Huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale ni mwenyeji wa Singida mi nlianza kumfahamu miaka ya tisini alikuwa tarishi pale world vision, Arusha alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la Siloam Gospel Assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi Uhuru Arusha.
Kwa kipindi hicho mi nlikuwa mwanafunzi wa primary tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'' ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana ka kuvaa mabagi na kunyoa pushback kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha.
Si kumsikia tena hadi miaka ya kuanzia tisini na sita hivi alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao ka watano hivi wa kuzugia.
Kituo hichi kilikuwa majengo karibia na Sacon Opposite na kanisa la KKKT Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha, aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko kisongo mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu ka ''mji wa Daudi'' kwa kweli huduma yake imejaa contrervasial saana maisha yake pia yana utata.
Means jinsi anavyiobehave pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh.
Simkubali na hii ni kutokana na matunda yake yaani tabia huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design ka yake ila sijui? Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu.