Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA TANO

TULIPO ISHIA UKURASA WA ISHIRINI NA NNE
"Nadhani umenielewa vizuri Mr Leone" aliongea kwa majigambo hakujua kama kila anacho kiongea ndani ya hiyo ofisi yake kilikuwa kinasikika ndani ya masikio ya mwanaume ambaye alikuwa anajulikana kama Josephat, alisikitika sana na kumsikitikia kijana huyo alikuwa amefanya moja ya makosa ambayo ilikuwa ni ngumu sana kusameheka. Alikumbuka vyema wakati TARIQ ameenda kumuita mwanasheria wa kampuni alichunguza kwa umakini sana kwenye ofisi hiyo hakuona kamera yoyote kuna kifaa kidogo mithili ya kiwaya ambacho alikibandika chini ya meza ya TARIQ hivyo alikuwa akisikia kila kilichokuwa kinaendelea humo ndani, walikuwa wamefika chini alitabasamu na kuingia kwenye gari safari ya kwenda hotelini ilianza.

ENDELEA...................
TANZANIA
Qader aliamka mchana wa jua kali baada ya kuhisi joto kali sana kwenye mwili wake, nguo zote zilikuwa zimelowa kwa jasho ambalo lilikuwa likimtoka kama maji, kichwa kilikuwa kinamuuma sana mpaka muda huo alitamani aendelee kulala ila hali ya ndani ya chumba hicho iliendelea kumsaliti sana hakuweza kuvumilia alisimama na kutulia. Kumbukumbu zilipita mbele ya ubongo wake alikumbuka vyema usiku wa jana yake alikuwa akimhoji mtu humo ndani lakini mambo ambayo baadae alikuja kuyasikia yalimtishia sana alibaki anashangaa ni kivipi mtu yule aliweza kuwa namna ile alijifuta jasho usoni kwa mkono wake mmoja alihema na kutoka humo ndani, alinyoosha moja kwa moja kwenye chumba chake cha kazi vijana wake walimshangaa inakuaje kiongozi wao amelowa namna hiyo na tangu asubuhi hawakuwa wamemuona kabisa ndani humo japo hawakuwa na haki ya kuuliza chochote walikuwa wanamjua akiwa na hasira kama Kuna mtu angemuongelesha hapo angeondoka na shingo yake muda huo huo.

Baada ya kuingia kwenye hiyo ofisi ambayo hakuna kijana wake hata mmoja ambaye alikuwa anaruhusiwa kuingia alifunga kila sehemu na kuelekea kwenye kabati moja kubwa sana ambalo lilikuwa ndani humo alilivutia pembeni kidogo na kukutana na ukuta mkubwa ambao ulikuwa na box dogo lilikuwa na namba nyingi sana, aliingiza namba kwa idadi ya 20 kwa kuzichanganya haraka haraka sana palifunguka ulikuwa ni mlango mkubwa sana kisha akaparudishia kama palivyokuwa mwanzo. Mbele yake ilikuwa ni ofisi moja nzuri sana na huko ndiko alikokuwa anayafanya mambo yake ya siri pasipo mtu yeyote yule kujua. Alifungua droo ya kwenye meza yake kulikuwa na pesa nyingi sana na bastola pamoja na passport nyingi zenye sura tofauti tofauti za kusafiria.

"Huyu mtu anasema nimekosea sana kufanya vile kwenye ile familia kwani hawa watu wawili ni akina nani hasa kati ya JITI MAALIMU na huyo ZAKARIA MANSOUR who are they? na huyu mtu amejua vipi kuhusu suala la familia yangu kitu ambacho hata bosi wangu hajawahi kukijua?" Alijiuliza maswali mengi majibu yake hayakuwezekana kabisa kuyapata kama alivyo hitaji yeye aliweza kuanza kuhesabu kwa umakini mkubwa kwamba ni wapi hasa amekosea hakuona kama kuna sehemu yoyote ile alienda vibaya bado alikuwa ana wasi wasi sana moyoni kila alipowaza kuhusu familia yake. Aliiwasha laptop yake ya humo ndani na Kuna namba aliipiga, ilionekana sura ya mwanamke mrembo akiwa karibu na watoto wawili mapacha wakike na wakiume, alitabasamu sana kuwaona watu hao watatu ndio walikuwa kila kitu kwake aliwapenda mno na hakuhitaji wapate matatizo yoyote yale kutokana na kazi zake ndio maana alienda kuwaficha mbali sana kwa siri.

"Mume wangu ni lini tutaanza kuishi maisha ya kawaida? Mimi nimechoka haya maisha kumbuka watoto wanahitaji malezi ya baba na mama kila siku wananisumbua wakitaka uje. Ni miaka kadhaa sasa unatuzungusha tu unadai kuna watu wanakufuatilia kwa usalama wetu tukae mbali hao watu umewakosea nini mpaka wawe na shida na sisi? I'm tired of this" mkewe aliongea kwa uchungu sana mwanaume alikata simu na kuzima laptop yake alijisikia vibaya sana kuona machozi ya mkewe hakuwa na kingine hicho ndicho kilichokuwa kimemleta humo ndani alikuwa akifanya nao mawasiliano kwa siri sana. Alitoka humo ndani na kuvaa suti ya bei, alitoka mpaka nje na kutoka ndani ya nyumba yake hiyo ya TABATA ambayo alikuwa akiitumia kwa mambo yake ya siri na kisha kurudi KIBO.

Safari yake iliienda kuishia NAMANGA karibu na kituo cha polisi cha OSTERBAY, aliliacha gari kwenye mgahawa mmoja akaanza kutembea kwa mguu alienda mpaka kwa mzee mmoja ambaye alikuwa anauza genge la vitu vya nyumbani na kashata, palikuwa panachangamka mno na watu wa mtaa huo walimzoea sana mzee huyo vivyo mida ya jioni kama hiyo walikuwa wanajaa hilo eneo ambapo hata kahawa ilikuwa inapatikana. Mzee huyo baada ya kumuona Qader alimuita kijana mmoja ambaye alimpa maagizo ya kumuacha pale kwenye kile kibanda yeye akaongozana na mwanaume huyo mpaka nyumbani kabisa kwa mzee huyo ambapo hapakuwa mbali kutoka pale na mzee huyo alikuwa anaishi mwenyewe kabisa bila mke ni ajabu kwa umri wake alitakiwa kuwa na mke pamoja na familia au watoto wa kutosha.

