FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #61
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+
UKURASA WA KUMI NA SABA
TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI NA SITA
"Relax mimi sio mbaya wenu nipo hapa kuwasaidia" aliongea akiwa anashusha kitambaa usoni kwake machozi mengi yalikuwa yanamtoka.
"Wewe ni nani?" Aliuliza mwanamke mmoja ambaye alionekana kuwa shupavu miongoni mwao wale wanawake.
"Ni komando wa nchi hii nimekuja hapa kumaliza hili kundi lote la hawa magaidi na nyie kuanzia saivi mpo huru mnaweza kuondoka humu ndani" waliangaliana kwanza kila mtu alibaki anamshangaa hakuna aliye amini kwamba wanaweza kutoka kwenye sehemu ambayo wao kwao ilikuwa ni jehanamu kama hii eti leo walikuwa huru ilikuwa inashangaza sana.
ENDELEA........................
Wanawake wote mle ndani walikuwa wameamka tayari walibaki wanamshangaa sana Aariz kauli zake hawakuwa wakiziamini kabisa Kwa namna alivyokuwa ametapakaa damu ikabidi awasimulie kidogo namna alivyo fanikiwa kuingia ndani ya kambi hiyo mpaka muda huo ambao alikuwa mbele yao hapo, baadae walimuelewa vizuri tu hiyo ilimrahisishia kazi yake alianza kusaidiana na yule mwanamke ambaye alikuwa kiongozi kuwatoa wanawake hao humo ndani aliwaacha wakawa wanaelekea porini sehemu ambayo ilikuwa na miti mingi sana na huko kulikuwa na kiza kinene.
"Una uhakika utawafikisha wenzako salama?" Aariz alimuuliza mwanamke huyo akiwa anamalizikia kutoka mlangoni, aligeuka na kumwangalia mwanaume huyo.
"Nilikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa humu ndani mpaka siku ambayo nilifanya jaribio la kutaka kuwasaidia hawa mateka nilikamatwa na kuwa mmoja wa mateka humu ndani kwahiyo hii kambi naijua mpaka nukta ya mwisho wake na kila aina ya ulinzi hapa naijua vizuri hawa nitawafikisha ila naomba nikushukuru sana kwa msaada wako mkubwa" Aariz alitabasamu Kwa mbali sana akiyafumba macho yake.
"Naomba unitajie jina lako ipo siku nitakuja nikutafute" sauti ya mwanamke huyo ilimshtua akafumbua macho yake na kumwangalia mwanamke huyo kwa umakini Sana alisikitika Kwa sababu wasingeweza kukutana tena kwenye maisha yao yote ila aliamua kumtajia tu jina lake.
"Aariz" dada wa watu alipotelea porini kuwaongoza wenzake ambao hawakuwa wakijua lolote kuhusu hiyo sehemu, dakika zilipita tatu tu Aariz alisikia alamu inapiga Kwa sauti kali sana akajua tayari ishajulikana humo ndani sio mahala salama sana, alicho kifanya alikaa chini akaweka silaha zake zote pembeni akaanza kusali akiwa amekaa amefumba macho yake mithili ya mashoulini wa kichina wanavyo fanya pale wanapokuwa kwenye imani zao na maombi mazito. Mboni za macho yake zilihisi uwepo wa vivuli vya watu humo ndani lakini hakuyafumbua macho yake mpaka ilipopita dakika nzima alinyanyuka ubavu wake wa kulia ukiendelea kuvuja damu aliokota silaha zake na kuziweka sehemu yake kwenye mwili mkononi alibakia na upanga mmoja tu ambao alikuwa akiuamini sana anapokuwa sehemu hatari kama hizo, alishtuka na kuguna watu ambao walikuwa mbele yake walikuwa ni tofauti kabisa na ambao alikuwa amekutana nao mwanzo hawa walikuwa watano tu walivaa nguo nyekundu ambazo zilikuwa ni safi mno lakini nyuso zao zilifunikwa na vitambaa vyeupe hiyo ni alama mbaya sana kwenye suala la mapigano watu wanaotumia nguo nyeupe huwa ni wa kutisha sana, nywele za mtu mmoja kati yao zilionyesha wazi alikuwa mtu wa Japan alilazimika kuukaza mkono wake alikuwa mbele ya viumbe vya ajabu na mmoja japo hakuwepo ilimpa mashaka makubwa mno hakuelewa huyo wa sita yuko wapi.
"You are the one who killed our guards right?" Hapa ndipo alipogundua kwamba hawa hawakuwa waarabu kwa sababu walikuwa wakiongea kiingereza ambacho kilikuwa kimechanganyika na lafudhi ya kikorea na kichina.
