Gerald Hando: Nitanunua Jezi ya Taifa Stars, Lakini sio hizi Mpya

Gerald Hando: Nitanunua Jezi ya Taifa Stars, Lakini sio hizi Mpya

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mtangazaji wa Wasafi Media kipindi cha 'Good Morning', Gerald Hando, ameweka wazi msimamo wake wa kutokuvutiwa na muundo (design) wa jezi mpya za timu ya taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars, zinazotarajiwa kutumika katika michuano ijayo.

Akiwa anazungumza kwenye kipindi hicho, Hando ameeleza kuwa ingawa ana mpango wa kununua jezi ya timu ya taifa, hatanunua aina ya jezi iliyopo sasa kutokana na muonekano wake kutomvutia na kusema anaungana na maoni yaliyotolewa awali na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.

"Mimi nina mpango wa kununua bila shaka, lakini sio hizi. Kama wakibadilisha nitanunua. Hizi hazijanivutia kabisa, muundo na muonekano wake sijazipenda... Naungana na Makonda, sio tamu kwa ajili ya timu ya taifa inayoelekea michuano mikubwa kama AFCON," alisema Hando.

Amedai kuwa, nguo au jezi za timu ya taifa zinapaswa kuwa na mvuto wa kipekee unaomfanya mtu ajisikie fahari kuivaa, hata kama si mshabiki wa kawaida wa timu hiyo kama ilivyo kwa jezi za timu nyingine kubwa duniani kama vile Ujerumani.



soma
 
Hata kama Taifa stars watavaa jezi za magunia, let them focus kwenye kuleta ushindi.
Haijalishi paka ni mweusi au mweupe, muhimu akamate panya!
Nadhani sasa discussion kubwa iwe, tunaiwezeshaje Taifa stars kuleta ushindi? Na sio maswala ya jezi.
 
Sasa ata akinunua mbn uwezi kujisifia kwa nchi ya watu wajinga wajinga wanaoona ujinga na wanafurahi
 
Chawa pro max anazeeka vibaya, huyu mnafiki sana ndiyo maana aliwasaliti masud na Fina Enzi zile.
 
Back
Top Bottom