George Ambangile VS Ali kamwe ni nani mchambuzi bora wa mpira wa miguu nchini Tanzania?

Wakuu habari,

Ni mchambuzi yupi mahiri katika uga wa mchezoo wa mpira wa miguu hii battle inamuhusisha George Ambangile kutoka Wasafi FM na Ali kamwe kutoka Azam Média
Kama ni Kuchambua huku akichomekea na maneno ya Kiingereza Kimakosa ( akichapia ) ambayo mara nyingi huwa namsikia basi George Ambangile anaweza Kuongoza.

Ila ukitaka kupata Uchambuzi wa Kiufundi kabisa wa Mpira unaoambatana na Sauti yenye Mvuto Kuisikiliza na akikupa Uhalisia mzima wa Mchezo ( Soka ) basi Ally Kamwe yupo vizuri sana.

Kwangu Mimi kwa hawa Wawili Ally Kamwe ni mzuri kuliko George Ambangile na kinachomwangusha zaidi Ambangile ni Unafiki na kutojificha Unazi wake kwa Yanga SC tofauti na Ally Kamwe ambaye huwezi jua yuko wapi Kiunazi ( japo Mimi namjua anaishabikia Timu gani ) hapa Tanzania kati ya hawa Giants Wawili wa Kariakoo.
 
George ni beast
Kama Kiingereza ni tatizo Kwako kuna haja gani ya Kukilazimisha hivi na Kukikosea?

Kwani ungesema tu kwa Kiswahili kuwa George Ambangile ni Bora ( Mzuri ) usingeeleweka au hata kuonekana nawe Umesoma?

Hiki Kiingereza chako cha George is beast ( badala ya George is the best ) umekitoa wapi? Ndiyo nyie mnatufanya 24/7 tunachekwa na Wakenya na Waganda ( mpaka hata na Wanyarwanda ) kuwa hatujui Kiingereza achilia mbali wale Wenyewe wenye Lugha yao Waingereza.
 
Kuanzia leo nampa jina jipya AMBA THE GREAT
huyu jamaa ana ka ujinias flani hv kusema kweli. Manake mnaweza kukaa wote mnacheki soka ww ukiona labda mapungufu mawili kwenye timu yy anaona mapungufu nane. He is a complete package.
 
Nakumbuka kuna siku huko twitter aliomba aulizwe swali lolote na atalijibu, kuhusu timu aishabikiayo tz alisema ni simba ingawa huwa haumii sana ikifungwa tofauti na anavyo umia inapofungwa Man united anayoishabikia kwenye EPL.
 
George ni beast iyo best umesema ww mkuu
 
Geoph Lea, huyu ni full packages...takataka zote za sports zipo kichwan mwake, Basketball, football, tenesi, golf twende! Udhaifu wa Ambangile yupo deep kwenye football tu na football yenyewe current na siyo historical, ukimuuliza swali la miaka 10 au 15 iliyopita sidhan kama atakuwa na idea nalo, ila Geoph yupo full nondo kuanzia miaka hiyo ya mababu yeye anatiririka tu ma info yan!
 
Sema toka bimkubwa wake kafariki hayuko poa
 
Umeanza kumfuatilia akiwa redio ipi??

Kama mpaka leo angekuwepo pale magic wengi tungemuona wa kawaida tu
 
Umeanza kumfuatilia akiwa redio ipi??

Kama mpaka leo angekuwepo pale magic wengi tungemuona wa kawaida tu
Me nimeanza kumfuatilia akiwa magic fm. Ni kweli jina lake limekuwa kubwa kutokana na media anayofanyia kazi now
 
Namfahamu huyu George tangu yuko Magic, niliona hana mpinzani ila Redio yake ndiyo ilikuwa si maarufu......anafanya utafiti, hana ushabiki, anaongea kwa mifano.....anafanya kazi nzuri
 
Wakuu habari,

Ni mchambuzi yupi mahiri katika uga wa mchezoo wa mpira wa miguu hii battle inamuhusisha George Ambangile kutoka Wasafi FM na Ali kamwe kutoka Azam Média
Ndio huyu aliyepewa pira na domondi?
 
Anaweza kuwa yupo sahihi kwa alichotaka kukisema..

Beast ni kitu noma.
 
Mpira wa bongo Amri kiemba&mayai,historia ya michezo yote Jeff Lea ,ufundi Ambangile,jicho la tatu (beyond the scene kwenye football) Ally Kamwe,vichekesho kwenye footbal Eddo,mkosoaji kwenye michezo Shaffih,mwandishi bora wa makala za michezo farhan,hakuna mchambuzi anayeweza kukupatia yote haya
 
Kwa mtu anayependa michezo na kuifuatilia, hawez kuacha kumfuatilia mchambuz bora kabisa kama Geoph Lea! Jamaa anachambua with facts!

Kwangu huyu ndiyo mchambuz bora na mwenye kipaji kikubwa sana cha uchambuz Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…