"Mhhhhhh vipi kuvamiana bila taarifa" ilikuwa ni sauti ta mzee huyo akiwa amekaa kwenye sofa la bei ghali ndani ya hiyo nyumba ambalo halikuendana kabisa na biashara ambayo alikuwa akiifanya, ndani ya nyumba yake ni watu wachache sana ambao walikuwa wanapata bahati ya kuingia alikuwa akiishi kwa siri sana kwa biashara ya kashata na genge mtaani na wengi walimjua hivyo. Qader hakujibu chochote alijibwaga kwenye sofa akionekana kuchanganyikiwa ni wazi hakuwa sawa, mzee huyo alinyanyuka na kwenda kutoa pombe kali sana kwenye vibati pombe hiyo ni maarufu sana ndani ya nchi ya Mexico pamoja na nchi zenye baridi kali kwa sababu inasadikika huwa ina joto kali sana na ni pombe ghali mno kwa mlala hoi hawezi kabisa kuzipata zaidi ya kuzishuhudia kwa watu wengine tu. Alimrushia moja akiwasha kiyoyozi alijua kinacho enda kutokea hata yeye alijichukulia moja na kuinywa taratibu akiwa anaikunja sura yake, Qader alipiga mafunda kadhaa na kuiweka mezani ilikuwa kali mpaka machozi yalimtoka.

"Hivi mzee ushawahi kukutana na wanadamu ambao ni kama majini?" Qader aliuliza swali ambalo lilimshtua mpaka mzee huyo.

"Una maanisha nini kusema hivyo?"
"Naomba unijibu kwanza"
"Kwa binadamu wa kawaida kuwa jini haiwezekani ila inasemekana majini yapo kutokana na nadharia nyingi za mambo ya ajabu ila kuna wanadamu ambao wanakuwa na uwezo ambao sio kawaida kwa mwanadamu kuwa nao na ndio hao ambao huwa wanaonekana viumbe vya ajabu baadae huwa wanafananishwa na majini" mzee huyo alimjibu Qader akiwa anamwangalia kwa umakini sana.

"Umekaa miaka mingapi kwenye hiyo idara yenu ya usalama wa taifa?" Aliuliza Qader akiwa anaigida tena hiyo pombe.

"Nina zaidi ya miaka 30 ndani ya idara ya usalama wa taifa nayajua mambo mengi sana ambayo binadamu wengi hawayajui, nimedumu na maraisi zaidi ya watatu mpaka sasa tofauti tofauti unahitaji nikusaidie kipi tena mimi nawewe tushamalizana labda kama utaongeza dau"

"Mzee pesa sio shida nipo hapa kwa sababu nilikulipa pesa nyingi sana uweze kunisaidia kupata taarifa za huyu kijana anaye itwa JITI MAALIMU ni kweli nilifanikiwa kumpata na kwenda naye kumhoji lakini bahati mbaya nimekuja kugundua yule mtu siye ambaye nilimdhania, nimekutana na mtu tofauti kabisa ambacho ni kiumbe cha ajabu sana mtu anaweza kuliunga jeraha likapona hapo hapo, anazijua siri nyingi mno mpaka maisha yangu yote, sasa nilitaka nikuulize haya mambo uliyajua mapema ukawa unaniingiza sehemu mbaya au nawewe hujui? Maana sikutaka nifanye kitu kibaya kwako bila kupata uhakika" aliongea kwa msisitizo sana alimwangalia mzee huyu ambaye alikuwa akimsikiliza kwa umakini sana.

"Mhhhhhh tangu nimejiunga ndani ya idara ya usalama wa taifa leo ndo kwa mara ya kwanza nasikia mtu ananitishia maisha yangu ni jambo la kushangaza sana na hili ndilo kosa kubwa ambalo vijana wengi huwa mnalifanya kwenye miaka hii ya leo halafu baadae huwa mnaanza kujutia sana uamuzi wenu. Kwa leo nitakuacha uende tu na hiyo kauli usije ukairudia tena mbele yangu unaweza usiwe na bahati ya kuishi tena" mzee huyo hakuwa na masiara tena na ule ulegevu ambao alikuwa nao ulikuwa umepotea kabisa mbele yake alikuwa imara sana.

"Mzee kwahiyo unanitisha mimi hahahahahhahahahah"
"Mimi sikutishi ila nakwambia ukweli usijisahau sana, kumbuka tulipo kutana siku ya kwanza nilikuwa kwenye misheni nzito ya kuwasaka watu ambao walikuwa wanavusha rasilimali za nchi kimagendo na kuingiza madawa ya kulevya ilitakiwa nikukamatishe siku ile tukaongea kikubwa yakaisha tangu siku ule umekuwa kama kijana wangu na tunafanya kazi pamoja. Uliomba nikusaidie kupata taarifa za huyo bwana mdogo ambaye sijui una kazi gani naye ipi mimi nilirisk kazi yangu nikaziiba taarifa hizo ndani ya idara na kukupatia kwa milioni miambili tu lakini Leo unakuja na kuanza kunipigia kelele hapa, ingekuwa ni vyema sana ungeeleza shida yako ila sio kuanza kunitisha itakuwa mbaya sana kwa upande wako hakuna unacho kijua chochote kuhusu mimi ndio maana kwenye maisha yangu huwa similiki simu" alijibu kistaarabu lakini kwa sauti nzito ambayo hata Qader aliishangaa, haikuwa ya yule babu ambaye alimjua kila siku ilikuwa inasikika sauti ya kiume tena yenye mamlaka makubwa sana.

"Huyo bwana mdogo JITI alishakufa muda mrefu sana na Kuna mwarabu mmoja ambaye anaivaa hiyo sura yake na kujifanya yeye ni huyo kijana hivyo anafanya kazi ndani ya usalama kwa kivuli cha yule mtoto, Jana nilifanikiwa kumteka baadae akaondoka kiwepesi tu baada ya kumjua kwa usahihi kwamba ni kiumbe cha ajabu sana na anajua karibia kila siri ya maisha yangu sikuwa na namna nilimuacha aende, nitakuongeza milioni miamoja ambazo zitaingia kwenye akaunti yako leo jioni naomba taarifa za mtu huyu kwa undani nimjue vizuri" Qader hakuongeza neno aliichukua hiyo pombe na kuinywa yote alitoka machozi yakiwa yanamtoka kwa ukali wa pombe hiyo hakuwajali watu ambao walikuwa wanamshangaa namna alivyokuwa analia, aliingia kwenye gari yake na kuondoka.
Aliingia kwenye makazi yake ya siku zote ambako mara nyingi alikuwa akiishi kwa starehe sana KIBO alifika hapo palikuwa kimya ni walinzi tu walikuwepo getini aliingia ndani na kuiwasha simu yake ambayo kwa muda mrefu sana aliizima aliingia kwenye uwanja wa meseji na kuandika kisha akatuma mahali na kuizima tena simu hiyo. Ndani ya nusu saa waliingia wanaume sita wakiwa na suti zao za bei kali.

