Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Hongera sana.Naamini ulitumia muda kusoma na kuandaa habari hii.Imenivutia na vyombo vyetu vina la kujifunza hapa (Reasoning kabla ya kutumia maguvu na enhanced methods of interogation)
Nashukuru sana Mkuu..

Kabisa kipo cha kujifunza kutoka kwa wenzetu! Vyombo vyote vya usalama viwekeze kutumia akili nyingi zaidi na intelijensia badala ya kutegemea nguvu peke yake
 
September 11, hawatakuja kuisahau Wamarekani na pia watawakumbuka Waisrael Walipowaambia wawauzie expertise Kwenye aviation security wao wakaona ghali kwa nchi "cheap" kama Israel
 
hii ni movei tu km zile vandame hakuna ukwel ktk hiyo stori hivi kijana apewe mafunzo ya hali ya juu then apewe dola 2800 tu? hakuka sehem osama alipanga mashambuliz ya trade centre ukwel unajulikana america alipanga mwenyewe shambuliz ili apate leseni ya kwenda kuuwa binadam afghstan na kwenda kuiba mafuta.osama ajawai kuteka ndege za kwenda kupiga amerika ni uongo uliotukuka
Kupewa dola 28000 inawezekana kabisa ilikuwa ni moja wapo ya mbinu kwao wakidhani pengine angepewa mzigo wa maana ingebidi achunguzwe zaidi.
ila pia kiongozi usiseme ni sinema, haya mambo ni kweli yapo. Jaribu kupitia baadhi ya operations mfn, Mask Alabama Hijacking, operation Red wings...na mpaka movie wametoa (Captain Phillip na lone survivor) sio mbaya ukapitia waisrael operation yao 90 minutes at Entebe. Hapo ndipo utaona kuwa Idara za usalama zipo juu na hawakurupuki tu, ni zaidi ya sinema
 
Daktari ambaye alitoa chanjo (Shakil Alfridi) alijulikana na alikamatwa mwaka mwaka 2012 kama sikosei, na kwa muda mrefu sana alishikiliwa na Serikali ya Pakistan katika magereza yao..
Kushilkiliwa kwake kulileta tension sana kati ya Marekani na Pakistan mpaka ikafikia hatua Marekani wakapunguza misaada ya kijeshi kwa Pakistan ili tu kuwapa presha Pakistan..

Marekani walikuwa wanadai kuwa Dk. Shakil Alfridi anapaswa kupongezwa na kupewa ulinzi kwa kuwa amesaidia kumtia nguvuni gaidi namba moja duniani na sio kuwekwa gerezani.
Lakini Pakistan walidai kuwa kitendo cha Dk. Shakil Alfridi kushirikiana na kusaidia taifa la kigeni kufanya ushushushu na oparesheni ya kijeshi ndani ya Pakistan kilikuwa ni kitendo cha Uhaini na kamwe hawawezi kumuachia.
Huu mzozo ulikuwa mkubwa sana na sijui waliumalizaje baadae..
Please ifuatilie hatima ya huyu Doctor yawezemana wameshamtia kitanzi tayari
 
Huyu Doctor alihukumiwa kama sikosei ni 2011 kama sio hivyo ni mwanzoni 2012 kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia kuhusu mauaji ya Osama
Hivi hao Waarabu hawakuwa na mpango hata wa kumkamata Osama pamoja na ugaidi aliokuwa ameufanya?
 
