Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

Tuendelee mkuu. Haaah...! Kumbe hata mwanzo sijaanza. Vipi mliosoma ni tamu wakuu?
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA SABA

ULIPO ISHIA UKURASA WA THELATHINI NA SITA

Aliichukua simu yake na kupiga kwenye namba hiyo simu ilikatwa, alipiga tena simu ilikatwa uliingia ujumbe kwenye simu yake kwamba aende sehemu ambapo ilipandwa miti ya kupumzikia karibu na bustanini mtu huyo amkute amevua nguo zote amelala hapo alikuwa ana hamu naye sana ya kufanya mapenzi, aliishiwa nguvu Aasia hakujua kwanini kijana huyo alikuwa anaidhulumu sana nafsi yake namna hiyo, alijikusanya na kuanza kukimbilia eneo alilokuwa ameagizwa ili akalimalize hilo suala aliogopa kama picha hizo zitasambazwa atakuwa kwenye hali mbaya sana pia anaweza kuidhalilisha mno familia yake ambayo watu wengi hawakujua kabisa anatoka kwenye familia gani. Haya yote yalikuwa yanatokea ndani ya Dubai kwenye moja ya vyuo vikubwa sana kwenye mji huo kinacho julikana kama ZAYED UNIVERSITY.

ENDELEA.................


HAZWA GEREZANI

“Hizi nyembe unatakiwa ujue namna ya kuzitumia kwa asilimia miamoja zitakusaidia sana” Maelezo hayo yalifuatiwa na mzee huyo kutoka kwa spidi sana kuelekea sehemu ambayo alikuwepo Zakaria kumshambulia alijua ni masiara alishtuka anapata maumivu makali sana baada ya nyembe kuzama kwenye mwili wake. Alijua hicho kitu kilikuwa ni siriasi sana alitakiwa kujihami, yalitumika masaa mawili kuweza kumkabidhi rasmi silaha hizo ambazo alitakiwa kuwa nazo sehemu yoyote ile ambayo alikuwa anaenda kwenye maisha yake, masaa mawili yalimtosha sana kuzijua vyema nyembe hizo na namna ya kuzitumia kwa usahihi sana.

“Hii zawadi ya hatari sana namna hii umeitoa wapi maana miaka yote hiyo sijawahi kukuona nayo kabisa”
“Huu ni urithi kutoka kwa babu yangu na haina umuhimu wowote ule wa wewe kujua hilo pokea tu kama kitu cha thamani sana kwenye maisha yako
“Kwanini umeamua kunipa mimi?”
“Umeishi namimi kwa muda mrefu sana kama alikuwepo ambaye angestahili basi nadhani umenielewa vizuri”
“Sawa mzee nashukuru snaa sasa unaweza kunipa historia yangu pamoja na kuniambia ni wapi alipo mke wangu na mwanangu?”

“Jina lako kabisa unaitwa Zakaria Mansour Omran mjukuu wa Mansour the seniour, miongoni mwa watu matajiri sana kwenye nchi yetu huyo ndiye chimbuko la familia yako. Wewe ulipotea kwa baba yako ndipo utata ulipo anzia na familia yako kuuawa yote na ukabaki pekeyako kwa kazi hii…………..” yalipita masaa Matatu mengine wakiwa wamesimama hapo Zakaria akiwa anasimuliwa historia yake yote ya maisha yake, alikaa chini miguu yake haikuwa na nguvu za kuendelea kusimama baada ya kuambiwa kila kitu kumhusu yeye, leo alikuwa amejijua yeye ni nani na familia yake ilikuwa wapi alikuwa na bahati mbaya sana licha ya kujua hilo lakini familia yake bado haikuwa ipo duniani ilimuuma sana mwanaume alilia mno kama vile ni mtoto mdogo.

“Hili jambo umelijua tangu lini?”
“Tangu ukiwa bado mtoto mdogo lakini kuna mambo ambayo bado sikuyajua nimekuja kuyajua kwa sasa”

“Ebu niambie hayo mambo” Zakaria alikuwa ameshabadilika tayari hata ambaye alikuwa mbele yake alihisi kama ni msaliti kwake.

“Naitwa Razack Hakim ni jasusi wa zamani wa idara yetu ya usalama ya Libyan Intelligence Service (LIS), mimi kwa wakati huo nilifanya kazi nyingi sana ambazo zilionekana kuwa na manufaa kwa nchi na nilikuwa nikifanya kwa oda maalumu kama unavyofanya wewe hapo, sikutakiwa kuuliza chochote kile kuhusu hayo mambo ambacho nilitakiwa kukifanya ni JUST DO OR DIE maana yake ukigoma kufanya lazima ufe na hayo ndiyo maisha yetu nadhani unaelewa. Siku moja niliitwa na viongozi wakubwa wa kiserikali ambao alikuwa ni Waziri mkuu na muidhini wa wa viwango vya dawa za binadamu kwamba kulikuwa na kazi ya kuweza kuwaangalia watoto ambao wanaandaliwa kwa ajili ya CEASE THE WAR OPERATION (CWO) , niliwekwa chini nikapewa maelezo mazima kuhusiana na kile kitu sikutakiwa kuuliza wala kuhoji kwa sababu ilikuwa ni amri ya wakubwa na huo ni utaratibu uliopo sikuwa na namna zaidi ya kuianza kazi lakini kwa bahati mbaya sana watoto wote walikufa na ukabaki wewe pekeyako na hapo ndipo rasmi nilipo anza jukumu la kuweza kuhakikisha usalama wako na utimamu wako kwa kila namna kwa sehemu yoyote ile ambayo ungekuwepo kwenye maisha yako”