"Jiandaeni watatu kati yenu muda huu tunaondoka na kwenda Bukoba huko" Leo alikuwa siriasi sana, saa moja baadae wanaume wanne walikuwa ndani ya AIR TANZANIA wakielekea BUKOBA ambako walifika salama, walichukua usafiri wa noa mpaka ndani ya kijiji cha KIBETA alikuwa analikumbuka jina la mtu ambaye alimfuata ndani ya kijiji hicho lakini hakumjua kabisa na hakuwahi kumuona kwenye maisha yake yote. Aliwaacha vijana wake sehemu wakiwa wanazuga baada ya kufika ndani ya kijiji hicho alinyoosha kwenye restaurant moja nzuri sana.

"Hello samahani naweza kuulizia kwa mzee Philebert?" Mhudumu ambaye alikuwa busy kuandaa chakula aliisikia sauti hiyo, huyo mzee alikuwa tajiri sana hivyo alifahamika sana kwenye hiyo mitaa.

"Zunguka huko nyuma hesabu hatua kumi mkono wako wa kulia utakutana na migomba imepandwa kwa mistali miwili katikati Kuna njia nzuri hivi nyoosha moja mwa moja jumba utakalo liona kwa mbele yako ndipo hapo hapo kwa mzee huyo. Alishukuru sana na kuondoka ulikuwa ni usiku sana tayari kila mtu alikuwa busy na kazi zake hakuna ambaye angewashtukia walijifunga vitambaa usoni na kusogea maeneo hayo palikuwa kimya sana taa za nje tu ndo zilikuwa zinawaka, walizunguka nyuma na kugawana madirisha walichomoa vioo kwa koleo zao ndogo na kutoa kistaarabu wakiwa wamegawana wawili wawili walizama ndani ila ilikuwa ni ajabu sana kwa Qader alishangaa humo ndani kulikuwa na kiza sana ila kioo ambacho walikitoa dirishani kilisaidia kuingiza mwanga kidogo. Mbele ya macho yake alifanikiwa kumuona mwanaume mmoja ambaye ni wazi alikuwa anawasubiri wafike alikuwa amevaa barakoa usoni kwake na nguo nyeusi, walikuwa wameingia cha kike.

Nyumbani kwa mzee Philebert Kuna wenyeji gani tena ambao wameongezeka hawa alio kutana nao Qader na team yake?, Atatoka hapa leo au ndo tunamsahau na hawa ni akina nani?

25 natupa kalamu chini tukutane tena wakati ujao

Langu jina naitwa

Bux the story teller

Chao.
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA SITA

TULIPO ISHIA UKURASA WA ISHIRINI NA TANO

"Zunguka huko nyuma hesabu hatua kumi mkono wako wa kulia utakutana na migomba imepandwa kwa mistali miwili katikati Kuna njia nzuri hivi nyoosha moja mwa moja jumba utakalo liona kwa mbele yako ndipo hapo hapo kwa mzee huyo. Alishukuru sana na kuondoka ulikuwa ni usiku sana tayari kila mtu alikuwa busy na kazi zake hakuna ambaye angewashtukia walijifunga vitambaa usoni na kusogea maeneo hayo palikuwa kimya sana taa za nje tu ndo zilikuwa zinawaka, walizunguka nyuma na kugawana madirisha walichomoa vioo kwa koleo zao ndogo na kutoa kistaarabu wakiwa wamegawana wawili wawili walizama ndani ila ilikuwa ni ajabu sana kwa Qader alishangaa humo ndani kulikuwa na kiza sana ila kioo ambacho walikitoa dirishani kilisaidia kuingiza mwanga kidogo. Mbele ya macho yake alifanikiwa kumuona mwanaume mmoja ambaye ni wazi alikuwa anawasubiri wafike alikuwa amevaa barakoa usoni kwake na nguo nyeusi, walikuwa wameingia cha kike

ENDELEA.....................

"Wewe ndiye mlinzi wa hii familia? haya nambie kabla sijakufanya kitu kibaya hawa watu wako wapi?" Qader alikuwa mtu wa kujiamini kupita maelezo alikuwa anauliza kwa majigambo kwa sababu alikuwa anajiamini sana linapokuja suala la mapigano, mwanaume ambaye alikuwa mbele yao hakujibu chochote alibaki anawatazama tu akawasogelea kidogo na barakoa yake.

"Unaweza ukanipa sababu ya msingi ya kuvunja na kuingia kwenye nyumba ya mtu bila ruhusa yake halafu unauliza kwa jeuri kama vile upo kwako vipi ulikotoka hakuna wakubwa ambao wamekufundisha namna ya kuishi pale unapokuwa ndani ya miji ya watu?" Ni sautu nzito mno ilipenya kwenye masikio ya Qader alishangaa mtu huyo anajiaminia nini

"Mko wangapi humu ndani?" Lilikuwa swali la kijinga sana kutoka kwa Qader lilimfanya mwanaume huyo atikise kichwa kuonyesha masikitiko.

"Kwenye maisha yako kama unaona kuna jambo huliwezi uwe unakaa pembeni wewe bado ni muoga sana sidhani kama maeneo kama haya yanakufaa kabisa, hii familia unayo itafuta wewe hautakuja kuipata maisha yako yote na nilikuwa nakusubiri hapa ili nijue ni nani huyu anayekuja bila wasiwasi sasa kwa muda huu nahitaji uniambie unatafuta nini kwenye familia hii mpaka uvamie usiku wote huu?" Mwanaume huyo aliuliza akiwa amewasogelea Qader na mwenzake walikuwa wapo karibu. Qader alichukulia kama dharau alijigeuza kwa double kick moja kali sana ambayo mtu huyo aliikwepa kidogo tu ikapita na hewa bila kumgusa.

