George Mpole Anaongoza Kwa Ufungaji Lakini si Tishio!

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Mpira umekua na vituko vya ajabu sana hususani hapa kwetu Tanzania,eti baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu mchezaji Fiston Mayele limetokea kundi kubwa sana la watu waliotokea kumchukia na kuomba kila dua kwa mungu Mayele asifunge magoli!.

Hii imepelekea hadi sasa kila timu ikiingia kucheza na Yanga safu ya ulinzi wote wanaagizwa kuwa macho na huyu mchezaji mmoja na kupewa special attention ati asifurukute.

Imekua kawaida sasa Mayele kukabwa na beki wawili,hadi watatu kila ashikapo mpira!..but the guy is so talented kwani ameshalijua hilo nae hucheza kwa juhudi kubwa ktk mazingira haya magumu kwa kuwapenyezea wenzake mipira washinde mabao na tumeona inaleta matokeo..

Wengine wamefikia mbali hata kufikia kutumia nguvu za giza yaani majini yamdhibiti huyu Mayele asifanikiwe kufunga!..unajiuliza hivi mpira umekua ni vita? Michezo ni furaha...michezo ni burudani..michezo ni amani..
Najiuliza Messi,Ronaldo au Lewandonsky wangekua wanacheza ligi yetu hii na ulimbukeni huu na roho mbaya hizi, si wangekua tayari hata tumeshazika miaka mingi?hivi kuna tatizo gani mchezaji akifanya vizuri?wengine wanaumizwa na nini?tutafika wapi ki soka kama nchi?

Mwisho nimpe hongera George Mpole kwa leo kuongoza ktk ufungaji ligi ya Nbc lakini nina imani hata na yeye anajijua kuwa si tishio kwa mabeki.na ndio maana hakuna mabeki wanayehangaika nae kitu kinachompa speed ya kukimbizana na Fiston..tofauti na ilivyo kwa Fiston ambaye hata baada ya mechi ya mwisho Ya Yanga kumalizika akihojiwa aliweka bayana wakati mgumu a aoupitia kwa kukamiwa

Mayele kwa kipindi kifupi ame trend Tanzania,afrika na hata baadhi ya nchi nyingine za asia na europe kwa ushahidi wa video kuliko mchezaji yeyote wa kigeni aliyewahi kucheza katika historia ya nchi hii

Hongera kwake Fiston na atabaki kuwa mshambuliaji tishio nchini kwa sasa hata kama itatokea azidiwe magoli 4.
 
Ni upopoma wa kiwango cha juu kusema timu flani au mchezaji anakamiwa ,kazi ya mabeki ni kuonyesha uwezo wao kukaba wafungaji,haijalishi anakabwa na mmoja au zaidi,kila timu inaingia uwanjani kutafuta ushindi sasa unataka wawe wanaachia Mayele afunge ?

Ni ujinga uliopitiliza mchezaji wenu akishindwa kufunga mnalia lia , kama Mayele ni striker mzuri ndo mda kuonyesha kwamba atachukua kiatu mbele ya Mpole ,na asipoangalia atakutwa pia na yule mwenye magoli 10
 
Hakuna anaye muombea asifunge, na hata ikitokea watu wanaombea hivyo basi maombi yao hayana mchango wowote wa kubadilisha ukweli

Watu wanafunga magoli kwasababu ya uwezo, watu hawafungi magoli kwasababu ya maombi ya watu nje ya uwanja.

Unaamini ile penati aliyokosa ilichangiwa na maombi ya watu au ni pressure ya mchezaji na maswala yake binafsi?

Jibu ni kwamba huyu mchezaji wenu anapigiwa promo sana, wanaompigia promo wanampigia promo kwa kuwashusha wachezaji wengine wanaocheza nafasi kama zake

Kwa kukipigiwa promo huko lazima watu watakuwa wanamuangalia yeye na kama hajafanya kile ambacho mmekuwa mkipigia promo basi lazima hili kundi ambalo lilikuwa likinyanyasika kwa kelele zenu lianze kuwachana ukweli.

