Geographia ya SUA

Geographia ya SUA

Hivi ule mpango wa kubadili jina la chuo kutokea Sokoine University of Agriculture to Sokoine University umeishia wapi? Kwani walisema haitakuwa inatoa "Agricultural based" degree bali ni degree zingine pia.
 
Ha ha ha...so SUA ni hatari wanatoa watu walioiva kikweli kweli kwenye fani zao... asanteni wakuu
 
Ha ha ha...so SUA ni hatari wanatoa watu walioiva kikweli kweli kwenye fani zao... asanteni wakuu

Furaha iliyopo SUA ni kuwa unaweza anza fist yr mpaka unamaliza 3yrs hujabahatka kuongea na Dr, Prof, may be academic advisor wako, kwahyo unakuwa hujaiva vizuri, maana seminar presentation baadhi ya coz hakuna. Majembe ni vijsna wa ARU aiseee fisrt tu unajikuta umeshasimama mbele ya panel wapo Dr, Prf, unapresent vitu vyako
 
Naombeni anaeijua bach of food science and technology anijuze kindani

Jiandae practical za kupika jikoni, raha ilioje jamani degree za mapishi na sayansi ya lishe aisseeeee
 
Naombeni anaeijua bach of food science and technology anijuze kindani

Hii koz inahusiana na production, processing,storage and analysis of food in general kama we umechaguliwa hii koz nipm no yako nikuelekeze kwa undani!!
 
SUA halisi ipo kandokando ya safu za milima ya uluguru eneo moja maarufu kwa jina la KIDIDIMO mjini Kasoro bahari kwa Waluguru huko Morogoro, ni KM 5 toka Msamvu stend ya Mabasi ya Mkoa. Usafiri kutoka Msamvu kwenda SUA direct ni TAX tu bei 5000/= pikipiki 3000/= au daladala 400/= mpaka mjini kati, ukishuka unaelekea soko kuu huko ndo parking ya gari za kwenda Sua zilipo ni Minibus nauli ni 500/= dakika 10 tu umeshafika SUA main campus huko barabara ni za lami tu, nchi iliyofunikwa na Kijani kibichi tu msimu wote, kila aina ya Mazao ipo huko, mfano ukienda Horticulture Unit huko utafikiri ndo Edeni ya Biblia, jinsi miti ya matunda ya kila aina ilivyozaa na maua mengi, mboga za majani za kila aina zipo huko.

First year, wanafikia Solomon Mahlangu Campus hii ipo Mazimbu, 7Km from Msamvu stendi. Huko ni kambi za kijeshi za Wapigania uhuru majemadari wa South Africa. Huko kuna umeme wa aina yake ambao hutaona nguzo hata moja kwenye hiyo Campus ila upo kila hostel kule zinaitwa Unit 1-6 na Freedom Square hapo ndo meeting place ya Mitihani kila jumapili, Maelezo haya ni kwa hisani ya matembezi ya 2007 hivyo kwa sasa kunaweeza kuwa na mabadiliko ya kigeografia zaidi maana binadamu ndiye anayeharibu miundombinu.

Wasomi wa SUA hawajatekwa na ulimwengu wa mitandao ya kijamii, wala shamrashamra za kuhudhuria matamasha ya miziki wkend, mkuu kule ni kitabu tu, ukifika utaipenda SUA, utasoma kwa raha na hofu ya kudisco itakuwa begani mwako kila uamkapo.

Nauli kutoka stand ya SUA to main campas kwa pikipiki ni 2000TSH-3000TSH hapa inategemea na bageini yako!! na nauli ni 400 kwa haice ila kwa bajaji ni 500 kama mkiwa wanne na 2000tsh kama uko mmoja!!! aisee hizo picha zimenikumbusha sana SUA!!!
 
kwaiyo maisha yakule ni maisha mazuri sana kwa kijana wa sasa...especialy in this global world...nashukuru mungu kwan aya ndio maisha i dremt of....vip irrigation and water resources ingeneer...
Irrigation and water resource engineer sio kozi bali ni mtu aliyesoma irrigation and water resources engineering, hiyo kozi utajifunza mengi kuanzia uchumi, biashara, maths na engineering in its details!!
Hivi civil engineering ya hapo ikoje?
SUA hakuna civil engineering as civil engineering bali kuna water resources kama branch ya civil...
Civil Eng.. Sua haipo ila kuna Agricultural Engineering hii ni nzuri ila utakuta wanaume ndo wengi girls wanaweza kuwa 3 tu. Ni nzuri unajifunga kufunga jembe la trekta ukiwa farm, vitu kama hivo. Huko hesabu za kina Prof Sembuche, nyingi tu
sio hilo tu mpaka ujenzi na ku design structures kama nyumba, madaraja, machines and the alike!!
Sua kuna digrii nyingi sana zipo za Nyuki, Mboga, Kupika, Kutandika vitanda, sayansi ya Lishe, na nyinezo sikuhizi nimeskia eti kuna Geomatics, teheee tehee chezea ulimwengu wa GIS Spatial Mapping duuu haya ni mambo ya UCLAS a.k.a ARU.

