kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mwanangu George Mpole hongera sana kwa kuonyesha juhudi uwanjani katikati ya ligi iliyojaa wageni wengi, juhudi zako zinatamanisha wapenda soka wote duniani. Lakini lakini lakini bado unahitaji kuonekana tena tena kwa wadau wa mpira ukirudia kukifanya hiki ulichokifanya kwenye msimu huu ili kuwaaminisha wadau kuwa hivyo ndivyo ulivyo na sio mambo ya chance (bahati). Yaani watu wenye hela zao wananunua kipaji, juhudi, maarifa na nidhamu ndani na nje ya kiwanja. Na ili kuthibitisha kuwa unavyo hivyo vitu 4 kuna vitu wanaviangalia, kwa kimombo wanaviita precision, validity na specificity, KIFUPI wanaangalia consistence kwenye kufunga katika mazingira tofautitofauti ya mechi, aina ya wachezaji kwenye mechi, hali ya hewa, ukiwa na furaha, ukiwa na huzuni, nk. Hivyo lazima ubaki kwenye timu ambayo itakufanya ucheze mechi nyingi sana ili wadau wapate wasaa wa kutosha wa kukuangalia tena na tena na tena. Sehemu hiyo sio Simba na Yanga, lahsha.
Simba na Yanga ni timu ambazo hazina uvumilivu hata kidogo, zinataka matokeo leoleo. Ni timu ambazo zinasajili wachezaji wengi kutoka ligi nyinge kwa lengo la kupata matokeo viwanjani leoleo, hivyo kama utacheza mechi 3 mfululizo bila kufunga bao hawatakuvumila, utakaa benchi na kupisha wachezaji wenye majina yao na wanaolipwa pesa nyingi sana. Hivyo utarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kumbuka mle msemo maarufu wa makocha usemao "The wining team never change" kikosi kinachoshida uwanjani hakibadilishwi, hawataki kujaribu kumpunzisha mchezaji mwenye uhakika wa kufunga eti kwasababu ya kukupatia wewe uzoefu.
Kama malengo yako ni kupata hela kuliko unazopewa Geita Gold basi nenda Yanga na Simba, lakini kama malengo yako ni kupata hela nyingi zaidi kuliko utakazopewa na Yanga na Simba basi endelea kubaki Geita au kwenye timu nyingine ya kati angalau kwa msimu mwingine mmoja wa kucheza kikamilifu.
Tumia makosa ya wengine (Ayee, Yusufu Mhilu, Ali Yusufu, Waziri Juma, Adam Adam, Salamba, Raphael, Nkane, Ambundo, Ngushi, Ndemla.....) ambao walitoka kwao wakiwa heros na kuishia kuwa zeros walipofika Simba na Yanga.