"Wewe bado ni mzito sana ningekuwa mimi ndo nimerusha hayo mateke mpaka muda huu ungekuwa hauna uwezo wa kutembea ebu tusipotezeane muda nambie kilicho kuleta hapa na kakutuma nani naweza kuwapa nafasi ya kuwaacha hai tena" ilionekana kama masiara ila alikuwa serious sana mwanaume huyu wakati anazitamka hizo herufi zake mbele ya wanaume wenzake wawili. Kijana wa Qader alisogea na kujirusha kwa kasi alipigwa ngumi moja ya mbavu ambazo zilisikika kabisa wakati zinavunjika ajirushwa mbali mpaka kwenye kioo ambacho kiliwastua ambao walikuwa chumba kingine walikuja kwa spidi kali wakati wanaingia ghafla sana umeme uliwaka mwanaume aliyekuwa mbele yao alikuwa na switch ndogo mkononi.
Wote walishangaa imekuwaje hata Qader hakuamini alicho kiona kijana wake mmoja alikuwa chini hakuwa hata na uwezo wa kunyanyuka alipo angukia mwanaume huyo kwa hatua za taratibu kabisa alitembea kuelekea pale alipo dondokea yule kijana aliinama bila hofu.

"Inaniuma sana kuua kiumbe dhaifu na kijana mdogo kama wewe hapo ila sina namna" alimaliza kuongea na kuizungusha shingo ya huyo bwana mdogo iligeuka kabisa akiwa bado amefumbua macho wenzake walifumba macho lilikuwa ni tukio ka kutisha na kusisimua sana.

"Who are you?" Qader aliuliza kwa hasira aliona mwanaume huyo anatoa barakoa yake usoni alikuwa ni mtu wa miaka inayo elekea 37 hivi sura ngumu iliyo komaa sana.

"Bwana mdogo hii nchi ina wahusika wake huwezi kufanya kila ambacho unajisikia wewe ebu niambie sasa unamtafuta nani hapa na kipi kimekuleta" Qader baada ya kusikia swali hilo kwa hasira alivua kitambaa chake na kubakia na sura tupu na kuchomoa kisu chake mwanaume huyo mbele yake alitabasamu sana, Qader alijirusha mateke mfululizo na kuikunjua ngumi yake ya mkono wa kulia ambayo ilimpata mtu huyo usoni alipepesuka kidogo na kusimama vizuri aliikunja mikono yake yote miwili, Qader anavyo jiandaa kushambulia kwa kisu alihisi kama mkono wake wa kushoto haufanyi kazi vizuri alipigwa teke ambalo hakutarajia litamfikia mwanaume huyo alirusha ngumi mfululizo ambazo zilimpata Qader kifuani alitoa damu ya kutosha na kudondokea mbali. Vijana wake wawili walikuja kwa pamoja mmoja wao alidakwa mguu wake ambao ulirushwa ulivunjwa alimaliziwa ngumi ya koromeo na mtu huyo akawa amekufa akiwa bado amesimama.

Wapili alianza kuogopa akawa anajishauri akimbie au abaki Qader alisimama akiwa bado ana maumivu mazito sana alirusha sindano kutoka kwenye mfuko wake zaidi ya sita, mwanaume huyo alizizuia kwa mkono wake ambao ulikuwa na guard(kizuio) hivyo hazikumfika mwilini, alitoa mkono wake usoni alikuja kushangaa hamuoni Qader, aliangalia dirishani akaona kuna kioo kinatikisika akajua mtu huyo kapitia hapo kukimbia aliwahi na kuchungulia dirishani hakuona kitu chochote kile. Aliyarudisha macho yake nyuma baada ya kukumbuka kuna kijana mmoja alibaki cha ajabu naye alikuwa chini akitapa tapa, alimkimbilia pale alishangaa anatoa povu mdomoni baada ya kumuangalia shingoni alikutana na sindano akagundua mtu huyo aliamua kumuua ili asiupate ushahidi wowote ule ndio maana yeye aliamua kukimbia, mwanaume alichukia sana alipiga ngumi chini kwa hasira.

Aliingiza mkono kwenye mfuko wake akatoa simu na kupiga mahali
"Mheshimiwa ni kweli kama ulivyosema kuna vijana wamefika hapa walikuwa wanamhitaji huyu mzee na familia yake, bahati mbaya sana watatu wamekufa ila mmoja kanikimbia na anaonekana ndo anaujua ukweli na ni nani aliye mtuma hapa ila usijali nimeiona sura yake nitamtafuta nina imani sio muda sana nitampata" aliongea kwa msisitizo sana na kwa heshima kubwa.
"Sawa mkuu" simu ikakatwa naye akaondoka humo ndani.

Hali ya Qader ilikuwa mbaya alipigwa ngumi mbaya sana kwenye maeneo ya kifua chake alikuwa anatokwa na damu sana mdomoni alihisi kifua kinambana sana na kila muda ulivyokuwa unazidi kwenda alihisi kama kifua kinawaka moto, alikuwa ameishika njia ambayo walikuja nayo wakati walipokuwa kwenye noah hakuona usafiri wowote ule ilikuwa ni usiku wa manane sana, aliwaza sana yule mwanaume imara sana kiasi kile ni nani? hakuwahi kumuona hata siku moja, na pale alikuwa anatafuta nini? Je alijua kama wanakuja? Na alijuaje?, Kumbukumbu zake ni kwamba wakati anaondoka Dar aliwashtukiza tu vijana wake na hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa anajua kuhusu hilo jambo haya mambo yaliyo tokea yalimfanya aanze kuyakumbuka kwa usahihi maneno ya Jiti Maalimu alikuwa kwenye hatari kubwa sana.

Alitembea sana ilifika sehemu alichoka mno hakuwa na msaada wowote ule alijikaza sana lakini inapofikia hatua hakuna namna ya kuishi tena basi kila kitu huwa hakina msaada ilifika hatua akaamua kukata tamaa kitu ambacho huwa ni cha mwisho kabisa kwenye maisha ya mwabadamu yeyote yule ambaye yupo hai kukata tamaa maana yake umekubali kufa mwanaume alipiga magoti katikati ya barabara hakuwa na uwezo hata wa kusogeza hatua yake moja mbele kifua kilikuwa kinawaka moto, damu ilikuwa inamtoka kwa wingi mdomoni macho yalianza kupoteza nuru yake, akiwa kwenye sekunde zake za mwisho kukata tamaa kwa mbali aliona kuna gari inatokea kule ambako alitokea yeye ilikuwa kwenye kasi kubwa mno hakuwa na imani kama haitamgonga kwa kasi iliyokuwa nayo ila moyoni alisali sana na kuomba ni bora afe lakini sio kuingia kwenye mikono ya yule mwanaume ambaye ametoka kumkimbia kule kwenye nyumba ya mzee Philebert.

