Georgia kama Ukraine, Raia wachachamaa wakiandamana kushinikiza kujiunga na umoja wa ulaya(EU) haraka

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huko Georgia kwa wiki moja sasa raia wanaandamana na kupambana na polisi baada ya chama tawala kusitisha kwa muda mpango wa nchi yao kujiunga na umoja wa Ulaya(EU). Kura mbalimbali za maoni za Georgia zimekuwa zikionyesha 80% ya raia wa Georgia wanataka kujiunga na umoja wa Ulaya na kuwa wanachama kamili lakini chama tawala ambacho ni pro-Russia kinachotuhumiwa kuiba uchaguzi mkuu uliokiweka madarakani kilisitisha ghafla mchakato wa muda mrefu wa kikatiba ambao ulikuwa umekusudiwa kuipeleka Georgia katika umoja wa Ulaya.

Rais wa Georgia ambaye ni Pro-west lakini mwenye nguvu kidogo za kikatiba wanatifuana vikali na waziri mkuu asiye pro-EU/west mwenye mamlaka makubwa ya kikatiba. Dmitry Medvedev mropokaji wa mara kwa mara toka serikali ya Russia ameionya Georgia kwamba inaelekea njia ya Ukraine. Tayari Russia kupitia waasi inaowafadhili wanakilia majimbo mawili makubwa ya Georgia kwa muda sasa.
 
Ukraine wanajutia kwa kua na msimamo wa kujiunga na EU na Nato, wengi wana mkosoa Zere kwa kutoona mbali, Russia hawezi Kubali kitu kama hicho na US inajua hilo Hook or crook Russia hawezi kukaribisha Nato mlangoni mwake. ...........kura za maoni 80% hamtaki zere tena wala hawataki kujounga na Nato tena
 
Russia ina bahati mbaya sana kila watu wakiungana nao anaonekana Russia kafanya hujuma ila akipingana na Russia anaonekana kachagua demoghasia westerners hawajawa tayari kuanguka ila ndio hakuna namna tuu
 
Huko Georgia kwa wiki moja sasa raia wanaandamana na kupambana na polisi baada ya chama tawala kusitisha kwa muda mpango wa nchi yao kujiunga na umoja wa Ulaya(EU). Kura mbalimbali za maoni za Georgia zimekuwa zikionyesha 80% ya raia wa Georgia wanataka kujiunga na umoja wa Ulaya na kuwa wanachama kamili lakini chama tawala ambacho ni pro-Russia kinachotuhumiwa kuiba uchaguzi mkuu uliokiweka madarakani kilisitisha ghafla mchakato wa muda mrefu wa kikatiba ambao ulikuwa umekusudiwa kuipeleka Georgia katika umoja wa Ulaya.

Rais wa Georgia ambaye ni Pro-west lakini mwenye nguvu kidogo za kikatiba wanatifuana vikali na waziri mkuu asiye pro-EU/west mwenye mamlaka makubwa ya kikatiba. Dmitry Medvedev mropokaji wa mara kwa mara toka serikali ya Russia ameionya Georgia kwamba inaelekea njia ya Ukraine. Tayari Russia kupitia waasi inaowafadhili wanakilia majimbo mawili makubwa ya Georgia kwa muda sasa.
Wanataka kujiweka mbali na shetani Putin.
 
Ukraine wanajutia kwa kua na msimamo wa kujiunga na EU na Nato, wengi wana mkosoa Zere kwa kutoona mbali, Russia hawezi Kubali kitu kama hicho na US inajua hilo Hook or crook Russia hawezi kukaribisha Nato mlangoni mwake. ...........kura za maoni 80% hamtaki zere tena wala hawataki kujounga na Nato tena
Ukraine gani anayejutia? Kujuta ajute Russia halafu majuto mumsingizie Ukraine?
 
Russia ajute kwa kitu gani.Anayeumia mara zote ni yule ambaye vita vinapiganwa kwake...Hiyo miundombinu inayolipuliwa kila siku Ukraine huoni, watu wanaokufa huonj, ardhi inavyopotea huoni, Kunyanganywa Crimea kibabe huoni..Luhanski imeisha, Donbass inasakwa..huoni au unataka kujuta mpaka mtu aandike barua??
 
Ukikuta maandishibna sauti za Russia kujuta huwa unaruka eti?
Wapi Ukraine ameandika barua kuwa wanajuta?
 