“Nakumbuka kuna siku wewe mwenyewe uliwahi kunifundisha kwamba binadamu anapokuwa anakosea sana hatakiwi kupewa nafasi nyingi kwenye maisha kwa sababu kufanya kitu huwa ni maamuzi iwe ni kwa kupenda au kutopenda lakini lazima wewe ndo ufanye maamuzi ndipo ukifanye, ulinieleza kwamba kama ameweza kufanya kwa mara ya kwanza akakosea au akakukosea na akapata sababu ya kusingizia basi hata kwa mara ya pili anaweza kufanya vile vile akawa na sababu ya kusingizia kwa sababu ulimuelewa kwa mara ya kwanza, nahitaji kujua wazazi wangu na familia yangu ilipoteaje kwenye hili na walihusikaje na je nawewe upo miongoni mwa hao watu ambao walihusika? Ili nijue kama kauli yako uliyo nifundisha kama iliwahi kufanya kazi kwako, huwa nakuchukulia kwangu sio kama tu mtu ambaye umenikuza kimafunzo ila nikikuangalia huwa naona neno baba ndani yake naomba usinifiche naomba uniambie ukweli naogopa sana nisije nikamgeuzia mgongo mtu ambaye nimemheshimu kwenye maisha yangu yote” neno baba lilimtoa machozi Razack Hakim, alijifuta na kuendelea

“Mheshimiwa Waziri mkuu na muidhini mkuu wa viwango vya dawa ndio hao ambao waliiua familia yako yote.

“Whaaaaaaaat?”
“Nadhani nimekueleza vizuri sana kwamba tangu mwanzo wakati wanakuja kukuomba pale kwenu baba yako aligoma kabisa wewe kuweza kuchukuliwa na serikali ambayo kiuhalisia haikuwa serikali walikuwa ni hao watu wawili tu ambao walikuwa wanatumia mgongo wa serikali kufanikisha mambo yao, baada ya wewe kuibiwa ndani ya muda fulani baba yako aliweza kujua hicho kitu alijaribu sana kuwatafuta wazazi wengine ambao watoto wao waliibiwa. Alipo wapata walikuwa na mpango wa Kwenda mahakamani Kwenda kuwashtaki watu hao ndipo hapo yalipo fanyika maamuzi magumu sana ya kuwaua watu wote wa hizo familia kulinda siri hiyo wakisingizia kwamba wanafanya hivyo kwa maslahi ya taifa la baadae”

“Noooooooooooooooo, no no, no kwanini waue familia ambayo waliidhulumu mtoto wao hapaanaaaaaaaaaaa Hapana na ulishuhudia hilo likifanyika mbele ya macho yako?”

“Mimi nilikuwa kama kibaraka tu sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kile hata hivi hapa nimetoa siri hii lazima naenda kuuawa ilikuwa ni siri ambayo nilipaswa kukaa nayo kwenye kifua changu mpaka siku ninayo ingia kaburini lakini kila nikikuona nakuonea huruma sana na baadae sana nimekuja kugundua mambo makubwa ambayo hata mimi yameanza kunitisha na kupoteza imani kabisa kwa wale watu ambao niliwahi kudhani kwamba huenda ni kweli walikuwa wanahitaji kulilinda taifa lake”

“Whaaaat is it” aliuliza kwa hasira akiwa amemkunja mzee huyo macho yake yalikuwa kama yanawaka moto leo watu ambao alikuwa anawatumikia kwenye maisha yake yote ndio alioweza kugundua kwamba walikuwa maadui wa maisha yake

“Nimegundua kwamba huu mpango ambao waliuanzisha miaka mingi sana iliyowahi kupita haukuwa wa serikali wala raisi hakuhusishwa kabisa, yule raisi wa wakati ule aliuawa kwa kisingizio kwamba alikuwa akishirikiana na magaidi lakini ulikuwa ni uongo raisi ndiye mtu pekee ambaye alikuwa anaupinga ugaidi kwa asilimia mia hivyo waliamua kumuua kwa sababu angeichelewesha sana mipango yao, baada ya kufanikiwa kumuua walimuingiza mtu wao ambaye yupo mpaka sasa lakini nae nadhani anaenda kuuawa muda wowote kuanzia sasa na atawekwa raisi mwingine”

“Shiiiiit so they have been using me and risking all my life for their own benefits? Why (kwahiyo wamekuwa wakinitumia na kuhatarisha maisha yangu yote kwa ajili ya faida zao wenyewe?) kwanini?)” mzee huyo alimuonea sana huruma kijana wake alikuwa anauliza kwa uchungu sana akiwa na hasira baada ya kugundua leo kwamba alikuwa akitumika tu kama kibaraka watu walikuwa wanaangalia faida zao na nafasi kubwa zilikuwa kwenye mikono yao.

