Mimi ni shabiki wa Yanga, lakini nafurahi kuona mchezaji mzawa anapambana na kuongoza kwenye list ya wafungaji bora.
Frank Lampard aliwahi kumnyima Didier Drogba penati, akaipiga yeye ili Drogba asimzidi magoli Wayne Rooney. Japo mpango wake haukufanikiwa (Drogba lilitupia goli bila hiyo penati), wenye akili tuliona nguvu ya utaifa na uzalendo hata kwenye mpira.
Kusema George Mpole sio tishio ni uongo, angekua sio tishio asingeongoza kwa idadi ya magoli. Kuona kijana ambae sidhani kama hata mshahara wake unafika laki tisa kwa mwezi akipambana na washambuliaji wa kigeni wenye mishahara minono, ni jambo la kupongeza!
Namkubali sana Mayele, ila tuache takwimu ziongee, na takwimu zinasema George Mpole ndio anaeongoza!