GE2025 Georges Busungu (ADA TADEA): Nikiwa Rais kila mfungwa atapata posho ya kila mwezi

GE2025 Georges Busungu (ADA TADEA): Nikiwa Rais kila mfungwa atapata posho ya kila mwezi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mgombea urais kupitia Chama cha Ada Tadea, Georges Busungu amesema endapo atachaguliwa kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 29, 2025, serikali yake itahakikisha magereza yote nchini yanaboreshwa na kila mfungwa anapata stadi za maisha pamoja na posho ya kila mwezi.

Busungu amesema posho hiyo itatunzwa katika utaratibu maalumu na mfungwa atakapomaliza kifungo chake, atakabidhiwa fedha hizo kama kianzio akitoka gerezani lengo ni kutaka kumuepusha asirudie makosa yaliyomsababisha kufungwa.

Akizungumza janaJumatatu katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika eneo la Fantom, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, mgombea huyo amesema mpango huo unalenga kupunguza uhalifu wa kujirudia, hasa kwa wafungwa waliokuwa wanatoka magerezani bila kuwa na mtaji au ujuzi wa kujitegemea.

“Serikali yangu itahakikisha magereza yote nchini yanaboreshwa, kila mfungwa atafundishwa stadi za maisha, na kila mwezi atalipwa posho itakayohifadhiwa rasmi. Atakapotoka gerezani, atakabidhiwa fedha zake kama kianzio cha kuanzisha biashara au shughuli halali za kipato. Hatuwezi kuruhusu mtu arudi kuiba kwa sababu hana namna ya kuishi,” amesema Busungu.

Chanzo: Mwananchi
 
Ana akili kuliko Tundu Lissu na John Heche combined 😀
 
Back
Top Bottom