“Hilo jambo ambalo walikuwa wanalifanya lilikuwa ni kinyume na sheria pamoja na katiba ya nchi hivyo kuna watu ambao walilipinga tangu zamani, walicho hitaji kukifanya ni kutengeneza watu wenye nguvu sana ambao wataweza kuwasaidia pale ambapo watahitaji kupata maslahi yao na pale ambapo watakuwa wanapata upinzani na ndio hicho ambacho wamekuwa wakikifanya kwako”

“Kivipi?”

“Kwa utambulisho wewe nndiyo ni komando wa nchi ya Libya lakini haujawahi hata siku moja kufanya kazi ya nchi yako, zote unazo zifanya ni za hao watu. Alih the Salijah of Jazira ni kundi la kigaidi ambalo uliambiwa kwamba ni misheni yako ya kwanza ya kiserikali lakini ulikuwa ni uongo ule ulikuwa ni mpango wao, lile kundi wao ndio waliokuwa wanalifadhili kwa miaka mingi sana mpaka linafanikiwa kuteka lile eneo la kusini mwa Libya wao walihitaji vile visima vya mafuta wavishikilie wao na ndicho kilicho tokea hawakutaka nchi itambue kama ni wao ndio wanahusika ndiyo sababu ya kuwatumia magaidi ila kuna mpishano ulitokea baada ya yule kiongozi wa hilo kundi kuhitaji kupewa asilimia nyingi zaidi ya hayo mafuta ndipo walipo amua kumuua kila kitu Kibaki kwenye mkono wao”

“Una maanisha kwamba mpaka hilo kundi linafanikiwa kuteka hilo eneo kila kitu wao walifanya na visima vyote vilikuwa chini yao?”

“Yes”

“Ohhhh my God”

“Walihakikisha yule mtu anakufa na kila kitu wanakimili wao na hicho ndo kimefanyika kupitia wewe wameweza kuliteketeza lile kundi bila kutoa hata aslimia moja ya mafuta kwenye visima kwa yule mtu nadhani unaanza kunielewa kwanini ulitengenezwa kwa gharama sana kwa sababu hata kazi unazo zifanya zimeshikilia uchumi mikononi kwa sasa uchumi wa mafuta upo kwenye mikono yao. Baada ya wewe kutoka kumaliza hiyo kazi uliambiwa kwamba unaenda kupewa kazi ya mwisho ambayo ukiifanikisha basi utaenda mbali kuishi maisha ambayo unayataka wewe hii ndio kazi hatari zaidi kwako nadhani hata wewe hujui hata mimi nimejua siku ya jana tu ndio maana nilivyopata nafasi nimekupigia simu na kukutaka uache kila anacho kifanya na urudi.

Hivi umekaa ukajiuliza huyo mtu ambaye alikuwa anakufuatilia alijua vipi kama umeenda kule? unahisi AMADOU MBAYE alijuaje kama wewe umetumwa na Kwenda kummaliza? Unahisi kwanini familia yako imepotea na imewezekanaje wakati watu ambao tulikuwa tunajua hili ni wachache sana?

Hayo yote yamefanywa na hao wote wawili, AMADOU MBAYE ni mtu ambaye wanashirikiana naye kwa asilimia karibia miamoja ila hapa walicheza karata moja ya akili sana ambayo walikuwa wanaua ndege wawili kwa kutumia jiwe moja tu. Wewe kule haukuenda kufanya kazi walikupeleka ili uuawe lakini kwenye kuuawa kwako walihitaji kwanza umpunguze nguvu sana AMADOU MBAYE kwa sababu hata yeye walitaka kumuua” Zakaria alikaa chini dunia ina siri nyingi sana na ina mambo ya kutisha mno, alijikuta anaogopa sana alikuwa anaendeshwa kama gari ambalo lipo kwenye dakika za mwisho Kwenda kwenye korongo na halina msaada wowote ule alikuwa anajichimbia kaburi lake yeye mwenyewe bila kujua ndiyo dunia yake na Zakaria ilivyokuwa.

