Geor Davie ni nani?

Acha kukuza maneno. Ninachojua jamaa alikuwa anampiga mke wake na alijaribu kumchoma moto. Watoto alikataa wasichukuliwe, mwanamke alifanya jitihada zote bila mafanikio. Hilo la kusema amekimbilia ndoa ya mtu mwingine unalijua wewe. Ninachojua huyo mwanamke hajaolewa tena.
 
Mlikuwa mnauliza ukweli. Nimewaambieni ukweli kuhusu mtu huyu. Roho zinawauma! Hakuna anayemwabudu mtu wala anayemtetea mtu wala GeorDavie hajitetei na wala hana muda huo. Sasa mpinga Kristo kati ya GeorDavie na wewe ni yupi?. Kinachokufanya upambane naye ni kwa vile amelibeba jina la Yesu Kristo. Wewe uliwahi kwenda kwenye hiyo huduma? uliona akiabudiwa? ulisikia akihuburi habari za shetani au za Yesu. Kama anatumia jina la Yesu Kristo na neno la Mungu kuharibu kazi za shetani kwanini kinakuuma kama haujavamiwa na roho ya mpinga Kristo; Neno la Mungu liko wazi haujui hata maandiko! Yesu alisema Ufalme mmoja ukijipinga wenyewe hauwezi kusimama. Shetani atampinga shetani mwenzake? Je Mungu atajipinga mwenyewe? Jichunguze sana ndugu isijekuwa umevamiwa na roho ya Mpinga Kristo na haujijui. Mwombe sana Mungu wako akuambie GeorDavie ni nani. Kwa akili yako unafikiri Nabii GeorDavie ana muda wa kujitetea! haujamjua bado. Mwombe Mungu akupe macho ya rohoni uweze kumtambua. Maake hata ukisoma niliyoandika hauwezi kuelewa kutokana na vifungo ulivyonavyo.Njoo kwa Yesu Ndugu iko furaha. Mpe maisha yako uweze kumwelewa vizuri uache kupambana na watu wake. Kisa neno mheshimiwa tu....umekwazika! lakini mafisadi wakiitwa waheshimiwa unasikia raha...mtumishi wa Mungu tukimwita mheshimiwa roho inalipuka....uko upande gani?! kama ungekuwa unampenda Mungu ungewainua watumishi wa Mungu na kuwasapoti wakafanya kazi ya Mungu vizuri! Mungu akatukuzwa nawe ukabarikiwa. Binafsi nimenawa mikono kama pilato! ukweli nimewaambia kazi kwenu...siku zote mafuta na maji lazima yajitenge. Mwenye macho na masikio autafute uso wa Mungu na amfanyie muumba wake Ibada ya kweli. Acheni kuangalia wanadamu mwangalieni Mungu atawavunulia yaliyofichika. Maisha haya tunapita ndugu! dunia hii ni safari! umejipanga vipi? Je Yesu akirudi leo utakuwa tayari....?
 
Kweli kuhusu nini. Huenda ikawa wewe ni mmojawapo wa wale wanaozusha Nabii GeorDavie amemchukua mke wa mtu. Kama Huyo bwana alikataa mke asichukue watoto huyo mama ajinyonge. Watoto wakiteseka huyo mume ndiye atakayedaiwa kwani yeye ndie aliyeivunja nyumba pia akaona haitoshi akamnyang'anya mama watoto wake kwa kudai yeye ndiye kidume. Huyu Nabii anaingiaje hapo au tatizo ni huyu mwanamama kuwa katika hiyo huduma.
 

wewe kweli mwanatumbi, hujui lolote.
 

Kwanza hueleweki, Jina lako la kike, lakini unaongea kibabe sana, nadhani wewe una pepo, Huyo mungu anayechukua wake za watu ni kabila gani? kutokana na jinsi ulivyojieleza, direct wewe ndo muhusika, unajaribu kufuta midomo kwa mikono baada ya kula unasahu kuwa harufu ipo. nani aliekwambia kuwa mwanamke ni almas? labda ungesema ana almas ungeeleweka.

Najua washirika wengi wa ngurumo hamjui maandiko kwakuwa huyo mshikaji wenu hana muda wa kuwafundisha, mnachojua ni pepo toka, bila kuwa na Neno, hata kama unaupako mpaka unapaa ni bure.

Viviane. kutoa pepo, na miujiza si kigezo cha utakatifu, linalotumika pale ni jina la Yesu, There is power in the name not in the person who use it, je hujasoma haya maandiko? (" Sio wote waniitao bwana bwana...............".) (Watesema, "tulitoa pepo kwa jina lako ..................")
 

