Ha ha ha...so SUA ni hatari wanatoa watu walioiva kikweli kweli kwenye fani zao... asanteni wakuu
Naombeni anaeijua bach of food science and technology anijuze kindani
Naombeni anaeijua bach of food science and technology anijuze kindani
SUA halisi ipo kandokando ya safu za milima ya uluguru eneo moja maarufu kwa jina la KIDIDIMO mjini Kasoro bahari kwa Waluguru huko Morogoro, ni KM 5 toka Msamvu stend ya Mabasi ya Mkoa. Usafiri kutoka Msamvu kwenda SUA direct ni TAX tu bei 5000/= pikipiki 3000/= au daladala 400/= mpaka mjini kati, ukishuka unaelekea soko kuu huko ndo parking ya gari za kwenda Sua zilipo ni Minibus nauli ni 500/= dakika 10 tu umeshafika SUA main campus huko barabara ni za lami tu, nchi iliyofunikwa na Kijani kibichi tu msimu wote, kila aina ya Mazao ipo huko, mfano ukienda Horticulture Unit huko utafikiri ndo Edeni ya Biblia, jinsi miti ya matunda ya kila aina ilivyozaa na maua mengi, mboga za majani za kila aina zipo huko.
First year, wanafikia Solomon Mahlangu Campus hii ipo Mazimbu, 7Km from Msamvu stendi. Huko ni kambi za kijeshi za Wapigania uhuru majemadari wa South Africa. Huko kuna umeme wa aina yake ambao hutaona nguzo hata moja kwenye hiyo Campus ila upo kila hostel kule zinaitwa Unit 1-6 na Freedom Square hapo ndo meeting place ya Mitihani kila jumapili, Maelezo haya ni kwa hisani ya matembezi ya 2007 hivyo kwa sasa kunaweeza kuwa na mabadiliko ya kigeografia zaidi maana binadamu ndiye anayeharibu miundombinu.
Wasomi wa SUA hawajatekwa na ulimwengu wa mitandao ya kijamii, wala shamrashamra za kuhudhuria matamasha ya miziki wkend, mkuu kule ni kitabu tu, ukifika utaipenda SUA, utasoma kwa raha na hofu ya kudisco itakuwa begani mwako kila uamkapo.
Irrigation and water resource engineer sio kozi bali ni mtu aliyesoma irrigation and water resources engineering, hiyo kozi utajifunza mengi kuanzia uchumi, biashara, maths na engineering in its details!!kwaiyo maisha yakule ni maisha mazuri sana kwa kijana wa sasa...especialy in this global world...nashukuru mungu kwan aya ndio maisha i dremt of....vip irrigation and water resources ingeneer...
SUA hakuna civil engineering as civil engineering bali kuna water resources kama branch ya civil...Hivi civil engineering ya hapo ikoje?
sio hilo tu mpaka ujenzi na ku design structures kama nyumba, madaraja, machines and the alike!!Civil Eng.. Sua haipo ila kuna Agricultural Engineering hii ni nzuri ila utakuta wanaume ndo wengi girls wanaweza kuwa 3 tu. Ni nzuri unajifunga kufunga jembe la trekta ukiwa farm, vitu kama hivo. Huko hesabu za kina Prof Sembuche, nyingi tu
Sua kuna digrii nyingi sana zipo za Nyuki, Mboga, Kupika, Kutandika vitanda, sayansi ya Lishe, na nyinezo sikuhizi nimeskia eti kuna Geomatics, teheee tehee chezea ulimwengu wa GIS Spatial Mapping duuu haya ni mambo ya UCLAS a.k.a ARU.
Ukisema wahadhiri wengi wa SUA ni kina Shomire utakuwa unakosea maana SUA ni taasisi kubwa yenye vitivo na idara kadhaa. Nakushauri ukarejee kufanya tafiti zako ili ujue ni katika idara/vitivo gani ratio ya hao kina shomire ni kubwa au ndogo ukilinganisha na wengine. Hii ni kwasababu zipo baadhi ya idara huwezi mpata mhadhiri wa namna hiyo na hata kwenye senate hali yaweza kuwa hivyo hivyo. Ebu nikuulize, ulipofanya huo utafiti wako uligundua SUA ina wahadhiri wengi wa Mkoa gani? ACHA MASUALA YA KUJA KUONGELEA UKABILA KWENYE MAENEO KAMA HAYA, HATA KAMA HAO KINA SHOMIRE NI WENGI BASI NI PONGEZI KWAO NA WENGINE INABIDI TUJIFUNZE TOKA KWAO SIYO KULALAMIKA MARA UKABILA, UKANDA, UDINI. HII NI SAWA NA CHURA APIGAVYO KELELE KANDO KANDO YA DIMBWI LA MAJI UKIMSOGELEA ANANYAMAZA.
Sifa za kijinga,kwa hiyo umesoma undergraduate SUA na ARU?Furaha iliyopo SUA ni kuwa unaweza anza fist yr mpaka unamaliza 3yrs hujabahatka kuongea na Dr, Prof, may be academic advisor wako, kwahyo unakuwa hujaiva vizuri, maana seminar presentation baadhi ya coz hakuna. Majembe ni vijsna wa ARU aiseee fisrt tu unajikuta umeshasimama mbele ya panel wapo Dr, Prf, unapresent vitu vyako
Ukisema wahadhiri wengi wa SUA ni kina Shomire utakuwa unakosea maana SUA ni taasisi kubwa yenye vitivo na idara kadhaa. Nakushauri ukarejee kufanya tafiti zako ili ujue ni katika idara/vitivo gani ratio ya hao kina shomire ni kubwa au ndogo ukilinganisha na wengine. Hii ni kwasababu zipo baadhi ya idara huwezi mpata mhadhiri wa namna hiyo na hata kwenye senate hali yaweza kuwa hivyo hivyo. Ebu nikuulize, ulipofanya huo utafiti wako uligundua SUA ina wahadhiri wengi wa Mkoa gani? ACHA MASUALA YA KUJA KUONGELEA UKABILA KWENYE MAENEO KAMA HAYA, HATA KAMA HAO KINA SHOMIRE NI WENGI BASI NI PONGEZI KWAO NA WENGINE INABIDI TUJIFUNZE TOKA KWAO SIYO KULALAMIKA MARA UKABILA, UKANDA, UDINI. HII NI SAWA NA CHURA APIGAVYO KELELE KANDO KANDO YA DIMBWI LA MAJI UKIMSOGELEA ANANYAMAZA.
Wakuu salam zenu ningependa kujua chuo cha sua kipo katika geographia gani nikiwa na maana umbali kutoka mjini,mazingira ya chuo kwa ujumla..nk....karibuni mnisaidie kwa mnaokifaaham iki chuo.
Natanguliza Shukraan