Gari ilienda kusimama sentimita chache sana kutoka pale alipokuwa yeye, alikuwa amelala chini kabisa alikuwa akiona kwa mbali sana macho yalizidi kumsaliti, aliona kuna mwanaume anashuka ndani ya gari akiwa kwenye nguo ambazo alihisi ni suti, mtu huyo alienda kuchuchumaa karibu na yeye alipo akiwa anamwangalia, alijaribu sana kujitajidi ili amjue mtu huyo bahati mbaya alikuwa anaona ukungu tu mbele yake hatimaye alipoteza kabisa uwezo wa kuona na hakuelewa kilicho endelea baada ya hapo.

Sauti ya kawaida tu ya televisheni na mziki wa wastani ndivyo vilivyokuwa vinasikika kwenye ngoma za masikio yake, aliyafumbua macho yake na kuangaza huku na huku chumba kilikuwa chenye nuru ya kutosha, kilikuwa ni chumba cha gharama sana ilimpa picha kwamba alikuwa kwenye moja ya majumba ya kifahari sana. Hakuna ambacho kilikuja kichwani mwake kwa wakati huo zaidi ya maumivu ambayo aliyahisi kifuani kwake ambayo hayakuwa makubwa wakati anahitaji kunyanyuka ilimlazimu alale tena ili angalau atafute nguvu za kunyanyuka.

"Nilikuonya mapema sana , kwenye maisha yako kosa kila kitu ila usikose akili utakuwa mtu wa hovyo sana na unaweza kuishia sehemu mbaya mno, hivi wewe haujiulizi kwanini mimi najua mambo mengi lakini huwa sikurupuki kufanya maamuzi ya hovyo kama yako? Vipi jana kama nisingekuwepo kule si ungekufa wewe" ni sauti ambayo haikuwa ngeni kabisa kwenye masikio ya Qader aliikumbuka vizuri sana, sauti ya Jiti Maalimu isingeweza kumtoka kirahisi sana namna hiyo mwanaume huyo alikuwa amekaa kwenye sofa anaangalia televisheni nyuma kidogo ya kitanda ambacho alilala Qader.

"Nina muda gani hapa?"
"Siku mbili tu"
"Whaaat?"
"Hapo unacho shangaa nini?" Hiyo kauli ndiyo iliyo mfanya Qader atulize akili na kuweza kukumbuka matukio ambayo yalitokea mpaka mara ya mwisho anadondoka barabarani na kupoteza fahamu ambapo alimshuhudia mtu mmoja akiwa na suti akija kuchuchumaa mbele yake hakuelewa kilicho endelea tena.

"Kwamba wewe ndiye ambaye ulikuja kinisaidia pale?" Aliuliza kwa mshangao akiwa amejishika kifuani akijikaza mpaka akanyanyuka kitandani bado kifua kilikuwa na maumivu, alisogea mpaka pale alipokuwa amekaa Jiti akakaa Kochi la pembeni yake wakati huo Jiti alimrushia kidonge kimoja kikubwa kiasi Qader akakiweka mdomoni na kukimeza dakika moja tu alihisi kifua hakina maumivu yoyoye alikuwa sawa kabisa Jiti hakuwa na muda wa kumwangalia alikuwa ameweka katuni ambazo alipenda sana kuangalia akiwa ametulia.

"Usije ukaruhusu tena huyo mtu akakupiga ngumi za aina hiyo zaidi ya tatu kwenye kifua chako kutakuwa na mawili kama sio kufa basi utalala kitandani maisha yako yote alikupiga ngumi mbaya sana na una bahati nilitokea mapema na kuondoka nawewe ungekuwa umekufa saivi tangu mwanzo nilikwambia wewe bado ni dhaifu sana kuna mambo huna uwezo nao sasa hapo hapo ndo unamtafuta Zakaria haupo siriasi" maneno ya Jiti yalimfanya Qader ameze mate alikuwa anaambiwa ukweli alikuwa mtu wa kukurupuka sana.

"Iliwezekana vipi wewe kujua kwamba mimi nipo kule na ukaja kinisaidia wakati niliondoka kwa siri sana Dar es salaam?"

"Jiangalie kwenye bega lako la kulia" Jiti aliniangalia kwa umakini na kuikuta doti nyeusi
"Hii ni nini?"
"Siku ile wakati natoka kwako nilikuwekea hicho ni kifa cha mawasiliano ambacho kinakuwa kama kidoti ila hiyo ni chip maalumu, siku ile baada ya kukupa taarifa ya uwepo wa ndugu wa Zakaria BUKOBA kwa akili yako nilijua utaenda tu ndio maana niliweka hicho kifaa nione kama ni kweli utafanya hivyo kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kukuona popote pale ulipo na kusikia kila ulichokuwa unakiongea, tangu mnapanda kwenye ndege hata mimi nilikuwepo mle, mnachukua Noah kwenda kwenye kile kijini mimi nilikuwa kwenye gari ya nyuma ambayo niliichukua mjini baada ya kumuua mmiliki wake ili nirahisishe safari na kama tahadhari kama kuna tukio baya litatokea mbeleni.

Hivyo kila ambacho mlikuwa mnakifanya nilikuwa nakiona na kukijua, ulivyo fanikiwa kutoka kwenye ile nyumba nilijua lazima tu utaanza kuhangaika kupata usafiri ndio maana niliamua kwenda kuchukua gari na kuanza kuifuata barabara haukuwa na sehemu ya kukimbilia ndio maana nilikuwa na uhakika wa kukupata mpaka pale nilipofika na kukubeba na kuondoka" mwanaume aliongea huku akiwa anaangalia zake televisheni hakuwa hata na muda na Qader, Qader alijifuta jasho usoni hizo hadithi zilikuwa zinamtisha sana huyo mtu mbele yake alikuwa makini sana kwa kila anacho kifanya tofauti na yeye alivyokuwa anayafanya mambo kwa kukurupuka.

"Sasa kama wewe ulikuwepo kule kwanini hukuweza kujitokeza mbele ya yule mtu ukanisaidia tukammaliza na yule mtu ni nani?"