Ukraine wanajutia kwa kua na msimamo wa kujiunga na EU na Nato, wengi wana mkosoa Zere kwa kutoona mbali, Russia hawezi Kubali kitu kama hicho na US inajua hilo Hook or crook Russia hawezi kukaribisha Nato mlangoni mwake. ...........kura za maoni 80% hamtaki zere tena wala hawataki kujounga na Nato tena
Georgia ni majirani wa Ukraine na Urusi kuliko wewe. Georgia raia wameamua watajiunga na EU, ushauri wako hauna matumizi kwao. Mikwara yako wameipuuza muda tu kina Medvedev wanaitoa mara nyingi.
 
Naona hao wanalilia Oreshnik.

1733223311749.png
 
Ukraine gani anayejutia? Kujuta ajute Russia halafu majuto mumsingizie Ukraine?
Tatizo lako wewe unabisha bila hoja au ushahidi unaushabiki kama ule wa Yanga na Simba wa hisia sio facts,

Ukraine inajutia kwasbb imeingia hasara kubwa kuliko faida itakao pata kutoka EU au Nato,
1. Imepoteza 20% ya aridhi yake kuenda Russia
2. Imeingia katika debt trap ya miaka haiwezi kulipa huo mkopo wakuendeshe vita bila kupoteza uhuru wake kwa EU na US
3. Viwanda via Ukuraini muhimu kama via nishati vimeharibiwa.
4. Kllimo cha ngano akipo tena kina kua controlled na Russia.
5. Nguvu kazi na jeshi lake liko exhausted
6 US, EU na Nato baada yakjmuhidi kujiunga na EU na Nato wameshindwa kutoa ratiba yake ya kujiunga manaake wamemsaliti
7. Raia ya Ukrain 60% ni wakombizi nje ya nchi yao hamna production manaake tena

Kwaufupi Ukraine imeingia hasara kubwa ambao ni irreversible wanajutia kuaminishwa na US na EU wakati US inahitaji Sanaa Russia kwa usalama wake na biashara kuliko Ukraine.
 
Russia ni sawa na ccm, wenye akili kamwehawawezi kumuunga mkono Russia kama ilivyo kwa CCM, mtu wz akili timamu hawezi kuwaunga mkono maccm
 
Georgia ni majirani wa Ukraine na Urusi kuliko wewe. Georgia raia wameamua watajiunga na EU, ushauri wako hauna matumizi kwao. Mikwara yako wameipuuza muda tu kina Medvedev wanaitoa mara nyingi.
Iyo nch aitolewi kwa kuandamana mamruki wawe tayali kufa kama kile kipindi wwnyewe wakanyooka kwani awa ndio wakwanza kuleta aya mambo wenzao walinyooshwa iyo miji ilipigwa wenyewe wakaomba pooo akuna NATO wala nyeto aliingilia kwasasa kuna majinga wanataka kuwaponza wenzao. Serikali sio wajinga wanajua kile walikutana nacho. Akuna Demokrasia ni uzushi tu. Na dawa ipo waendelea kulilia wembe.
 
Tatizo lako wewe unabisha bila hoja au ushahidi unaushabiki kama ule wa Yanga na Simba wa hisia sio facts,
Ushahidi na facts gani amazo wewe unazitaka? Facts ni mpaka zikufurahishe wewe? Haya twende kwenye hizo zako unaziita facts kwa akili zako za kitoto
Ukraine inajutia kwasbb imeingia hasara kubwa kuliko faida itakao pata kutoka EU au Nato,
1. Imepoteza 20% ya aridhi yake kuenda Russia
Hiyo 20% unayosema Ukraine ameipoteza na kupata hasara, kwa taarifa yako aliyepata hasara zaidi ni Russia. Kabla Russia hajaingia kule mazima alikuwa tayari ameweka waasi akiwasaidia silaha na mafunzoili wajitegnge. Ukraine alivoamua kujiunga EU Russia akaamua kutoka mafichoni na kuingia front kupambana na alipeleka silaha nyingi na kubwa na vikosi vya askari vilivyofyekwa na silaha kuharibiwa. Kwa akili zako wewe unadhani mgogoro kwnye hilo eneo ulianza February , 2022..
2. Imeingia katika debt trap ya miaka haiwezi kulipa huo mkopo wakuendeshe vita bila kupoteza uhuru wake kwa EU na US
Acha kujidanganya, Ukraine hakopi ili kupigana vita, kinachofanyika anasaidiwa na sababu ya msaada huo ni kwamba Ukraine kumzuia Russia ina faida kwao
3. Viwanda via Ukuraini muhimu kama via nishati vimeharibiwa.
angeweza kuwa na hivyo vowanda lakini akakosa soko. Kingine hiyo ndiyo maana ya vita. Kwamba unatwambia siku Kagame au Kenya akiamua kupora ardhi ya Tanzania aangaliwe tu sabsbu anaweza akashambulia viwanda na kuviharibu? Hzi akili zinatokana na makapi ya vitu gani?
4. Kllimo cha ngano akipo tena kina kua controlled na Russia.