Mungu wa Mbinguni hawezi kuacha jina lake lisipate utukufu......watalitumia na watatumika kama punda lakini kibano chao kinakuja.....huu uzinzi sio kwa huyu tuu...Mungu tusaidie ni heri usijue mambo ya hawa wanaojiita watumishi wa Mungu lakini matendo yao yanadhihirisha kuwa ni watumishi wa shetani 100%...Kwasababu kwa ushuuda wao sasa hawa watasababisha watu wengi wasiokoke...na sio huyu tuu...inasikitisha sana sana juu ya hawa ... Wazee...wengine wanawatisha waumini wao wanaojua habari zao kwamba kwa waumini kuongelea uzinzi wao watapata ukoma kama Miriam alivyopigwa na ukoma kwa kumsema Musa.....Mtumishi wa Mungu Kakobe Mungu azidi kumtumia na kumtia nguvu...mimi sio mumini wake lakini ni mtumishi ambaye amedhubutu kusema madhabahuni kama ikiwa kunamtu anafahamu kasha yake yoyote ya uzinzi asema au aandike!!!! Sasa twende pale kwenye ile Benki....Twende kule kwenye Makuti Kawe aibu tupu Mungu awarehemu watu hawa na unafiki wanaoufanya na kundi kubwa likiwa nyuma yao na kuwasikiliza .......bila kujua mambo yao machafu mnooooo..........mapaka mtu unakaa unajiuliza hivi kweli hawa ni watumishi wa Mungu......!!!!!????????
 
<br />
<br />
thanx mkuu,u really made my day...waambie ukweli hao wanaotetea ujinga.
 
Huyu ni msanii kama wasanii wengne.
 
Mnajichanganya tu, wala hakuna anayemwelewa GeorDavie.... Pamoja na kulitaka jina la YESU lipitayo majina yote. Bila kufanya agano na Yesu akakukabidhi mamlaka na kukupaka mafuta utataja Jina la YESU mpaka mapovu yatakutoka....na pepo litaendelea kukutolea macho. Kabla hamjasema kitu hakikisheni mna uhakika na mkisemacho.
 


Watu wanaenda na facts hapa ndiyo JF utaongea hadi mapovu yakutoke mdomoni kama huna facts hakuna wa kuamini huu utumbo.Wote waliomtuhumu wameweka facts wewe je? Unabaki wivu,sijui nini aren't you ashamed bro/sister? Pangua hoja za jamaa kwa hoja siyo kujaza pages tu.Halafu cheki hapa
Join Date : 2nd September 2011

Posts : 13
Rep Power : 0

Umetumwa siyo bure!!
 

Nyinyi watu hebu muogopeni Mungu kidogo yaani mnatetea hadi huyo "nabii " wenu kupora mke wa mtu?Hivi ukimfuata huyo "nabii" ndo hata kutumia akili yako kupambanua mambo huwezi? eti "kwa taarifa yake hakunyang'anywa na GeorDavie alinyang'anywa na Mungu.." Pum..vu!! Mungu anaweza kumpora mtu mke?Acheni unafiki njaa zitakufikisheni pabaya.Uliyeporwa mke Mungu atakulipa usijali
 

GeorDavie's hanger-on at work
 

Does this justify what your "nabii" has done?
 
Mtu yeyote ambaye ni "Mtumishi wa Mungu" kwa maana yake halisi hahitaji kulindwa na mabaunsa! Yesu ambaye ni Mungu kweli alipanda punda wala hakutafuta ufahari wowote. Sasa huyu mtu aitwaye georgedavie nakubaliana na wote waliosema ni "nabii wa uongo." Kipekee sina ushahidi juu ya mengine yaliyosemwa lakini kama ni kweli akatubu.
 
Mna maanisha nini kusema analindwa? Mimi naona hiyo ni style yake. Ni kama vile mtu anavyoamua kutembea kwake azungukwe na wazee au vijana au watoto. Kama angekuwa analindwa basi wale watu wange beba bunduki, bastola, mashoka, rungu, panga n.k. kwani ulinzi maana yake nini? mmesahau neno la Mungu linalosema Mungu asipoilinda nyumba wailindao wanakesha bure? Sijawahi kumwona mlinzi bila silaha! Mimi ninaona hiyo ni style yake na hanisumbui. Ni kama vile mtu kuamua kuvaa mayeno au bukta au kunyoa au kufuga nywele. Sielewi kwanini mambo kama hayo yanawaumiza vichwa na kumfuatilia jinsi hii. Hata Yesu mwenyewe alipenda kutembea na wale Mitume 12.Mnafikiri alikuwa anaogopa kutembea pekee yake? hakumwambia Petro arudishe upanga...vita vile sio vya nyama na damu? Ilibidi iwe vile ili maandiko yapate kutimia otherwise wasingeweza chochote? Kwa akili zenu GeorDavie alivyoshujaa anaweza kuogopa wanadamu atafute watu wa kumlinda? Sioni point hapo mpendwa!
 

