Jamaa ni mjamaa haswa, ukikaa nae hata nusu saa tu kumsikiliza unajua what kind of a person are you talking to. Ana mipango mikubwa sana na anajiamini, ana heshima na anatreat kila mtu with utter most respect. Nikiwa kama mdau wa Jimbo hili niseme nimemfuatilia kimya kimya bila hata kujitambulisha kwake lakini nimevutiwa na ari yake ya kutumikia wananchi.
Halima won't be easy, lakini 2015 alirudi bungeni on the endorsment ya wanaCCM wenyewe ambao walijikuta kwenye makundi ambayo yalikigawa chama ndani ya Kawe na hatimae kushindwa kumsupport mgombea wa CCM kipindi kile , Kipi Warioba. On a United CCM, Halima doesn't stand a chance na baada ya kuvurunda kuwawakilisha basi kazi itakuwa nzito kwake.
My Dark Horse is Geofrey Timoth. Tukutane October 2020 ...Amini nawaambieni, kama CHADEMA watamsimamisha Halima Mdee tena , basi Mjamaa Wa Kawe will be a daily nightmare to my sister Halima.
Geofrey Timoth ni muadilifu,Mwenye Nia na Wana CCM wa Kawe wameanza kuimba kiitikio hicho.