Geographia ya SUA

gagarichaa

Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
38
Reaction score
2
Wakuu salam zenu ningependa kujua chuo cha sua kipo katika geographia gani nikiwa na maana umbali kutoka mjini,mazingira ya chuo kwa ujumla..nk....karibuni mnisaidie kwa mnaokifaaham iki chuo.

Natanguliza Shukraan
 
kama km 1.5 toka mjini mazngira yako poa sana.Karibu SUA mkuu.
 
wakuu salam zenu ningependa kujua chuo cha sua kipo katika geographia gani nikiwa na maana umbali kutoka mjini,mazingira ya chuo kwa ujumla..nk....karibuni mnisaidie kwa mnaokifaaham iki chuo asanteni sana..
SUA iko katika mkoa wa Katavi, yapata km 20 kutoka mji mdogo wa Ifakara. Chuo kinatoa shahada za uzamili na uzamivu tu katika taaluma ya ukunga. Chuo hiki kilianzishwa na marehemu Nelson Mandela alipoitembelea Tanzania mwaka 1984.
 
SUA iko katika mkoa wa Katavi, yapata km 20 kutoka mji mdogo wa Ifakara. Chuo kinatoa shahada za uzamili na uzamivu tu katika taaluma ya ukunga. Chuo hiki kilianzishwa na marehemu Nelson Mandela alipoitembelea Tanzania mwaka 1984.

ipo day tutafika!
 
wakuu salam zenu ningependa kujua chuo cha sua kipo katika geographia gani nikiwa na maana umbali kutoka mjini,mazingira ya chuo kwa ujumla..nk....karibuni mnisaidie kwa mnaokifaaham iki chuo asanteni sana..

SUA halisi ipo kandokando ya safu za milima ya uluguru eneo moja maarufu kwa jina la KIDIDIMO mjini Kasoro bahari kwa Waluguru huko Morogoro, ni KM 5 toka Msamvu stend ya Mabasi ya Mkoa. Usafiri kutoka Msamvu kwenda SUA direct ni TAX tu bei 5000/= pikipiki 3000/= au daladala 400/= mpaka mjini kati, ukishuka unaelekea soko kuu huko ndo parking ya gari za kwenda Sua zilipo ni Minibus nauli ni 500/= dakika 10 tu umeshafika SUA main campus huko barabara ni za lami tu, nchi iliyofunikwa na Kijani kibichi tu msimu wote, kila aina ya Mazao ipo huko, mfano ukienda Horticulture Unit huko utafikiri ndo Edeni ya Biblia, jinsi miti ya matunda ya kila aina ilivyozaa na maua mengi, mboga za majani za kila aina zipo huko.

First year, wanafikia Solomon Mahlangu Campus hii ipo Mazimbu, 7Km from Msamvu stendi. Huko ni kambi za kijeshi za Wapigania uhuru majemadari wa South Africa. Huko kuna umeme wa aina yake ambao hutaona nguzo hata moja kwenye hiyo Campus ila upo kila hostel kule zinaitwa Unit 1-6 na Freedom Square hapo ndo meeting place ya Mitihani kila jumapili, Maelezo haya ni kwa hisani ya matembezi ya 2007 hivyo kwa sasa kunaweeza kuwa na mabadiliko ya kigeografia zaidi maana binadamu ndiye anayeharibu miundombinu.

Wasomi wa SUA hawajatekwa na ulimwengu wa mitandao ya kijamii, wala shamrashamra za kuhudhuria matamasha ya miziki wkend, mkuu kule ni kitabu tu, ukifika utaipenda SUA, utasoma kwa raha na hofu ya kudisco itakuwa begani mwako kila uamkapo.
 

Attachments

  • 1411529972107.jpg
    29.7 KB · Views: 337
  • 1411529984852.jpg
    40.5 KB · Views: 321
nashukuru sana kwa maelezo....vip kuhusu maisha ya ndani ya chuo...
 
kariiibu mlogolo!!!!!
U will enjoy being at SUA
 
nashukuru sana kwa maelezo....vip kuhusu maisha ya ndani ya chuo...