"Huwa sijishugulishi na kazi ambazo hazinihusu hata hivi inabidi ushukuru tu mimi kupoteza muda wangu kukuokoa"

"Una maanisha nini?"
"Leo nataka unijue sasa uhalisia wangu mimi ni nani na kwanini naifanya hii kazi na sababu inayo nifanya nimtafute Zakaria kwa gharama yoyote ile" aliweka kituo akaichukua limoti na kuzima kabisa televisheni akimgeukia Qader akiwa anamtazama kwa makini sana, Qader hicho ndicho alichokuwa anatamani sana kukijua, kuna mengi sana alihitaji kuyajua kutoka kwa huyu mtu leo hii aliitamani sana hiyo nafasi hatimaye ilikuwa imefika.

Nini Siri nzito anaishi nayo Jiti Maalimu kwenye kifua chake ambayo leo lazima Qadee aijue na Qader abahusikaje na hiyo siri mpaka mtu huyu ajitoe kwenda kumuokoa?.

26 leo nasema basi mpaka wakati ujao tena.

Langu jina naitwa

Bux the story teller
Chao.
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672

Wakuu tusameheane sana kwa sababu kuna muda inachelewa kidogo tunajaribu kutafuta tafuta mishe za kuliweka sawa tumbo kwanza, sasa hizo mishe zisipo enda sawa hata nguvu ya kuingia ingia mitandaoni huwezi kuipata stress zinasumbua kichwa. Leo tunasoma kurasa mbili ya kwanza naileta muda huu ila hadithi ipo mpaka mwisho ambapo kurasa ya mwisho kabisa ni ukurasa wa 115.
 
UKURASA WA ISHIRINI NA SABA

TULIPO ISHIA UKURASA WA ISHIRINI NA SITA
"Leo nataka unijue sasa uhalisia wangu mimi ni nani na kwanini naifanya hii kazi na sababu inayo nifanya nimtafute Zakaria kwa gharama yoyote ile" aliweka kituo akaichukua limoti na kuzima kabisa televisheni akimgeukia Qader akiwa anamtazama kwa makini sana, Qader hicho ndicho alichokuwa anatamani sana kukijua, kuna mengi sana alihitaji kuyajua kutoka kwa huyu mtu leo hii aliitamani sana hiyo nafasi hatimaye ilikuwa imefika.

ENDELEA......................
CASA LAPANO VITAE HOTEL
Ni miongoni mwa hoteli maarufu sana na ya kifahari mno ndani ya jiji la BENGHAZI ambayo ilikuwa upande wa kulia wa mtaa ujulikanao kama LAPANO STREET NCDB TOWN, ilikuwa imejengwa kwa namna ya kipekee sana kila mtu angetamani kujumuika na kuwa mmoja ya watu ambao walipata bahati ya kupata japo hata usiku mmoja tu wa kuweza kulala humo ndani, hoteli yenye ghorofa zaidi ya 80 na mabwawa ya kuogolea zaidi ya manne ambapo moja lilikuwa katikati ya ghorofa ya 40 na lingine likiwa juu kabisa ya ghorofa namba 80 mandhari ilikuwa ya kuvutia sana kwenye hiyo hoteli iliwafanya watu ambao walikuwa humo ndani na karibu na eneo hilo kuyaburudisha macho yao.
Hiyo ndiyo hoteli ambayo alikuwa amepelekwa Mr Josephat tajiri huyu kutoka Afrika ya kusini kama yeye alivyoweza kujitambulisha, chumba chake kilikuwa ni namba 008 hakikuwa mbali sana na chini, ni muda mfupi tu tangu aingie humo ndani alishangazwa na maandalizi makubwa ambayo yalikuwa yamefanyila alitabasamu tu hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Alitazama kwa umakini sana kila pembe na kila eneo ambalo alihisi humo ndani lingekuwa na ukakasi kwake, baada ya macho yake kuzunguka sana kwenye pazia kubwa la dirishani kulikuwa na kifungo kidogo sana cha shati ilikuwa ni ngumu kukiona, hiyo ilikuwa ni kamera ambayo ilikuwa inaonyesha kila kitu , mwanaume alisogea hapo na kulikunja pazia hilo kwa namna ambayo ilionyesha kwamba hajui chochote hakuhitaji kushtukiwa kabisa maana alijua anaonekana, alienda nalo mpaka bafuni na kuliloweka kwenye maji kisha akakitoa kifungo hicho na kukigeuzia kwenye pipa la takataka humo chooni.

Aliitoa laptop yake na kuanza kuangaza angaza kwenye ile ofisi kubwa ya MBAYE TRANSPORTATION aliacha kamera zake maeneo mengi sana
"Kama ningeambiwa nimuue nadhani ningemaliza kazi mapema sana ila mambo ya kuanza kumchimba mtu ni hatua kubwa mno ambazo zinahitajika kuchukuliwa na inaweza kuchukua muda mrefu kuweza kulikamilisha zoezi hili" alijiongelesha huku akifunika laptop yake na kwenda kujibwaga kwenye sofa.

Saa nane kasoro usiku mr Josephat aliamka akajinyoosha aliangalia saa yake mkononi muda ulikuwa umeenda sana alitoka mpaka sebuleni aliikumbuka vizuri kwamba alizima taa za umeme wakati anaenda kulala, aliwasha taa zote na kwenda kufungua mlango akauacha wazi na kuingia ndani tena aliingia chumbani hakutoka tena, kabla ya kufungua huo mlango alisikia hatua za watu wakiwa wanasogelea mlango huo ndio maana alienda kuufungua na kutoka. Ni kweli kwa nje palikuwa na kiza sana taa zote zilikuwa zimezimwa kuna wanaume watano walikuwa wana silaha mikononi walikuwa wananyata kuelekea ulipo huo mlango baada ya kuona mlango umefunguliwa ghafla walijibanza kuona kama kuna mtu atatokezea baada ya kupita kimya cha muda mrefu waliamua kuingia ndani hawakuona mtu sebuleni walienda mpaka chumbani walitafuta kila sehemu hawakuona mtu.

Mmoja wakati anageuka aliona dirisha la chumbani liko wazi akasogea mpaka pale dirishani kwa chini aliona kuna mtu anajifuta futa akiwa ana mashaka sana.