“Wamemtumia AMADOU MBAYE kuweza kufanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kupitia makampuni yake ya usafirishaji, wamemtumia AMADOU MBAYE kuweza kusafirisha viungo vya wanadamu kupitia kampuni yake ya usafirishaji lakini pia ile ile kampuni walihitaji kuitumia kutakatisha fedha za nchi hii ambazo mpaka sasa walikuwa wamefikia kiwango kikubwa sana, walikutuma wewe kule wakiamini utaanza kuyajua haya mambo lakini wakati huo utakuwa umempunguza sana nguvu AMADOU MBAYE ili naye wamuue kirahisi sana baada ya kufanikisha mambo yao kwa asilimia nyingi hawakuhitaji hii siri iweze kutoka ndio maana kuna mtu ambaye walimtuma akufuatilie hatua kwa hatua kila unacho kifanya. Sikujua kilicho endelea huko ulikokuwa ila nilipokea simu kwamba nilitakiwa kuondoka nyumbani kwako kwa sababu nilikuwa naishi pale kwa siri, baada tu ya mimi kutoka pale ndio muda ambao familia ilipotea na baada ya kufuatilia kwa umakini sana nimekuja kugundua kwamba ni hawa hawa wawili wameweza kufanya hivyo kwa familia yako kuipeleka kwa AMADOU MBAYE wakitenda kama msaada kwa kupitia kutumiwa video na mtu wao ukiwa unamuua mtoto wa tajiri huyo na komando ambaye walimuagiza akufuatilie huko, hiyo video waliweza kuituma kwa mtu huyo ambaye aliahidi kuiteketeza familia yako baada ya kumuua mwanae ambaye alimpenda sana, hivyo hao watu walimuahidi yeye kumsaidia kukupata wewe na familia yako na kumpa taarifa kwamba wewe kule ulitumwa na serikali kwa siri Kwenda kuikamilisha kazi ya kummaliza na wao ndio wanataka kumsaidia kwahiyo familia yako ipo nchini Senegal hivi ninavyo ongea na ipo chini ya huyo mtu ambaye umemuulia mtoto wake ila wameipeleka familia yako huko sio kwamba wanahitaji kumsaidia mzee huyo kweli kukupata wewe hapana wana mahesabu yao makali sana ni watu wenye akili mno”

Mahesabu gani wanayo hawa wazee wawili mpaka wanacheza hii michezo ya pata potea sana namna hii? Ni kitu gani kwenye maisha yako hautakuja kuamini kwamba ni yule uliye muamini kakufanyia hata iweje? Hicho ndicho kinachomkuta Zakaria ndani ya chumba ambapo aliambiwa kwamba ndipo ilipo hatima nzima ya maisha yake, kivipi?

37 niseme bye-bye

Wako

Bux the storyteller
Wasalaam, leo tuguse kidogo
IMG_20230111_221127_955.jpg
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA MBILI

ULIPO ISHIA UKURASA WA AROBAINI NA MOJA
"Unatakiwa kumuamini yeye pekee kuliko unavyo jiamini wewe kwa sababu wewe pale unakuwa hupajui kabisa zaidi yake yeye,maana yake pale unaishi kwa akili yake na sio yako vipi kama akiamua kukupoteza? Lazima utakubali kwamba yupo sahihi kwa sababu wewe hujui chochote kuhusu lile eneo zaidi yake, asilimia 99 unakuwa unaitegemea akili yake na uwezo wake pamoja na maamuzi yake yeye na sio yako, sijui umenielewa mjukuu wangu?"

"Umeniacha kidogo babu"

ENDELEA........................
ZAYED UNIVERSITY (DUBAI)
Aasia akiwa mwingi wa wasiwasi alikimbia sana kuelekea lile eneo ambalo aliagizwa na kijana Khelaif baada ya kuona zile picha zake akiwa uchi kabisa pamoja na video ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa upande wake yeye hakuamini kama kile kitu kilikuwa kinamtokea yeye kwenye maisha yake, alifika pale na kuvua nguo zake kama alivyokuwa ameelekezwa ili kuweza kuokoa aibu ambayo ingempata kama mwanaume huyo angesambaza vitu hivyo. Khelaif alifika bila kumuandaa mwanamke huyo alifanya naye mapenzi kwa fujo sana Aasia hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutoa machozi tu kwenye macho yake hata hivyo mwanaume hakumjali kabisa.

"Khelaif kwanini unanifanyia hivi, kipi nimekukosea mpaka umefikia sehemu ya kunifanyia mambo kama haya? tafadhali nichukulie kama dada yako usifanye hili jambo ni hatari sana sio kwangu tu hata kwa usalama wako unaweza kuwa na wakati mfupi sana kwenye maisha yako japo utanidhalilisha"

"Hahahahahahahah, hahahahahahaha huna lolote unaloweza kuongea mbele yangu wewe kahaba, ebu nisikilize kwa umakini sana kesho saa sita usiku njoo GRAND PALM HOTEL ukufika pale simama kwa nje kuna mtu atakuja kukuchukua halafu nitakwambia ni kipi ambacho unatakiwa kukifanya"

"Whaaaat, Khelaif unataka kuanza kuniuza mimi do you know who i am?"

"Sijali wewe ni nani by the way kesho unapaswa uje uwaridhishe marafiki zangu watano na hapo ndipo nitakapo futa zile picha zako na video zako, huo muda ambao nimekutajia hapo kama ukishindwa basi unaenda kuwa maarufu sana mitandaoni"

"I'm sure I'm going to kill you Khelaif (nina uhakika naenda kukuua Khelaif)" aliongea Kwa msisitizo sana akiwa analia mno, mwanamke ameumbwa na uvumilivu sana ila kama akiamua kubadilika huo mziki wake hata shetani huwa anakaa kando kuweza kupata somo, ilimuuma sana kwa kijana ambaye ndiye pekee aliyekuwa amefanikiwa kuugusa mwili wake halafu ndiye ambaye alikuwa anamfanyia mambo ya hovyo sana namna hiyo.