"I'm here to kill you all" ndiyo kauli ambayo ilitoka kwenye mdomo wake huku akiwanyooshea upanga wanaume hao watano lakini alishangaa mmoja mmoja anajigawa na kwenda kukaa mbele yake alibakia mwanaume mmoja tu ambaye huyo ndiye aliyetakiwa kusimama naye kwenye mapigano, nyota ndogo ndogo zilikuwa zinakuja kwa nguvu alizipangua tatu kwa upanga wake bahati mbaya sana moja ilimuingia pale pale palipokuwa na jeraha ubavuni ni wazi mwanaume huyo alikuwa ashajua sehemu hiyo yenye tatizo, Aariz aliishika sehemu hiyo baada ya damu kuongezeka alishtuka na kurudi nyuma baada ya kuona imeanza kutoka damu yenye rangi nyeusi hizo nyota zilikuwa na sumu kali kupita kiasi. Uwepesi wa ubongo wake ulimpa taarifa hizo silaha zilikuwa na sumu kali mno hapo alikuwa na dakika chache sana za kuwakimbia au kuwamaliza watu hao ili akatibiwe haraka vinginevyo alikuwa anakufa akiwa anajiona.
Upanga ulikuwa unakuja alifanikiwa kuukwepa ulipitiliza ukaenda kutoboa ukuta mjapan huyo alijipindua na kupiga kwenye kifua cha Aariz alidondoka chini na kutapika damu teke lililo ingizwa hapo lilikuwa na uzito wa tani kadhaa aliyakumbuka maneno ya mwanamke ambaye alikutana naye nje ya kambi wakati anaingia alivyo mwambia kwamba kama akifanikiwa kutoka salama basi atakuwa moja ya binadamu wenye bahati sana ambao waliishi kwenye kizazi hiki. Ilitakiwa atumie kila uwezo alio nao ili atoke humo ndani mlango ulikuwa umefungwa aliyafumba macho yake kwa hisia akiwa bado yupo chini mjapan alikuwa amemfikia alirusha upanga wake ili kuitenganisha shingo ya mwanaume huyo alijikuta amepiga hewa hapakuwa na kitu chochote alishtuka sana tumbo lake lilikuwa linamwaga damu Kwa wingi alijigusa na kugundua mtu huyo alinyanyuka Kwa kasi na kulikata tumbo lake alidondoka chini akiwa ameshikilia utumbo wake kitambaa kilimtoka usoni alikuwa ni kijana mdogo sana mpaka Aariz mwenyewe alishangaa inawezekanaje kijana kama huyo kuwa mtu wa kutisha hivyo.
Wenzake wote wanne walijikuta wakisimama Kwa mshangao hawakuwa na matarajio mwenzao angeuliwa kirahisi sana namna hiyo, walijikuta wanamshambulia mtu huyo kwa wepesi sana walitaka kumhusisha na uchawi lakini walikuwa vitani ungekuwa ni upotezaji wa muda nyota tano zilifanikiwa kutoka na nywele zake tu hakuna iliyo mpata alitishia kuingia kwatikati Kwa kasi halafu akasimama wanaume wawili walizamishiana panga zao wenyewe alikuwa amewachonganisha wakati wanashangaana alipita na shingo ya mmoja mpaka muda huo ambaye alikuwa amebaki salama alikuwa ni mmoja tu. Alijichanganya baada ya kutishiwa akakubali kwenye Aariz alidunda kwenye kifua cha mwanaume huyo ambaye alijizoa na kwenda kujibamiza kwenye moja ya kuta humo ndani alitaka kusimama kisu kilipita kwenye koromeo na kutokezea nyuma kwenda kukita ukutani, Aariz alidondoka chini na kupiga goti lake damu nyeusi ilikuwa inamtoka kwenye jeraha lake ilikuwa ni alama mbaya mwili ulianza Kwa mbali kupoteza nguvu yake ila bado alikuwa na kazi nzito mbele yake alielewa yule mmoja ambaye hakuwa hapo alikuwa ndiye anamlinda bosi wake na huenda ndiye huyo aliye ambiwa kwamba alikuwa ni mtoto wa bosi. Alitoka nje kwa kujivuta mpaka nje alitoa maji ambayo ilikuwa ni dawa ya kuongeza nguvu yalikuwa ya baridi mno alibugia nusu ya maji kidogo mwili ukawa na nguvu za kumuwezesha kutembea, alitukana baada ya kuona hata macho yanataka yaanze kumsaliti kuona.
Aliangalia saa yake Kwa umakini.