"Hakuna chochote humu mzigo haupo mtu wetu yupo chini kabisa kule nimemuona tumuwahi atatupatia mwenyewe" baada ya kauli hiyo waliondoka kwa kasi humo ndani kuweza kuwahi chini kumpata mtu huyo ambaye alikuwa na zaidi ya billion za kitanzania 30 mkononi mwake ulikuwa ni utajiri ulio jitosheleza kabisa. Waliwahi lile eneo waliona kuna mtu anaishia kwenye kona basi iliwalazimu kumfuata kwa kasi sana, mbele yao kulikuwa na njia mbili ziliachana palikuwa na uwanja mkubwa tu eneo hilo ambao hata magari mawili yangepishana bila tatizo lolote. Mmoja wao alienda chini shingo ilitobolewa kati kati na muuaji hakuonekana walipagawa wakaanza kuzunguka huku na huku, wakiwa wamesimama hapo wanatafuta muuaji wa mwenzao yuko wapi kwa sababu hawakuwa na imani kama ndo yule ambaye walimkosa kwenye ile hoteli.

"Nakufaaaaaaaaa(mmoja aliongea kwa kiarabu) baada ya mkono wake kwenda chini na upanga mmoja ambao ulitokea kwenye kona moja ya duka ulitokea palikuwa na kiza sana na mrushaji hakuonekana kabisa, waligeuka na kupiga ile sehemu risasi za kutosha ni sauti ambayo iliwashtua hata wakazi wa hilo eneo lakini hakuna hata mmoja ambaye alithubutu kutoka wala kukohoa ilibidi waokoe maisha yao huko huko waliko lala wakiendelea kusali. Walisitisha zoezi la kupiga risasi baada ya kuona bado palikuwa kimya tu, mmoja akisogea mpaka kwenye ile kona alitamka tu herufi moja.
"Ru..." Nadhani alihitaji kuwaambia wenzake kwamba run ila hakuimalizia ngumi yenye kilo nzito ilitua kwenye shingo yake shingo ilivunjwa vibaya mpaka ikapinda silaha aliyokuwa nayo mkononi ilitua kwenye mkono wa mwanaume huyo ambaye alitokeza hadharani, wanaume waliokuwa wamesimama walikuwa wamebaki wawili tu, waliona mwili wa mwenzao ukirudishwa juu juu waliupiga risasi nyingi sana wote walidondona chini risasi zilipasua vichwa vyao walikuwa busy kushambulia mwili wa mwenzao aliyekuwa amerushwa wakamsahau adui. Alitokeza Mr Josephat mwenyewe akiwa na kofia kichwani aliuokota upanga wake na kwenda kuchuchumaa mbele ya yule ambaye alikuwa amekatwa mkono wake, alimwangalia alikuwa ni kijana mdogo bado.

"Una miaka mingapi?" Alikuwa anaongea kiarabu chenyewe kabisa kwa sababu alijua hao ndiyo lugha ambayo walikuwa wanaijua.
"21"
"Kwanini kijana mdogo kama wewe unajiingiza kwenye kazi za hatari namna hii?"
"Shida ya pesa ndo maana nafanya haya yote"
"Una tatizo gani?"
"Naishi na bibi yangu ana kansa ya koo walisema ili atibiwe inabidi niwe na milioni hamsini ndiyo maana huwa naingia hadi kwenye kazi kama hizi ili kupata walau chochote kitu nikamsaidie bibi yangu" yale maneno yalimfanya Mr Josephat akae chini upanga ulimdondoka, aliishiwa nguvu machozi yalianza kumtoka taratibu kwenye macho yake alijutia alichokuwa amekifanya kwa huyo bwana mdogo, alikuwa ameukata nusu ya mkono wake ulikuwa chini lakini kumbe bwana mdogo huyo alikuwa anayafanya hayo yote ili tu kuinusuru nafsi ya bibi yake ilikuwa ni mara ya kwanza yeye kutoa machozi hadharani kwani kilikuwa ni kiumbe kigumu mno mpaka huyo kijana alibaki anamshangaa mwanaume huyo ambaye alikuwa katili sana mbele yake, hakuelewa kwanini analia, kiuhalisia Mr Josephat hakuwahi kuishi kwenye malezi ya familia ila alikuwa anaelewa umuhimu wa familia alijua huyo kijana ni lazima bibi yake ndiye aliyekuwa kila kitu kwenye maisha yake.

Aliingiza mkono kwenye mfuko wake akatoa kidonge alimwambia kijana huyo akimeze alifanya hivyo maumivu yote yalikata japo mkono ndio ilikuwa basi tena alihitaji kijana huyo amuelekeze kwao ni wapi ili amepeleke alimbeba mgongoni akachukua upanga wake na mkono alio ukata wa huyo kijana waliongoza njia, kwa maelezo ya huyo bwana mdogo walitumia dakika arobaini tu kwenye mitaa ya uswahilini(slums) huko ndiko yalikokuwa makazi ya huyo bwanamdogo, alimwelekeza mlango aliugusa tu ukafunguka yalikuwa ni maisha mabaya sana ambayo alikuwa anayaishi kijana huyo. Kwenye kitanda kimoja kikuu kuu cha zamani sana ulikuwa umepumzika mwili wa mwanamke mmoja mzee sana ambaye alikuwa kwenye hali mbaya mno alimkalisha kijana huyo kwenye kiti na kukisogeza kiti hicho pale kitandani.

Kuna hadithi huwa ni rahisi sana kuzisimulia kiwepesi ila ni ngumu sana kuzishuhudia bibi huyo alikuwa macho japo humo ndani kulikuwa na kibatari tu ila kiliwezesha kuona kila kilichokuwa kinaendelea, alimshuhudia mjukuu wake akikalishwa kwenye kiti huku akiwa hana mkono mmoja, mwanamke huyo mzee machozi yalianza kumtoka kwenye uso wake hakujua ni kipi kilimpata mjukuu wake ambaye alikuwa ni kila kitu kwake alimpenda sana ila bahati mbaya alikuwa na kansa ya koo hakuwa na uwezo wa kuongea aliishia kutoa machozi tu kwenye uso wake .Mr Josephat hali aliyo iona alipiga magoti mbele ya mwanamke huyo alilia sana mwanaume kuona mwanamke huyo mzee alikuwa anatoa machozi yote ni kwa sababu yake baada ya kumkata mjukuu wake mkono, machozi ya huyo mwanamke yalimuumiza sana ni mbaya sana kwenye maisha kumliza mtu mzima kama huyo kwa tamaa za ujana wako au maslahi yako lazima kuna siku hayo machozi utayalipa tu kwa namna moja ama nyingine.