Dah huyo Abu Ahmed al-Kuwait alishindwa kuishi kama yupo kwenye nyakati za zamani, alimponza Bin Laden
sababu yeye ndio alikuwa anaongea kama osama,asingengeweza calculate ni kwa muda gani wamejificha?/walikuwa watu brave sana sema walipambana na dunia haikuwa rahisi kujificha
 
Vile vile katika ripoti hiyo ya commission inamtaja afisa mmoja wa shirika la kijasusi la Pakistani (ISI) kuwa kuna uwezekano alihusika katika njama za marekani kumkamata Osama kwa kuwa wiki moja kabla ya tukio la kumkamata Osama, aliwatuma watu kukata miti mikubwa iliyokuwa inazunguka ile nyumba Abbottabad ikiwa ni maandalizi ya helicopter kutua. Vile vile baada ya tukio la kukamatwa Osama aliuza vitu vyake na kuondoka Pakistani. Tofauti kati ya mashirika ya intelligence ya huku kwetu na nchi zilizoendelea ni kuwa wenzetu mashirika yao yanafanya mission zenye maslahi kwa taifa siyo kwa chama tawala. Ndio maana mission ikishakamilika wanatoa taarifa yote in detail kasoro baadhi tu ya tactics ambazo wanaona wataendelea kuzitumia kwenye mission nyingine. Huku kwetu mission zilizojaa TISS ni zile za kukandamiza Upinzani kama kumuua Kombe, kuua viongozi wa upinzani, kuwarushia mabomu Chadema n.k hizi mission hauwezi kuja kujua ukweli mpaka mmoja wao awageuke aropoke. Wenzetu mission zao zinakuwa high classified, lakini ikishakamilika tu wana-disclose kila kitu. Kwa mfano mission ya kumkamata Khaleed Sheikh Mohamed (KSM) the ring leader and mastermind wa 9/11 na akina Ramzi Yousef inajulikana ilifanywaje. Walifuatilia trail ya hela zote zilizokuwa wired kwenye account ya Mohamed Attar (kiongozi wa magaidi waliobamiza ndege WTC) Walianzia Dortimund Ujerumani ambakao Mohammed Attar alikuwa anasoma master of Science in Urban Planning katika chuo kikuu cha Dortimund. Walifuatilia trail ya ufadhili wa hela, msikiti aliokuwa anaswali hadi wakajua cell yao ilikuwa na kina nani, safari zake Pakistani na watu aliokuwa anakutana nao. Mohamed Attar ndio alikuwa ana-distribute hela kwa wale wengine za kusomea u-pilot wa ndege marekani. lakini hadi wanasomea upilot walikuwa hawajui mission yao itakuwaje. aliekuwa anajua mission ni KSM na Mohamed Attar. Kuna gaidi mmoja ambaye alikuwa yupo kwenye kikosi cha kwanza lakini alinyimwa viza ya kuingia marekani ndio alimtaja KSM kuwa ndie aliekuwa anawafadhili. Tofauti na kina Osama, KSM alikuwa anaishi maisha ya kifahari, anaingia kwenye club za usiku, anatumia vileo, anatumia simu, anachukua machangu, hakuwa anaishai maisha ya kiislamu. Kosa la kwanza na kubwa ambalo KSM na Ramzi walilifanya ni kumualika mwandishi wa habari wa Al-jazeera kwenda kuwahoji Pakistani. Ikieleweka kuwa kabla ya 9/11, Osama alikuwa anajulikana lakini hakuwa maarufu sana, hivyo kulikuwa na struggle kati ya magaidi kila mtu akitaka kupata umaarufu kuwa yeye ndio gaidi zaidi. Hiki ndicho kiliwasukuma KSM na Ramzi kumualika yule mtangazaji wa Al-jazeera kwenda kuwahoji. Yule mtangazaji alienda Islamabad akafungwa kitambaa usoni akazungushwa kwenye gari kuanzia asubuhi hadi jioni ili asijue muelekeo, mwishowe akashushwa kwenye gari wakamuingiza kwenye nyumba ambayo ina bunker alipofunguliwa kitambaa akakutana uso kwa uso na KSM akiwa na Ramzi Yousef. Pale KSM aka-declare jihad against American na ku-confess yeye ndiye aliyepanga na ku-finance mission nzima ya kubamiza ndege WTC. Yule mtangazaji wa Al-jazeera alipomaliza kuwahoji akaomba aondoke na Video footage wakamkatalia ila wakamruhusu achukue Audio record, hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa sana maana ile audio iliporushwa tu Al-Jazeera, CIA wakaenda kuichukua Al-Jazeera wakatenganisha voice print za kila mtu alieongea kwenye ule mkutano wakaingiza kwenye mashine yao inayo-identify voice print ya kila mtu kama finger print. Hapo ndio ukawa mwanzo wa Drone attack Pakistani. Mtu akiongea kwenye simu kabla hajakata simu anashangaa bomu limeshatua. Kuna tukio moja walikuwa wamewasiliana wahudhurie harusi na Ayman Al Zawahil atakuwepo, machale yakawacheza Zawahili hakwenda, ile harusi ilibutuliwa na drone walikufa watu ukoo mzima. Baada ya kukamatwa Ramzi, KSM alistuka kuwa anafuatiliwa kwenye simu hivyo alikuwa hatumii simu yake, anaomba watu atumie simu zao ndio maana zoezi la kumkamata KSM lilishindikana zaidi ya mara 20, wakimtrace sehemu wakienda hawamkuti, alikuwa halali sehemu moja mara mbili mfululizo, Mpaka walipoamua kumtengenezea ramani kwa kutumia simu anazotumia, waka-identify sehemu 14 ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kumkuta. Hizo sehemu zote zikafanyiwa kitu kinaitwa "synchronized ambush", yaani vikatengenezwa vikosi 14 vya askari wa Pakistani vikishirikisha maafisa wa CIA katika kila kikosi ambavyo vita-ambush sehemu zote 14 kwa muda mmoja, hapo ndipo walipomkamata KSM lakini walichoshangaa ni kuwa kwenye location moja katika zile 14 walikuta kiwanja hakina nyumba. walipofuatilia waya wa simu unaotumika kwa ID ya kiwanja hicho uko kwenye nyumba ipi ndipo ofisa wa ISI mtaalamu wa IT akai-trace nyumba inayotumia ID ya kile kiwanja humo ndipo walipomfurumusha na kumpiga risasi Abu Zubeida ambaye alipelekwa kutibiwa ujerumani akapona na kutoa siri kibao.
 