Kwa hiyo ulitaka pwatulie nchi yao ichukuliwe kisa wasije kushindwa kulima ngano?
5. Nguvu kazi na jeshi lake liko exhausted
kwa akili zako unadhani Russia ndiye yupo imara? Unajifanya ulikuwa umelala pale vikosi vyake vilipopukutishwa hadi akaamua kutumia mercenary wa Wgner? Alipoona Wagner inamzidi umaarufu akai dissolve na kurudisha vikosi vyake ambavyo vikachapwa tena mpaka akaenda North Korea kuomba msaada wa wanajeshi? Hayo unajifanya hauyaoni?
6 US, EU na Nato baada yakjmuhidi kujiunga na EU na Nato wameshindwa kutoa ratiba yake ya kujiunga manaake wamemsaliti.
Hizo ni hisia zako kuna utaratibu wa jinsi ya kujiunga NATO. Ukraine tayari ipo vitani, ikiingia NATO italindwa vipi? Mpango wa kuchelewesha umelenga kuhakikisha kwanza Ukraine inakomboa maeneo yake ikiwemo Crimea, kinyume cha hapo mkataba huo hautakuwa na maana kwa Ukraine na watakosa nguvu ya kisheria kuilinda kwenye maeneo yanayokaliwa na Russia. Hili nalo linakupa shida kulielewa?
7. Raia ya Ukrain 60% ni wakombizi nje ya nchi yao hamna production manaake tena.
Yes raia ni lazima waondoke, serikali yao pia iliwahimiza kuondoka na wakaziomba nchi za Ulaya, Marekani na Canada ziwapokee na kuwatunzia wananchi wao hadi hapo watakapomaliza vita. Huko walipoenda kuna Programs kpwa ajili ya wakimbizi kutoka Ukraine, maana yake vita ikiisha Ukraine itapiga hatua sana sababu hao 60% tena siyo 60% ni 75% wapo nje ya Ikraine wanaendelea kupatiwa program za kuiendeleza Ukraine baada ya vita. Mtafute britanicca atakuelezea vizuri zaidi kuhusu hili. Siyo sawa na nyie ambapo wakimbizi wenu huishia kuishi kama machokoraa
Kwaufupi Ukraine imeingia hasara kubwa ambao ni irreversible wanajutia kuaminishwa na US na EU wakati US inahitaji Sanaa Russia kwa usalama wake na biashara kuliko Ukraine.
Sababu hutaki kusikia hasara kuhusu Russia, ila kwa taarifa yako Putin ameshatamka kwamba hii vita ni bora iishe tu.
 
Ukraine wanajutia kwa kua na msimamo wa kujiunga na EU na Nato, wengi wana mkosoa Zere kwa kutoona mbali, Russia hawezi Kubali kitu kama hicho na US inajua hilo Hook or crook Russia hawezi kukaribisha Nato mlangoni mwake. ...........kura za maoni 80% hamtaki zere tena wala hawataki kujounga na Nato tena
Hii ni taarifa kutoka masjid ubwabwa. Hivi kweli kuna nchi inaweza kukataa kujiunga na jumuiya ya ulaya hata Tanzania leo wangeambiwa wajiunge na jumuiya hiyo wangeenda mbio na hata Russia tu anaimezea mate vibaya lakini basi tu hana sifa za kuweza kuruhusiwa kujiunga.

Kuna kipindi kwenye miaka ya themanini Morocco baada ya kujiondoa kutoka iliyokuwa OAU aliomba sana aruhusiwe kujiunga na jumuiya ya ulaya lkn walimtolea nje kwa madai kwamba hiyo jumuiya ilikuwa ni kwa mataifa ya ulaya tu.
 
Ukiacha wanakoita peponi; there has never been any other alliance mwenye akili angetamani kujiunga nao zaidi ya US and EU. That's the fact.
 
Ukraine wanajutia kwa kua na msimamo wa kujiunga na EU na Nato, wengi wana mkosoa Zere kwa kutoona mbali, Russia hawezi Kubali kitu kama hicho na US inajua hilo Hook or crook Russia hawezi kukaribisha Nato mlangoni mwake. ...........kura za maoni 80% hamtaki zere tena wala hawataki kujounga na Nato tena
Una uhakika na unayosema mkuu. Ukraine yenyewe ilitaka kujiunga na ulaya zele wala hakuwa na ndoto za kuwa raisi. Na maandamano ndio yaliyomtimua Rais aliyekuwepo siku nyingi
 
Back
Top Bottom