kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Simba na Al Ahly zimetolewa kwenye mashindano ya African Football League (AFL) bila kushinda mechi hata moja. Baada ya Simba kushindwa kuifunga Al Ahly hata baada ya kutangulia kuifunga, mchambuzi wa michezo, Bw. George Job alisema Al Ahly imeshuka kiwango (unga) ndio maana alishindwa kuifunga Simba mbovu pia. Alisema kama simba ingekuwa nzuri ingeitoa Al Ahly (mbovu msimu huu) kwenye mashindano.
Baada ya kusema hivyo, wachambuzi wenzake walimjia juu na kusema anaikosea heshima Simba, wakimaanisha kuwa Simba bora imetoka sare Al Ahly bora. Lakini Al Ahly kutupwa nje ya mashindano ya AFL pia kunasadifu uchambuzi wa Mr. Job kuwa Al Ahly msimu huu imeshuka kiwango, imeshindwa kupata matokeo hata kwenye uwanja wake wa nyumbani tofauti na zamani.
Tumpe Job maua yake kwenye football, Simba msimu huu haina timu ya kushindana kimataifa.