"I have remained only with ten minutes to get out of here damn" aliongea huku akiihisi maumivu makali sana alikuwa na dakika kumi za kumaliza kazi, aliliangalia lile ghorofa kubwa ambalo lilikuwa limezimwa taa zote kulikuwa na kiza sana, baada ya kuliangalia Kwa muda wa dakika mbili tu ramani nzima ilikuwa kichwani mwake hiyo ndiyo taaluma aliyo isomea Kwa miaka yake yote hivyo alikuwa akiijua kuliko hata jina lake, hakuwahi kuingia humo ndani ila Kwa aina ya nyumba ilivyojengwa haikumpa shida kabisa kuelewa namna nyumba hiyo ilivyokuwa imejengwa. Alijikongoja mpaka mlangoni mlango ulikuwa upo wazi kabisa hii ilimtia shaka sana Kwa mtu kama yeye hiyo ilikuwa ni ishara mbaya mno alitembea kwa hatua kumi alisimama baada ya moyo wake kudunda sana alisimama na kutulia mwanga mkali ulimfanya ayafumbe macho yake mkononi akiwa na upanga ambao ulikuwa unatoka damu nyingi sana hata yeye mwili ulitapakaa damu sana mkono wake mmoja wa kushoto aliutumia kushika kwenye ubavu wake wa kulia ambao ulikuwa unavuja damu nyeusi.
Wanaume wawili na wanawake kumi walikuwa wanamtazama, mmoja alikuwa amekaa na wanawake karibia wanne walimkalia wakiwa wapo nusu uchi huku wangine sita wakishindana kumpa huduma wakati mwanaume mwingine alikuwa amesimama pembeni ya mwanaume huyo akiwa ameikumbata mikono yake ni wazi waliutarajia ujio wake humo ndani ndio maana waliacha mlango wazi, aliyekuwa amekaa alikuwa anaitwa Bashiru Hazir huyu ndiye alikuwa mkuu wa hii kambi ya kigaidi na ndiye aliyekuwa chanzo cha mambo yote ambayo yalisababisha vita hili eneo la kusini mwa Libya pembeni yake alikuwa ni mwanae wa kumzaa na ndiye aliyekuwa mlinzi wake mkuu alijulikana kama Abushiri Hazir. Aariz aliliangalia kwa umakini hilo jengo bila kuongea chochote alikiangalia kidonda chake na kujisikitikia, hakufanya hivyo kwa bahati mbaya mtu ambaye alikuwa mbele yake ndiye aliyempa hofu ya kufanya hivyo angekuwa timamu ilikuwa ni kazi rahisi tu ila hali aliyokuwa nayo alihofia sana, Abushiri alikuwa kwenye mavazi meupe na usoni hakujifunika chochote ilikuwa ni bora na wale watano ambao walikuwa na vitambaa vyeupe tu vya usoni sasa huyu nguo zake zote zilikuwa nyeupe na usoni hakuwa na chochote alimtishia mno alielewa sio binadamu ambaye unaweza ukamgusa kiwepesi sana.
"Haya yote umeyafanya Kwa sababu tu ya pesa au kuna mengine nyuma ambayo hayajulikani?" Aariz alimuuliza mzee ambaye alikuwa yuko busy na wanawake wala hakujali kama humo ndani kulikuwa na mgeni.
"Ogopa sana neno pesa na nguvu kwenye maisha yako, kwanini umeamua kuyatoa maisha yako sadaka kirahisi sana namna hii unajua kabisa siwezi nikakuacha ukiwa hai kwa hicho ulicho kifanya" ni sauti zito na baya lilitoka Kwa mtu huyo alionekana kuwa mkatili sana.
"Hey ladies get out of here" aliongea kwa sauti ya kawaida tu lakini hakuna kilichotokea.
"Hey I say out" aliongea Kwa sauti ya ukali mpaka alitoa damu kwenye mdomo wake, wanawake hao waliogopa sana na kuanza kusogea nyuma, Aariz Alifanya shambulio la ghafla Sana kwa kurusha visu vyake viwili pale alipokaa yule mzee, alishuhudia kitu ambacho hata yeye mwenyewe kilimtisha sana visu hivyo vilidakwa Kwa vidole vinne tu vya yule mwanaume ambaye alikuwa pembeni vilirudishwa kwake alividaka lakini mkono wake ulipata maumivu vilitoka kwenye mikono ya mwanaume mwenye nguvu mno.