Mfano mzuri George mpole kafunga magoli mengi lakini kwanini haiwi habari kubwa?

Ni kwasababu hakuna mpambe ambaye anaweza kumpigia promo ya kufikia hatua ya kuwa habari kubwa kwenye media zote hadi mitandaoni.

George mpole ni husler ambaye magoli yake naweza sema 100% yote ni juhudi zake hakuna goli lililopatikana kwa mbeleko kama ambavyo wachezaji wa timu hizi mbili wanavyobebwa.

Mi naamini kabisa huyu Mayele angekuwa Geita Gold akacheza nafasi ile ile ya George Mpole kwa aina ile ya kikosi na aina ile ya uviziaji sidhani kama angefikisha goli 2.


Nazo hizo 2 labda za penati japo napo kwenye penati ni tatizo ila strugling kwa mwana ni zero sana huo ni ukweli
 

Mayele Hamna mshambuliaji pale , ni mchezaji local sana mchezaji wa hapa hapa. Akisimama na beki wanaotumia akili na uzoefu kidogo tu anauza sura. Hana chochote cha ziada alichokionesha so far
 
Nenda kalime tumbaku mpira hujui
 
Utumbo mtupu bila points.
 
Kwa hiyo unataka Mayele asikabwe?
Waache mabeki wafanye kazi yao, kazi yao ni kutoruhusu mshambuliaji afunge.

Nakufananisha na Mwamnyeto, kwenye mipita yote ya kona Bakari huwa anamlinda Mayele asikabwe, ni ujinga wa kiwango cha juu.

Acha watu wacheze mpira kama uwezo anao basi atafunga.
 
Kwan mtz mwenzio akichukua kiatu kinakuuma nn ?mayele anakamiwaaa bali uwezo wake ndio upo alipo now
Hainiumi kinachokera ni jinsi hii tabia mchezaji anayefunga sana hapa nchini kuchukiwa...na ushahidi wa roho mbaya unauona hata humu kwenye wachangiaji..cjui shida iko wapi...

Tazama leo Prience Dube yuko wapi mtu alikua mtupiaji mzuri tu...ndiyo kisa nasema Messi asingeweza cheza hapa kutokana na roho mbaya za watu
 
Mayele Hamna mshambuliaji pale , ni mchezaji local sana mchezaji wa hapa hapa. Akisimama na beki wanaotumia akili na uzoefu kidogo tu anauza sura. Hana chochote cha ziada alichokionesha so far

Mtoa mada anaona Mayele anakamiwa sana tena kwa makusudi ili asifunge, anasahau kazi ya mabeki ndio hiyo ya kuzuia kufungwa nadhani mahaba yake kwa Mayele na mafanikio ya Mpole yanamtatiza.
njaakalihatari Championship CHAMASON-MORISON-SAKHOSON Ghazwat Its Pancho JAYJAY
 
Mimi ni shabiki wa Yanga, lakini nafurahi kuona mchezaji mzawa anapambana na kuongoza kwenye list ya wafungaji bora.

Frank Lampard aliwahi kumnyima Didier Drogba penati, akaipiga yeye ili Drogba asimzidi magoli Wayne Rooney. Japo mpango wake haukufanikiwa (Drogba lilitupia goli bila hiyo penati), wenye akili tuliona nguvu ya utaifa na uzalendo hata kwenye mpira.

Kusema George Mpole sio tishio ni uongo, angekua sio tishio asingeongoza kwa idadi ya magoli. Kuona kijana ambae sidhani kama hata mshahara wake unafika laki tisa kwa mwezi akipambana na washambuliaji wa kigeni wenye mishahara minono, ni jambo la kupongeza!

Namkubali sana Mayele, ila tuache takwimu ziongee, na takwimu zinasema George Mpole ndio anaeongoza!
 
Tengua kauli yako,mchezaji anayefunga sana kwa sasa ni Mpole .
 
We unaleta uzalendo...Messi ameweza kuiteka Spain japo yeye ni mu argentina..this is football tuache siasa jamani...haya mambo ya uzawa ukabila nyerere alishakataza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…