Sorry huifahamu SUA!!
 
SUA pasikie tu, baadhi ya malecture hawana utu wala mzaha linapokuja suala la kuhitaji huruma..
Mnaokwenda pale mjiandae, wanafunzi wa pale wanahofu hofu tangu siku ya kuripoti hadi ya graduu
 
Ukisema wahadhiri wengi wa SUA ni kina Shomire utakuwa unakosea maana SUA ni taasisi kubwa yenye vitivo na idara kadhaa. Nakushauri ukarejee kufanya tafiti zako ili ujue ni katika idara/vitivo gani ratio ya hao kina shomire ni kubwa au ndogo ukilinganisha na wengine. Hii ni kwasababu zipo baadhi ya idara huwezi mpata mhadhiri wa namna hiyo na hata kwenye senate hali yaweza kuwa hivyo hivyo. Ebu nikuulize, ulipofanya huo utafiti wako uligundua SUA ina wahadhiri wengi wa Mkoa gani? ACHA MASUALA YA KUJA KUONGELEA UKABILA KWENYE MAENEO KAMA HAYA, HATA KAMA HAO KINA SHOMIRE NI WENGI BASI NI PONGEZI KWAO NA WENGINE INABIDI TUJIFUNZE TOKA KWAO SIYO KULALAMIKA MARA UKABILA, UKANDA, UDINI. HII NI SAWA NA CHURA APIGAVYO KELELE KANDO KANDO YA DIMBWI LA MAJI UKIMSOGELEA ANANYAMAZA.

baba yako ni DVC nini.? Mbona unapatetea sana hapo sua, sema ukweli bana, acha kuficha mambo.
 
nivizuri kupeana moyo nakushauriana katika njia njema nasio kukutishaana tamaaa wakubwa kwan chuo tunaenda kufata nini zaidi ya elimu bora sasa kama kaka zetu mtushauri vizuri tafadhali
 
Furaha iliyopo SUA ni kuwa unaweza anza fist yr mpaka unamaliza 3yrs hujabahatka kuongea na Dr, Prof, may be academic advisor wako, kwahyo unakuwa hujaiva vizuri, maana seminar presentation baadhi ya coz hakuna. Majembe ni vijsna wa ARU aiseee fisrt tu unajikuta umeshasimama mbele ya panel wapo Dr, Prf, unapresent vitu vyako
Sifa za kijinga,kwa hiyo umesoma undergraduate SUA na ARU?
 
Ukisema wahadhiri wengi wa SUA ni kina Shomire utakuwa unakosea maana SUA ni taasisi kubwa yenye vitivo na idara kadhaa. Nakushauri ukarejee kufanya tafiti zako ili ujue ni katika idara/vitivo gani ratio ya hao kina shomire ni kubwa au ndogo ukilinganisha na wengine. Hii ni kwasababu zipo baadhi ya idara huwezi mpata mhadhiri wa namna hiyo na hata kwenye senate hali yaweza kuwa hivyo hivyo. Ebu nikuulize, ulipofanya huo utafiti wako uligundua SUA ina wahadhiri wengi wa Mkoa gani? ACHA MASUALA YA KUJA KUONGELEA UKABILA KWENYE MAENEO KAMA HAYA, HATA KAMA HAO KINA SHOMIRE NI WENGI BASI NI PONGEZI KWAO NA WENGINE INABIDI TUJIFUNZE TOKA KWAO SIYO KULALAMIKA MARA UKABILA, UKANDA, UDINI. HII NI SAWA NA CHURA APIGAVYO KELELE KANDO KANDO YA DIMBWI LA MAJI UKIMSOGELEA ANANYAMAZA.

Mkuu watu wengine ni kuwapuuza tu namshangaa huyo mtoa post..Angesema shule ya pale si ya mchezo labda lakini ukabila ni muongo tu.Kakremu mambo eti Nshomire,uzushi mtu.
 
Wakuu salam zenu ningependa kujua chuo cha sua kipo katika geographia gani nikiwa na maana umbali kutoka mjini,mazingira ya chuo kwa ujumla..nk....karibuni mnisaidie kwa mnaokifaaham iki chuo.

Natanguliza Shukraan

Kama unareport Solomon basi ukifika msamvu panda daladala za mjini,then ukifika mjini panda daladala za mazimbu.Kama ni pikipiki ni 2000 mpaka 3000 iwe main campus au mazimbu
 
Back
Top Bottom