"Hahahahahahahah" alicheka sana Khelaif na kuondoka. Ilipita muda ni kweli Aasia alienda mahali alipokuwa ameelekezwa, akaingiliwa kwa nguvu na wanaume sita ikiwemo Khelaif mwenyewe na marafiki zake watano. Baada ya lile tukio Aasia aliweza kurudi nyumbani kwao, wakati anafika tu getini alipokelewa na wanawake kumi (alikuwa kama malikia) walimuongoza kwenye jumba moja kubwa sana ambalo ndilo lilikuwa kasiri la baba yake.

"What's wrong with you my little princess? (Kipi kinakusumbua binti mdogo wa mfalme)" ni sauti ya upendo ambayo ilitoka upande wa juu ya ghorofa, mapenzi yalikuwa mazito sana kutoka kwa baba yake mzazi akiwa kwenye kanzu yake nzuri na ndefu za kutosha kwenye sura yake pana sana. Hakufanikiwa kujibu chochote kile zaidi ya kuendelea kulia sana, baba yake alishuka pale na kwenda kumkumbatia mwanae, alimbembeleza mpaka pale alipopelekwa chumbani kwake na wanawake zaidi ya sita.

"Mpigie simu Azidi na team yake wote waje hapa" simu ilipigwa Kwa hao watu ambao waliagizwa kufika hapo, ilichukua saa zima mpaka wakawa wamefika, walikuwa ni vijana nane
"Paaaaaa, paaaaaa, paaaaaa" risasi tatu zilipenya kwenye vichwa vya vijana watatu walidondoka hapo hapo.

"What is going on Azid?(nini kinaendelea Azid)"

"Everything is good boss(kila kitu ni kizuri bosi)"
"What the f******, where is my daughter?( Binti yangu yuko wapi?)

"Yupo chuoni bosi"

"Are you sure( una uhakika?)"

"Ye......" Hakuimalizia sentensi yake zilipenyezwa risasi tano kwenye paja la huyo kijana ambaye alijulikana kama Azid alikaa chini akiwa anagugumia maumivu alikuwa anaelewa sheria ya hapo hakutakiwa kabisa kupiga makelele wala kumfanya mtu ambaye yupo mbali na hilo eneo aweze kujua kilichokuwa kimetokea hapo.

"Kill them ( Waueni)" ni kauli moja ambayo ilitoka kwa huyo bosi, walitokea wanaume ambao walikuwa wamejifunika hood kwenye vichwa vyao walitoa mapanga yao na kusepa na shingo za vijana wote ambao walikuja na Azid hapo ndani isipokuwa yeye pekee ndiye ambaye alikuwa yupo hai japo mguu wake ulikuwa umemeza risasi za kutosha hakuwa na uwezo hata wa kusogeza mahali pengine huo mguu.

"Unaijua kazi yako?"

"Ndiyo bosi"

"Ni ipi?"

"Kumlinda madam"

"Akiwa wapi?"

"Chuoni"

"Inakuaje unakuwa hata hujui mwanangu aliko?"

"Bosi samahani sana nilikuwa sipo chuoni kwa muda nilivyoona usalama wa kutosha niliondoka na kwenda kuendelea na majukumu ya..." Damu ziliruka juu kwa nguvu alitobolewa vibaya sana shingo yake, ilikuwa ni kukosa heshima mbele ya tajiri alimpa kazi ya kumlinda binti yake leo anamjibu kwamba alikuwa kwenye majukumu mengine.

"Whoever did this i need him by now (Kwa yeyote aliyetenda hili jambo namhitaji muda huu)" aliongea sauti kali sana kila mtu humo ndani alitoka walikuwa wakimuogopa sana tajiri huyo, walitakiwa kuleta majibu haraka sana kwanini binti yake wa pekee aweze kutoa machozi namna hiyo inamaanisha alikotoka sio kwema kabisa, ndiyo sababu alimuwekea walinzi wa siri kila sehemu lakini watu hao hawakuwa na umakini kwenye kazi yao ndiyo sababu aliweza kuwaua wote.

Baada ya muda mrefu kupitia CCTV eneo la GRAND PALM HOTEL ndilo eneo ambalo kwa mara ya mwisho alionekana bibie Aasia alikuwepo kabla ya kurudi nyumbani, baada ya muda kidogo alionekana kijana mmoja ambaye alikuja kumchukua, picha yake ilitolewa, zilipita sakika tatu tu taarifa zake zilikuwa zipo mbele ya komputa kubwa sana, Khelaif ndilo lilikuwa jina lake wasifu wake ulionyesha kwamba kwa wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha ZAYED. Ni dakika chache sana msafara wa magari zaidi ya matano walifika kwenye chuo hicho, ilichukua dakika kumi tu kuweza kumpata huyo kijana waliondoka naye.

"Unamfahamu huyu binti?" Khelaif aliulizwa akiwa ndani ya gari na mwanaume mmoja ambaye alikuwa anaisafisha bastola yake

"Hapana ndiyo"

"Umelielewa swali langu?"
"Ndiyo ndiyo"
"Ni nani yako?"
"Alikuwa mpenzi wangu"
"Una uhakika?"
"Ndiyo"
"Umemfanya nini?"
"Hamna kitu hamna kitu?"
"Bwana mdogo sina haja ya kuanza kukipunguza kiungo chako kimoja kimoja kwenye mwili wako nijibu nilicho kuuliza" alimkazia macho Khelaif akiwa anamtazama machoni.