"Kill him" ni sauti moja tu ya mamlaka kutoka kwa yule mzee ambaye alionekana kuongea kawaida ila alikuwa na uchungu na hasira sana kambi yake ilikuwa imeharibiwa vibaya sana, alitaka kutoka humo ndani baada ya kuona wanawake wale wamekimbilia nje na kuanza kusambaa hovyo hovyo hayo mambo yalikuwa hayawahusu kabisa ya vita Aariz aliurusha upanga wake baada ya kupigwa mapigo makali kutoka Kwa mwanaume ambaye alikuwa amesimama nbele yake, upanga huo ulienda kuzama kwenye mgongo wa yule mzee alidondoka chini akianza kutapa tapa.
"Dadiiiiiiii" yule mwanaume aliita kwa uchungu sana na kuanza kumpiga Kwa hasira Aariz kwenye mbavu zake mwanaume alizidi kutapika damu ila ghafla alipotea yule mwanaume alianza kuhangaika kumtafuta huku akipiga kelele na kumtaka ajitokeze, hali yake ilikuwa mbaya sana alikuwa amesimama nyuma ya mwanaume huyo kiganja kizito kilitua kwenye shingo ya Abushiri na kumfanya apinde kidogo hata hivyo alirusha teke ambalo lilidakwa na mguu wake ulivunjwa alipiga kelele na kutoa bastola yake ambayo ilitoa risasi tano zote zilizama kwenye ubavu wa kulia ule ule ambao Aariz alikuwa ameharibiwa vibaya sana, maumivu makali mno yalitembea Kwa spidi kwenye mwili wake akiwa anatoa damu nyingi sana ubavuni na mdomoni alikunja vidole vyake na kuzamisha kwenye shingo ya Abushiri na kuikata mishipa ya shingoni mwanaume huyo alipiga kelele akiwa anajibamiza chini maumivu aliyo yapitia ni wazi yalimpa uchizi, Aariz naye alikuwa chini akiwa kwenye hali mbaya alimshuhudia mwanaume mwenzake akiwa anakata roho alijivuta mpaka alipokuwa anahangaika yule mzee aliuchomoa upanga wake Kwa nguvu hali iliyo mpa mzee yule maumivu makali sana.
"Huu sio mwisho huu ni mwanzo tu wa haya mambo hahahahahaha..." Aariz hakutaka kujisumbua kutaka kujua hiyo kauli za mzee huyo ilimaanisha nini aliamua kupita na shingo yake akanyanyuka kwa kuyumba yumba na kuanza kuondoka hilo eneo macho yake yalikuwa yamepoteza nuru alitoa saa ambayo aliichukua kwa yule mwanamke aliminya kwenye alama ya kijani milango yote ilikuwa wazi alitembea kwa muda kama dakika ishirini akiwa anaona Kwa mbali sana, alimshukuru MUNGU baada ya kuliona gari lake alikuwa tayari yupo nje ya pori alipanda na kutoa limoti ambayo aliichukua mle ndani Kwa wale wanaume sita wa mwanzo aliibonyeza ulisikika mlipuko mkubwa ambao hata yeye hakutegemea kuusikia tetemeko zito lilipita na kumfanya aondoe gari lake haraka hilo eneo lakini macho yake yalimsaliti alipapasa simu pembeni yake MUNGU alikuwa upande wake aliipata alitafuta kwa haraka namba moja na kupiga haikuchukua muda ilipokelewa.
"I'm dying" ni kauli yake moja tu aliitamka haikusikika sauti nyingine tena simu ikiwa bado ipo hewani.
"Kheeeee aliwezaje kuishi tena?" Takribani masaa 27 mpaka muda huo raisi na mzee huyo walikuwa wamekaa ndani ya chumba hicho kichafu sana cha GEREZA akiwa anasimuliwa historia ya huyo mtu aliingilia kati kuulizia aliweza vipi kupona kwenye hiyo hali, mzee huyo aliinama na kuinua uso wake na kuufungua tena.
"Huo ndio ulikuwa mwanzo wake wa kuwa binadamu ambaye ataishi miaka mingi sana akiwa bado yupo hai na itamchukua muda sana kuzeeka" raisi alishangaa mpaka akasimama alitamani kuondoka ila hilo lingemfanya asijue chochote kabisa kuhusu hadithi ambayo ni kama ilikuwa imefikia katikati hakuhitaji kuikosa hata nukta alirudi tena na kukaa chini ili apewe alicho hitaji kujua.
Kuna siri gani nyingine nzito sana kwenye historia ya mwanaume huyu? Ni kweli ataishi miaka mingi? Kivipi? GEREZA LA HAZWA naweka nukta ukurasa wa 17 tukutane wakati ujao.
Langu jina wananiita
Bux the story teller