Kuna upako ndani yako kweli mbona nashindwa kutofautisha majibu yako na ya wale wadada wa taarabu uswahilini, tofauti hapo ni kutaja jina la Mungu basi. Turudi Kwa Mchungaji wenu nabii mtakatifu mheshimiwa. mbona hafanani kabisa na mtume anaye muwakilisha yaani Yesu Kristo ambaye ni mwana wa Mungu lakini hakuhitaji kabisa makuu. wakati mchungaji wenu amejipachika majina ishirini yasiyo na maana. Bwana Yesu alikataa hata kuitwa mwalim, wakati mchungaji wenu anatembelea magari ya kifahali akiwa na walinzi akitandikiwa carpet ili apite, Biblia inatuambia tuwe na Kiasi hata kama unacho kingi lazima uwe na kiasi ili utofautiane na watu wa mataifa. Bwana Yesu alitembea kwa miguu kijiji hadi kijiji hakutumia hata punda achilia mbali farasi waliokuwa ndio usafiri bora kipindi chake. na kwa nini mtumishi wa Mungu awe na kasha kiasi hicho unafikili ni chuki za watu kweli. Mbona akina mwakasege wanaheshimika wakati wanatangaza injili hiyo hiyo. lazima kuna kitu juu ya huyu anayejiita nabii mtakatifu
 

Mh! Mbona sijawahi usikia huyo Nabii akijiita mtakatifu! Mimi jamani jinsi ninavyomjua Mungu! Hapa duniani nitarithi kila kitu, magari, majumba, furaha kila kitu na zaidi sana mbinguni. Mungu hajali ninaitwa nani! Kumbe niwe maskini wa kutupwa ndio mjue kwamba nina Mungu! Kwa taarifa yako Yesu hakuwa maskini, Vazi lake tu lenyewe liligombaniwa. Mwanapunda kipindi hicho ndio usafiri uliokuwajuu na wakuheshimika. Yesu alipoulizwa wewe ni mwana wa Mungu?? aliposema mimi ndiye lol! walipambana naye vikali sana.

Nabii GeorDavie anaelewa mamlaka aliyopewa na Yesu Kristo na ulimi wake umebeba nini. Naona muanze kupambana na mimi kwa maana,mimi ni mwana wa Mungu! Nina mamlaka aliyonipa Yesu Kristo! Yesu anaishi ndani yangu! Niko juu! Mimi ni tajiri! jamani, kumbe tukiri udhaifu?? Mimi ninakiri na kutamka ushindi na ndivyo nilivyo tena mimi ni mwana wa mfalme na shetani haniwezi akiniona anahaha! Ukikiri udhaifu ndivyo utakavyokuwa pia unavyojiona ndivyo utakavyokuwa pia ndivyo utakavyoishi. Tena nyie mnaofanya kazi ya Mungu kama hamuwezi kumwakilisha Mungu vilivyo kila siku mna shida na madhaifu mnamwaibisha Mungu! Ulimi unaumba jamani.

Mungu alitamka tu vitu vyote vikatokea. Soma basi hata bible jamani, uombe pia Mungu akufunulie ili uweze kuelewa. Uache kubambana na GeorDavie.
Kila mtumishi ameitwa kivyake, na amepewa karama tofauti.Mwakasege ni mwalimu na GeorDavie ni Nabii kuna tofauti! Hauwezi kumlinganisha mwinjilist na Mwalimu au Nabii! Japo wote wako katika serikali moja. Binafsi mimi ninamfagilia GeorDavie! Tena asingepigwa vita ningeshangaa sana....Katika maandiko ni mtumishi gani hakuwa na vita. Ukilitaja jina la Yesu unatangaza vita na shetani...unategemea nini??

Nabii GeorDavie kuna mahali umegusa....mpige shetani kisawasawa usirudi nyuma, jipe moyo mkuu! usijali maneno.Zidi kumwinua Yesu Baba majina yote mazuri ni ya kwako. Ninachojua Mungu/Yesu ana majina mengi na mazuri...Yesu! na alikuwa akipenda kuongozana na watu pia.
 
Mimi ni Muislamu,
Mwanzoni mwa mwaka 2008 nikiwa Arusha nilipata kusikia sana juu ya huyu mtu,
Popote nlipopita ilikua ikiongelewa masuala ya Upako wa huyu mtu tu.
One day nikiwa mpweke tu hotelini nilikofikia nikaona wacha nimchunguze huyu jamaa anaetajwa tajwa kila mahali, hivyo nikafunga safari mpaka Kisongo lilipo kanisa lake,
Ukweli lilijaa sana na hata barabarani gari nyingi zilibadili route kuelekea huko.
kwakua nilikua kwenye ka-research kangu simple tu ka kupitishia wikiend nikaamua niingie kanisani kabisa (uwanja wenye viti vya plastic kama alfu 10 hivi na turubai juu).
Nlichotaka kuthibitisha ni madai ya watu kua jamaa ana uwezo wa kumsoma mtu mawazo (ramli!!??), pia kama hujampokea Kristo unaangushwa na mapepo, Hivyo nikasubiri mpaka ile session yake ya kuzunguka mstari mpaka mstari huku nikimsema kimoyomoyo nione kama atasikia, au kustukia kwamba mimi ni Muislamu nipo kiuchunguzi zaidi.
But hakunijua na wala sikuanguka,
Ndipo nilipo-confirm kua watu wa Arusha wameingizwa mkenge na huyu jamaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…