"Hamna kii...." Alipiga kelele kisu kilizama sehemu yake ya bega

"Kuna video na picha nilimrekodi lakini hakuna nilicho kifanya kibaya"

"Tupe simu yako" baada ya kuitoa simu yake mwanaume huyo aliangalia kwa muda alitikisa tu kichwa chake Kwa alichoweza kukiona ndani ya simu ya huyo kijana.

"Nani alikutuma ufanye jambo kama hili"

"Hakuna mtu ni mimi tu"
"Ulikuwa na nani?"
" Na marafiki zangu"
"Wako wapi?"
"Wapo ndani ya chuo saivi kwenye chumba namba 69" gari ziligeuzwa tena na kwenda kuwachukua hao vijana wenzake ambao walikuwa ndani ya hicho chumba. Hivyo ndivyo namna walivyoweza kukamatwa vijana hawa sita ambao walikuwa wamefungwa kwenye yard ya magari wakisubiri tajiri aweze kufika na kufanya maamuzi yake.

Huyu binadamu ambaye anatupotezea muda kuweza kumjua hapa ana maana kubwa sana kwenye hadithi hii, twende sawa sio muda utanielewa.

42 naweka nukta Kwanza tukutane wakati ujao.

Bux the story teller

Chao.
Saa mkuu tuko pamoja.
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA SITA

ULIPO ISHIA UKURASA WA AROBAINI NA TANO


"Kama utashindwa kunijibu kwa mara ya mwisho unakufa hapa hapa wewe ni nani na unamtaka bosi wa nini?" Yule mmoja wa wale wanaume wenye suti aliuliza kwa sauti kali ambayo hata hivyo haikufika mahali popote pale kutokana na sauti ya mvua na muungurumo wa radi.

"Ulikuwa na nafasi moja tu ya kuongea namimi kistaarabu umeshaipoteza sasa wewe ndiye ambaye unaenda kunijibu maswali yangu kwa lazima" aliunguruma kwa sauti yake nzito mwanaume huyo akadunda chini na kuondoka alipokuwa kuelekewa kwa hao wanaume watatu kwa nguvu sana.

ENDELEA....................
Mwanaume alijizoa hapo chini na kukimbia kwa spidi sana ilikuwa ni kama amejipiga mtama mwenyewe aliteleza kwenye maji na kuwafikia hao wanaume watatu, teke lake za mzungusho liliwakosa akainama na kujizungusha kwenye maji alikuwa anakuja na viganja vyake viwili hata hivyo alipiga hewa viliishia kutua chini ambapo maji yalitawanyika kwa nguvu alipiga zege zito ambalo lilikuwa hapo ardhi ilitetemeka, hawakuwa na hofu wale wanaume ila nadhani walishtuka sana nguvu alizokuwa nazo huyo mwanadamu mwenzao hazikuwa za kawaida kabisa hata kwa kutania, alinyanyuka akiwa haamini macho yake alitikisa kichwa kuona kama yuko sawa bado alikuwa sawa tena vizuri zaidi ya jana, aliziachia pua zake moshi ukatoka kwa wingi, ni Moshi wa sigara ambao alionekana kuuhifadhi kwa muda mrefu sana tangu atupe sigara kwa mara ya kwanza wakati anapambana na wale vijana ambao alitoka kuwaua kikatili mno hapo kwenye huo uwanja.

"Hahahaha hahahah hahahahah" alicheka kwa nguvu na kuwapa maswali wale wanaume wavaa suti watatu hawakuelewa kama mtu huyo alikuwa timamu au aliweuka hakuna kitu ambacho kilikuwa kinachelesha pale ila yeye alicheka sana.

"Nimeanza kuzeeka vibaya sana kazi za hatari kama hizi inabidi nianze kuacha kabisaa tena mapema sana nitakuwa na wakati mgumu mno kwenye maisha yangu, haijawahi kutokea nikamkosa mwanadamu yeyote na hilo pigo tangu siku ya kwanza nilipo liingiza kwenye mwili wangu, huwa nina sheria zangu kwenye upiganaji huo moshi ambao nimeutoa kwenye pua zangu ni ishara ya Kwamba kwa leo nimeshindwa pambano, huwa nikiwa sehemu nikiuhifadhi kwenye mapafu basi huwa nautoa mpaka pale ninapomaliza kazi ambayo inakuwa imenipeleka mahali husika, kuutoa bila kumaliza kilicho nileta ni ishara mbaya mno siwezi tena kukaa hapa nitawaua mapema na kuharibu kazi, naenda naenda mimi nitarudi siku nyingine hahahahahhaah" kwa mwanadamu wa kawaida akili zilikuwa kama mtu ambaye amekuwa kichaa ila huo ulikuwa ni uongo kwa sababu alikuwa ni mtu imara sana mwenye uelewa mkubwa tu kwenye kichwa chake.