Daktari ambaye alitoa chanjo (Shakil Alfridi) alijulikana na alikamatwa mwaka mwaka 2012 kama sikosei, na kwa muda mrefu sana alishikiliwa na Serikali ya Pakistan katika magereza yao..
Kushilkiliwa kwake kulileta tension sana kati ya Marekani na Pakistan mpaka ikafikia hatua Marekani wakapunguza misaada ya kijeshi kwa Pakistan ili tu kuwapa presha Pakistan..

Marekani walikuwa wanadai kuwa Dk. Shakil Alfridi anapaswa kupongezwa na kupewa ulinzi kwa kuwa amesaidia kumtia nguvuni gaidi namba moja duniani na sio kuwekwa gerezani.
Lakini Pakistan walidai kuwa kitendo cha Dk. Shakil Alfridi kushirikiana na kusaidia taifa la kigeni kufanya ushushushu na oparesheni ya kijeshi ndani ya Pakistan kilikuwa ni kitendo cha Uhaini na kamwe hawawezi kumuachia.
Huu mzozo ulikuwa mkubwa sana na sijui waliumalizaje baadae..
The Republican presidential front-runner waded into the controversysurrounding Afridi's imprisonment during a recent interview on Fox News in which he said he’d get Afridi released in "two minutes."

"I would tell them let [him] out and I'm sure they would let [him] out," Trump said. "Because we give a lot of aid to Pakistan."

Trump's statement drew a strong response from Pakistani Interior Minister Chaudhry Nisar Ali Khan, who released a statement on Monday saying that Pakistan had sole authority to handle Afridi’s case.

“[N]obody else has the right to dictate to us about his future,” Khan said. “Trump’s statement only serves to show not only his insensitivity, but also his ignorance about Pakistan.” Hii ni ya Mei 2016 labda Trump akiwa raid atamtoa!
 