Life style kule ni zuri sana, chakula bei nafuu, kipo kwa wingi aina zote. Maji mengi ya kutosha main na mazimbu pia hakuna uhaba wa maji, isitoshe wsnachuo wengi kule ni wacha Mungu kwahyo baada ya lecture tu mchana hupanda juu milimani kusali kwa kule Mazimbu, hakuna maisha ya ulimbukeni na kujionyesha sana ufahali kama vyuo vingine hususani Dar,. Isitoshe jamii ya kule ni ya mchanganyiko watu wazima 40 yrs wakitafta first degree na vijana wa 20 yrs, yeah kitu kama hicho
 
kwaiyo maisha yakule ni maisha mazuri sana kwa kijana wa sasa...especialy in this global world...nashukuru mungu kwan aya ndio maisha i dremt of....vip irrigation and water resources ingeneer...
 
Hivi civil engineering ya hapo ikoje?

Civil Eng.. Sua haipo ila kuna Agricultural Engineering hii ni nzuri ila utakuta wanaume ndo wengi girls wanaweza kuwa 3 tu. Ni nzuri unajifunga kufunga jembe la trekta ukiwa farm, vitu kama hivo. Huko hesabu za kina Prof Sembuche, nyingi tu
 
Sua kuna digrii nyingi sana zipo za Nyuki, Mboga, Kupika, Kutandika vitanda, sayansi ya Lishe, na nyinezo sikuhizi nimeskia eti kuna Geomatics, teheee tehee chezea ulimwengu wa GIS Spatial Mapping duuu haya ni mambo ya UCLAS a.k.a ARU.
 
Civil Eng.. Sua haipo ila kuna Agricultural Engineering hii ni nzuri ila utakuta wanaume ndo wengi girls wanaweza kuwa 3 tu. Ni nzuri unajifunga kufunga jembe la trekta ukiwa farm, vitu kama hivo. Huko hesabu za kina Prof Sembuche, nyingi tu

Niliangalia kitabu cha TCU nikaiona hiyo course ya civil ndomana nikauliza.
 
Niliangalia kitabu cha TCU nikaiona hiyo course ya civil ndomana nikauliza.

Kozi mpya hiyo basi mkuu mi TCU siijui, umri ulishapita wa kuvist hiyo web,,,, basi sasa chuo kitakuwa na zaidi ya kozi 70 ni noma aiseee na hizi division five coz pale first yr laxima usome Physical Chemistry na wengi huwas wanafeli na kudisco mwaka wa pili semester ya kwanza coz kafeli three times hiyo physical vhemistry ya akina Prof Nkoma, Elisante, Tungaraza na wenginro wapya wa sasa hivi
 
mwambieni ukweli pakoje mbona mnaficha baadhi ya mambo ya sua, yangu ni haya,
Pale SUA only one mistake ni kudisco au kusapua, mitihani hadi jumapili, tena j'pili asubuhi. Maisha ya pale ni full presure na stress nyingi sana... Degree ya SUA nazani zinatakiwa ziwe masterz, ngumu kinoma hadi malecture wa pale wagumu kinoma furaha yao ni kumdisco mtu hawana ubinadamu wala huruma linakuja swala la kumdisco mtu, wee fikiria somo moja lecture mmoja anakudisco semister ya sita/mwaka wa tatu mwishoni.
 
Bzimana SUA ukabila na Chuki na Wivu ndo mijeledi iliyopo pale ukizingatia wahadhiri wengi pale ni akina Shomire, sasa ole wako uwe Mhehe na kwenye Baraza la Senate kutetea disco hakuna mnyalu, unategemea utatetewa na nani. Ndo sifa za kijinga za SUA,
 
Last edited by a moderator:
sio first year wote wanaripoti mazimbu campus! koz kama bvm, animal science, general agriculture, food science n.k wao wanaripoti main campus
 
sio first year wote wanaripoti mazimbu campus! koz kama bvm, animal science, general agriculture, food science n.k wao wanaripoti main campus

Unasema hivo baada ya kukamilika ujenzi wa hostel mpya pale Mbuyuni iliyofunguliwa na Mkapa kama sikosei ndo availability ya Accomodation na lecture theatre kuongezeka, lakini uliza miaka ya nyuma ilikuwaje pitia maoni vizuri mkuu, tunapeana updates tu, Lakini chuo chenu ni hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…