Baada ya kuona ameshindwa kukifanya kile ambacho alikuwa amekipanga kwa muda wake hakuona haja ya kuendelea kukaa hapo alitakiwa kuondoka haraka mno ili arudi siku nyingine, kwenye maisha yake yote hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kuweza kumkosa binadamu wa kawaida na hilo pigo lake la kutumia viganja, viganja vilikuwa vimekomaa mno kama vile hakuwa mwanadamu wa kawaida, mwanaume alianza kuondoka taratibu kuelekea pale ulipokuwa mlango mdogo wa mtu kupita getini hakutaka tena kubaki japo, alisimama baada ya kuhisi mjongeo wa maji japo ulikuwa ni kwa mbali sana ila alielewa vizuri.

Alikimbia kwa hatua mbili tu halafu akageuka haraka mno, aliruka sarakasi ya mbele na kutua kifuani kwa mwanaume ambaye alikuwa anakuja na moja ya goti zito ni wazi alihitaji kuutegua uti wa mgongo wa mwanaume huyo, huyo mwanaume wa kazi alishuka naye mpaka chini kabisa alichomoa kisu kidogo kwenye buti lake na kukizamisha kwa huyo mtu kisu kilipita kwenye shingo kama vile anakata ni mfuko wa kubebea mahindi.

"Niliamua kuwaacha kwa leo mmeamua kuzigomea nafsi zenu ziendelee kuishi" alitamka na kusimama alipishana na ngumi mbili za kasi haikumpa shida aliinama chini na kuinuka kwa kasi aliudaka mkono wa mmoja wao na kuuvunja vibaya sana alimpiga teke la mbavu alidondokea chini kwenye maji, alikuwa mmoja ambaye bado alisimama alitaka kukimbia kisu kilikita kwenye shingo yake ya nyuma na kutokezea mbele alisimama hapo kwa dakika mbili kuonyesha kwamba alikuwa mgumu mno hata hivyo mwili wake ulimsaliti alidondoka hapo hapo chini na kupoteza maisha yake, aliyekuwa chini alikuwa anajivuta taratibu raundi hii hakukumbuka hata kuifuta suti yake alikuwa kwenye maumivu ambayo alihisi kama kuna mtu anachoma moto ndani ya mwili wake hakuelewa aushike mkono wake au mbavu zake.

"Nisamehe nisamehe" alitamka huku akiendelea kujivuta, sura yake ilionyesha kama vile analia ila mvua ilimkatili hakuweza kujulikana kama anafanya hivyo, huyo mwanaume ambaye alikuwa kwenye kombati yake alizidi kusogea na kwenda kuchuchumaa pale pale chini.

"Unapokuwa mpambanaji kwenye maisha siku zote huwa kuna kukosa na kupata ila inapotokea ukapata nafasi moja tu ambayo itakuwezesha wewe kukipata kitu ambacho umekuwa ukikipambania kwenye maisha yako yote basi hakikisha hauipotezi hiyo nafasi kwa gharama yoyote ile usije ukajidanganya au ukadanganywa na walimwengu kwamba lazima upate nafasi nyingi ndipo ufanikiwe kukipata hicho ambacho unakuwa unakipigania. Leo kwa mara ya kwanza nimetoa nafasi ya kumuacha mtu hai kwenye maisha yangu bado kaikataa hiyo nafasi yeye mwenyewe kwa kuzishindwa tamaa za nafsi yake yenye matamanio ya vitu ambavyo ni wazi hata yeye anajua kabisa kwamba hawezi kuvipata, je unahisi hata MUNGU atanilaumu kwa hili ninalo lifanya hapa kuwaua wakati mnanilazimisha wenyewe? Kwenye maisha yako yote usiamini sana ushindi kwenye kila kitu muda mwingine amani huwa ni ya thamani zaidi kwa ajili ya kuutengeneza ushindi wako wa wakati ujao" somo lake lilimuingia vizuri sana msikilizaji wake alikuwa yupo chini akiwa anatetemeka tu.

"Sitarudia tena naomba unisamehe" kifo kinatisha sana huwezi amini mwanaume wa kazi kama huyu alikuwa analia mbele ya mwanaume mwenzake akiwa anaomba tu aweze kuachiwa maisha yake.

"Wewe ni nani na unahusiana vipi na huyu bwana mdogo"
""Sisi tulikuwa ni watu wa kukodishwa tu huwa anatulipa pesa nyingi sana ili tuweze kuzifanya kazi zake"

"Unamjua vizuri?"
"Hapana namjua kikazi tu"
"Anaitwa nani jina lake?"
"Qader"
"Ni mtu wa wapi?"
"Ni mwarabu ila hajawahi hata siku moja kutupa uhalisia wa maisha yake kwa sababu kuna baadhi ya vitu huwa anavifanya kwa siri sana bila mtu yeyote yule kujua"

"Kwa sasa yuko wapi"
"Sijui"
"What?"
"Ndiyo sijui"
"Hujui alipo bosi wako unayefanya kazi kwa ajili yake?" Mwanaume aliongea kwa ukali mpaka mishipa ilijichora kwenye shingo yake.

"Siku kadhaa zilizoweza kupita aliwachukua wenzetu watatu na kuondoka nao akidai kuna kazi wanaenda kuifanya, cha ajabu mpaka leo hajarudi tena hata mawasiliano yao hayapatikani kabisa, tulijaribu sana kuwatafuta kila sehemu hata hivyo hatukufanikiwa kabisa kuwapata, nyumba zake zote hayupo hivyo sijui yupo upande gani wa dunia kwa sasa"

"Umesema nyumba zake? Ana nyumba ngapi kwani?"
"Nazo zifahamu mbili"
"Wapi na wapi?"