Issue ya doble agent inatumika sana katika hizimission ili ku-infiltrate enemy territory ingawa sometimes inback-fire.Successful mission mojawapo iliyotumia double agent ni ile iliyomuua yule imamwa yemen mzaliwa wa marekani Anwar Al Awlaki. Huyu alikuwa anatafutwa namarekani kwa kuhusika kwake na 9/11 ambapo ilikuja kujuikana kuwa hijackerswatatu wa 9/11 walikuwa wanasali kwenye msikiti wake. Vilevile moja waoalieongoza flight 77 alikuwa na namba yake kwenye diary yake. Huyu imamalikimbilia yemen akajificha huko. Kilichomponza ni kuwa mahubiri yake mengialikuwa anayapost kwenye U-tube mpaka kuna wakati CIA waliomba kibali congressili waondoe baadhi ya mahubiri yake yaliyokuwa yana-incite jihad kwenye utube.Sasa alipokuwa yemen CIA kwa kushirikiana na Danish Intelligence Agency PETwakam-recruit kijana mmoja wa denmak ajulikanaye kama Storm aende akazoeanenaye. Yule kijana akajifanya nye ni sympathizer wa jihadi akawa naye anachangiakwenye mahubiri anayotoa Anwar kwenye internet mwishowe akaenda yemen kukutanana Anwar. Anwar akamweleza kuwa anapanga kushambulia kwenye ma-supermarketmakubwa marekani kwa kutumia biological weapons. Baada ya mahusiano ya mudamrefu Anwar akamwomba amnunulie Flash am-downloadie magazeti ya marekani iliajue wanamwandikaje kwa kuwa yeye alikuwa mafichoni. Hapo ndipo CIA wakampaStorm flash disc yenye tracking micro-chip. Wiki moja tokea ampe ile flash CIAwalituma drone ikamuua akiwa kwenye gari na wenzake watatu baadae kakamuua namtoto wake.

Lakini hii technique yak u-recruit doble agent huwasometimes inaback-fire kwa sababu huwa subjected to loyality. Si unakumbukakule Afghanstani kwenye base ya marekani ya kupambana na mitandao ya kigaidi yaalqaeda, Haqqan na talebani inayojulikana kama CAMP CHAPMAN kilinuka mwaka2009. CIA na Jordanian Intelligency walim-recruit Jordanian doctor aliyekuwaanasympathize na Alqaeda aliyejulikana kama Humam Khalil Abu-Mulal al-Balawiakawa “TRIPLE AGENT”, Huyu anatoka kijiji kimoja na Alqaeda leader inMesopotamia Abu Musab Al Zarqawi. Sasa Al Balawi alifanya kazi na CIA na kuwapataarifa za ukweli walipo wapiganaji wa Alqaeda na ikawa ni kweli CIA wakitumadrone inawaua. Si wakamwamini, akawaambia yeye atawafanikishia CIA kumuua aukumkamata Ayman Al Zawahil, CIA wakaingia mkenge akawa akiingia kwenye base yaoya chapman hawamsachi. Siku akawadanganya anataarifa muhimu sana kuhusiana naAl Zawahil hivyo anahitaji kuonana na top officials wa CIA, Basi yule mamaambaye alikuwa Chief of operation katika ile base anaitwa Jennifer Lynne Matthews akawaita hadimaafisa wengine wa CIA kutoka Kabul, alipofika getini hakusachiwa ingawa kunamageti matatu, maofisa wote wakatoka kumpokea nje, kumbe kajifunga bomu la kilo15 akalilipua aliua watu 9 palepale na wengine kadhaa kujeruhiwa. Hii ndio riskya ku-recruit double agent hauwezi kujua loyality yake ipo kwa nani. Mara baadaya kujitoa muhanga na kuuwa maofisa wa CIA, Al Balawi alionekana kwenye videofootage iliyorushwa kwenye channel za TV Pakistani akiongea kuwa amefanya liletukioa kama kulipiza kisasi cha kiongozi wa Alqaeda Pakistani Baitullah Mehsud aliyeuwawa na CIA kwa drone
 
Back
Top Bottom