Aliomba sana msamaha lakini hakuna kilicho saidika bibi huyo alifumba macho yake akiwa bado anatoa machozi ni wazi hakuhitaji kumuona mjukuu wake kwenye hiyo hali ya kutisha ambayo alikuwa nayo huenda alikata tamaa hakuwa na mtu mwingine wa kumtunza. Mr Josephat alimgeukia kijana huyo amabye alikuwa kwenye kiti akiwa anautazama mkono wake kwa huzuni japo kwa huo muda kutokana na kidonge alichokuwa amekimeza hakuwa akihisi maumivu yoyote yale.
"Unaitwa nani jina lako?" Mwanaume alimuuliza kijana huyo kistaarabu sana.
"Aaban Farukh"
"Unamjua daktari yeyote mkubwa kwenye hili jiji?"
"Ndiyo, daktari bingwa wa mji huu ndiye tuliye muona alisema mpaka tuwe na pesa mkononi ndo atatusikiliza hivyo alinipa namba tu kwamba nikikamilisha pesa nimpigie"
"Namba yake iko wapi?"
"Hii hapa" Aaban aliitoa namba hiyo kwenye mfuko wake
"Kwanini unatembea na hiyo namba mfukoni?"
"Kila ninapo iangalia huwa inanikumbusha hali ya bibi kwahiyo huwa napata nguvu mpya ya kupambana" maneno hayo yalimchoma sana Mr Josephat hakuongeza neno alizikopi namba hizo kwenye simu yake na kupiga, simu iliita kwa dakika kadhaa ikapokelewa.
"Hello dokta"
"Yes naongea na nani"
"Ndugu yake Aaban nadhani una taarifa kuhusu ugonjwa wa bibi"
"Nataka pesa sio maneno"
"Unataka shilingi ngapi?"
"Milioni hamsini ndo nitamfanyia oparesheni ya hilo tatizo lake"
"Nakupa milioni miamoja njoo haraka muda huu na gari la wagonjwa pia kuna mgonjwa mwingine ameongezeka anahitaji mkono wa bandia kuwekewa jumla nayeye nitakupa milioni miamoja na hamsini mkononi ila hakikisha wanapata tiba ya kueleweka"
"Are you serious?" Pesa ni dawa ya matatizo dokta hakuwa anaamini kama anapewa pesa yote hiyo.
"Wahi haraka uchukue pesa yako ila hakikisha wagonjwa wangu wanatibiwa vizuri kama ukienda nje na makubaliano basi tusije tukalaumiana baadae"
"Sawa nakuja muda huu kuwachukua" siku ilikatwa, Aaban alikuwa bado haamini mpaka muda huo hakujua kabisa huyo mtu ni nani alimshangaa tu kwanini alikuwa analia baada ya kujua kuhusu bibi yake?, Hakujua hizo pesa zote huyo mtu angezitoa wapi maana kwa jinsi alivyokuwa usiku huo hakufanania na pesa ambazo alikuwa anazitaja, na hata hakujua kama kwenye ile kazi walitumwa kuiba mabilioni ya fedha hiyo siri alikuwa nayo mtu mmoja tu miongoni mwa wale watano.
"Shika hii kadi ya benki(akimtajia namba za siri) ina shilingi milioni mianane ikitokea hatutaonana tena basi tengeneza maisha mazuri kwa ajili yako na bibi, na kuna hii milioni 50 zitakuwa ni za matumizi mpaka pale bibi atakapo kuwa Sawa nawewe mkono wako ukiungwa, za huyu daktari pesa zake hizi hapa utamuonyesha zakwako ziweke sehemu salama" mwanaume alitoa maburungutu ya fedha na kuyaweka kitandani alipokuwa amelala bibi huyo kitu kilicho mfanya mpaka huyo bibi afumbue macho yake alikuwa anatajiwa namna ambazo miaka ya zamani aliwahi kusikia wakiziandika magazetini kuhusu pesa ambazo walikuwa nazo matajiri, alibubujikwa na machozi mwanaume ambaye aliona ameharibu maisha yake kwa kumkata mjukuu wake mkono aligeuka malaika ghafla na kuacha zaidi ya bilioni moja kasoro ndani ya kijumba chao kibobu, Mr Josephat alimbusu bibi huyo na kuanza kutoka hakutaka mtu yeyote ajue uwepo wake humo ndani alitamani sana kumuuliza huyo bwana mdogo kama angekuwa na taarifa za mtu aliyewatuma hakuona umuhimu akaamua kuacha nayo kabisa.

"Wewe ni nani na kwanini unatusaidia" ni kauli ambayo Mr Josephat aliisikia akiwa anakaribia kwenye mlango mbovu uliokuwepo hapo, alisimama na kugeuka.
"Maisha yangu yote sijawahi kulelewa na familia yangu nimeishi nikiwa mwenyewe kwa asilimia zote najua shida yake inavyokuwa kwahiyo huwa sipendi kuona mtu mwingine anayaishi maisha kama yangu, ilitakiwa nikuue kwa sababu mtu aliye watuma kwangu alitaka kunitapeli shilingi zaidi ya bilioni 30 ila nimeamua kukuacha baada ya kujua sababu ambayo imekufanya uwepo pale kwamba unahitaji kuokoa maisha bibi yako. Usije ukarudia tena kufanya tukio kama lile kwenye maisha yako yote wewe bado ni mdogo sana mtunze bibi yako. Jina langu naitwa Zakaria" mwanaume hakusubiri swali lingine alitoka ndani na kupotea baada ya kusikia mlio wa ambulance alielewa kwamba mtu ambaye amempigia simu muda mchache uliopita alikuwa amefika kumchukua mgonjwa wake ambaye kwa mara ya kwanza aliwakataa kwa sababu hawakuwa na pesa leo alitajiwa pesa ndefu aliwafuata yeye mwenyewe sehemu ambayo mara ya kwanza aliondoka bila kutoa huduma.

Nini kinaendelea kujiri? Kwa mara ya kwanza hili dubwana linalia kwa uchungu....ngoja tuzidi kumfahamu mwanaume huyu ambaye mpaka muda huu mzee mmoja aliyekuwa anaonekana kuwa kichaa anampa mheshimiwa raisi wa Libya historia ya maisha ya huyo binadamu ambaye aliambiwa hamjui kwa chochote kile.

27 sina la ziada tukutane wakati ujao

Langu jina naitwa

Bux the story teller

Chao
 
Back
Top Bottom