"Hapa pamoja na Kibo"
"Namba ya nyumba?"
"1079"

"Kwa leo nakuacha hai kwa sababu umekuwa muwazi kwangu na hii ni nafasi ya pili kuipata jitahidi sana uitumie vyema, nenda sehemu fungua biashara, tafuta mwanamke mzuri sana muoe mpate watoto wazuri mfurahie maisha ,hiki kitabu ulichokuwa unataka kukifunua hauwezi kuisoma hata kurasa yake moja tu hivyo jitahidi ukae mbali na haya mambo kurasa zake ni nzito na zinatisha mno tunajaribu kufuatilia maisha ya kiumbe ambacho kinadaiwa kuwa cha hatari sana na ndio hicho ambacho natamani siku moja nikutane nacho nijipime uwezo ili niwe na uhakika kama kwenye dunia hii kuna watu wanaweza kunishusha chini kwa lazima bila mimi kuhitaji"

"Asante sana asante sana ila samahani pia najua umeniacha kwa mapenzi yako naomba niruhusu nikuulize maswali kidogo" mwanaume huyo ambaye alikuwa amesimama tayari ili kuondoka humo ndani baada ya kumkosa mtu wake aligeuka nyuma na kumtazama kijana huyo kisha akatabasamu, hiyo ilikuwa ni alama ya kumruhusu aulize kile ambacho alikuwa nacho kwenye kifua chake.

"Hivi wanadamu wagumu sana kama nyie huwa mnaishi wapi hapa nchini na huwa mnatengenezwa hivyo kwa ajili ya kazi zipi? Imenitisha na kunitisha tena kwenye maisha yangu kukutana na mtu wa aina yako nimeogopa mno" aliongea na kujiweka sawa alikuwa na amani kwa sababu alikuwa ameachwa hai hakuwa na wasiwasi sana na hilo zaidi ya kuweza kuuhangaikia mkono wake pamoja na mbavu yake moja ambayo iliteguliwa vibaya.

"Watu kama mimi wapo tena wapo wa kutosha tu ila wewe huwezi jua wanapatikana wapi hilo sahau mpaka unakufa huwezi kuambiwa kwa sababu wengine mnaishi nao huko huko mtaani unawazoea na kujua ni wanyonge wenzako, wapo wanao uza chipsi mtaani, wengine wanajifanya wabeba vyuma ambao hawana kazi mtaani, wengine ndio hao vichaa waokota makopo mabarabarani ambao mnawadhihaki kila siku ndivyo hivyo viumbe vya ajabu namna vinavyo ishi sasa kijana wa kawaida kama wewe unawaona na kuwajulia wapi? Mimi hivi unavyo niona sijawahi kukutana nao lakini najua kuna watu hata mimi hapa mi wa kawaida mno nikisimama nao, hawa watu huwa hawatokei kila sehemu huwa wanatokea kwenye matukio ya mhimu tu kwenye maisha yao unaweza ukawa haujawahi kumuona hata mmoa ila wapo tena sana. Unadhani nani anahakikisha usalama.wa wananchi? Unahisi amani inalindwa hovyo hovyo tu? Kuna watu wanayatoa maisha yao ili wengine muishi kwa amani halafu unamkuta mwananchi wa kawaida tu amekaa kilingeni akiwa anatukana mamlaka huku anakuna kitambi chake kwa amani kabisa bila kujua hiyo amani inayo mfanya kuwa huru inapatikana vipi, na hizo ndizo kazi zetu ambazo tunazifanya, tuna muda mchache sana wa kuupata usingizi kama wanavyo fanya wananchi wa kawaida tu, jibu la swali lako nafikiri ni kwamba tupo kila mahali ila wewe hautakuja kujua namna ya kutupata kwenye maisha yako yote hata mimi hapa huenda baada ya leo hatutakutana tena kwenye haya maisha. Chunga tu na ujue namna ya kuutumia mdomo wako kwa usahihi, mahala sahihi na kwa kitu sahihi" alimaliza kuongea na kuanza kuondoka hakutaka kuendelea kukaa hapo tena.

"Jina lako?" Ni sauti ambayo aliisikia kwenye masikio yake kutoka kwa huyo kijana ambaye alilala chini

"Chagua mawili ukinijua basi maisha yako yanaishia hapa lazima nikuue au niondoke zangu nikuache hai" kauli yake haikujibiwa kabisa alicheka baada ya kugundua kwamba kijana huyo alikubali tu kutokumjua mtu huyo ili awe salama.

"Joash" alitamka kwa msisitizo na kutokomea nje ya geti hilo.

Unamkumbuka Joash? Ni nani? Na anadai anataka kukutana na kiumbe gani ili ajipime naye? 46 nanyoosha mikono juu tukutane wakati mwingine.

Langu jina naitwa

Bux the story teller

Chao.

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Febian nipo safarini, nikifika ninapoenda kesho saa nne asubuhi nitakucheki Kaka.
 
Back
Top Bottom