STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+
UKURASA WA HAMSINI NA SITA
TULIPO ISHIA UKURASA WA HAMSINI NA TANO
Kama itatokea kuna siku utajifariji kwamba pesa sio kila kitu basi usije ukatamani kukaa maeneo ya majiji wala mjini, nenda kijijini huko ukalime na kula mtunda tu basi ukizisubiri siku zako za kutoweka hapa duniani, pesa imebeba zaidi asilimia 90% za maisha ya mwanadamu kwa sasa, MONEY IS NOT EVERYTHING BUT MAKE SURE YOU EARN ALOT BEFORE SPEAKING THAT NOSENSE (PESA SIO KILA KITU ILA HAKIKISHA UNAKUWA NAYO YA KUTOSHA KWANZA KABLA YA KUONGEA HUO UJINGA)" yalikuwa ni maelezo mafupi ya bwana Kanivasi Zagota akiwa anahojiwa na mdada mmoja mrembo sana wa moja ya chombo cha habari ndani ya nchi ya Tanzania, alikuwa ni tajiri mpya ndani ya nchi ambaye aliwekeza pesa yingi sana kwenye biashara ya madini, usafirishaji na kusaidia jamii.
ENDELEA...............................
"Mheshimiwa kuna kitu ambacho umewahi kukijutia sana kwenye maisha yako mpaka leo umekuwa kwenye mafanikio makubwa sana namna hiyo?"
"Ndiyo kipo kipo siwezi kabisa kukisahau kwenye maisha yangu huwa kila nikilala na kuamka nakikumbuka sana tena sana"
"Unaweza kuwaambia vijana wenzako wapambanaji hapa ili nao wapate somo kidogo huenda ukawaongezea kasi ya upambanaji mtaani huko"
"Mhhhhh vijana wa siku hizi wanaishi kwenye dunia tofauti sana ambayo inawaweka mbali sana na mafanikio, wana roho nyepesi sana na kuhisi wana kila kitu wakati uhalisia wana maisha magumu sana"
"Lakini bado hujatuambia hilo jambo mheshimiwa"
"Hahahaha hahahaha hahaha nakumbuka nakumbuka wala siwezi kusahau kabisa swali lako UMASKINI ndilo jambo ambalo huwa nalijutia zaidi kwenye maisha yangu, umaskini unatisha sana, umaskini ni ugonjwa tena sio ugonjwa tu bali ni ugonjwa sugu tena sugu sana hapa ninaweza kueleweka kwa watu wachache sana kwa sababu umaskini unatofautiana sana. Elimu ya darasani inakwambia kwamba umaskini ni hali ya kushindwa kuyamudu mahitaji yako ya mhimu ambayo ni chakula, mavazi na malazi, lakini hapo hapo kumbuka kuna watu hivyo vitu vyote wanavipata lakini kwa kiwango kidogo je kwamba wao sio maskini? Jibu rahisi ni kwamba hata wao ni maskini ila wamepishana kiwango tu maana kuna wale maskini ambao wanacho lakini hawana kila wanacho kitaka na kuna maskini ambao hawana hata kimoja kati ya hivyo.
Sasa mimi nipo kwenye kundi la maskini ambao hawana chochote hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu mimi, huwa nakiheshimu sana chakula cha jalalani kimenikuza mimi, kimenifanya nikawa mtu mzima hicho chakula ambacho wengine hawaruhusu hata mbwa wao wale kwangu ilikuwa ni zawadi ya kila siku, mtaa umenikuza, mtaa umenilea, mtaa wa mianzini pale nimekaa sana hakuna kitu cha kutisha na kuhatarisha maisha yangu sijakifanya sasa kwanini nisijutie kuwa maskini, ukipata nafasi unabidi uyaishi maisha na kuyafanya kuwa mazuri kwa namna yoyote ile kwa sababu hiyo nafasi huwa haijitokezi mara mbili mbili.
Hapa unapo niona nikikwambia niliwahi kupigwa fimbo mia moja na hamsini ili nipate tu mfupa wa kutafuna unaweza ukaniamini? Umekulia kwenye maisha safi kazi yako kubwa ni kushika kalamu tu na maiki baada ya hapa kuna gari ya kifahari inakuja kukuchukua utaelewa nini kuhusu haya maisha? Umaskini ndicho kitu kibaya zaidi ambacho mimi nimewahi kukipitia, umaskini unadhalilisha sana, umaskini unakufanya hata mapenzi uishie kusimuliwa, umaskini unakufanya haki uipate kwa MUNGU tu pekee hakuna sehemu duniani utaipata haki kama wewe ni maskini labda hiyo sehemu mtawala wake awe ni baba yako, kwahiyo hizo nguvu ambazo unaziwekeza kulalamika sana kwa kuipigania haki yako itumie kuzitafuta pesa kwa namna yoyote ile kwa sababu bila hizo pesa hakuna sehemu utakuja kuipata hiyo haki mpaka siku unakufa" ni maelezo ambayo yalimtoa machozi kila ambaye alikuwa amekodolea macho yake kwenye skrini, ilikuwa ni hotuba ambayo ilijaa majivuno sana lakini kwenye hayo majivuno yaliongelewa mambo ya maana sana ambayo yalimfanya kila mzazi aone ana jukumu zito sana kwenye malezi ya mtoto haikuwa sawa mtoto kupokea fimbo miamoja na hamsini ili tu apate mfupa wa kutafuna ili kupunguza njaa huku wewe ukichagua nyama ya kuku na nyama zingine unawarushia mbwa bado hujayajua maisha.
Mwanaume ambaye alikuwa anatoa hayo maelezo alikuwa anaitwa Kanivasi Zagota, tajiri ambaye aliibuka na kuwa na pesa nyingi sana ndani ya jiji la Dar es salaam watu wengi sana walitamani kumtumia kama mfano wao kwa vijana wote wapambanaji bila kujua mwanaume huyo huo utajiri aliupatia wapi , siri sirini ndani ya dunia, ajabu licha ya kuwatoa watu machozi sana namna hiyo yeye uso wake ulikuwa mkavu sana huku akiwa anatabasamu bila wasiwasi, hata mtangazaji alishindwa kuvumilia alitoa kitambaa chake na kuinama akajifuta machozi yake kwa sababu hata yeye alikuwa anaenda kuwa mama kwenye jamii jukumu la kulea watoto lilikuwa linaenda kuwa chini yake mpaka siku anakufa hakuna hata siku moja mtoto utaacha kuwa chini ya wazazi wako mpaka siku unakufa hata ukiwa na mji wako kuna maamuzi huwezi kuyafanya bila kuwashirikisha wazazi wako ( poleni sana kwa mlio wapoteza wazazi wenu, it suddens me alot when i remember R.I.P my DADY).
"Sasa mheshimiwa unawashauri nini vijana ambao sasa ndo wanaingia kwenye utafutaji na wengine tayari wapo huko?"
"Mhhhhh unamaanisha vijana wa siku hizi?"
"Ndiyo"
"Sina ushauri wowote kwao mwenye shida na pesa anajua njia ya kuzipata"
"Unamaanisha nini mheshimiwa? Kama wana uhakika na wanajua pa kuipata unahisi wangekuwa wanateseka mtaani huko?"
"Hahahaha nikuulize swali bibie?"
"Ndiyo mheshimiwa"
"Hapo ulipo muda huu unamiliki kiasi gani cha pesa?"
"Siwezi kutaja ila kwa kuishi sina shida sana"
"Ukiwa huna hata mia halafu mama yako akazidiwa anataka kufa inatakiwa laki tano tu ili umuwahishe hospitali ili uokoe maisha yake utaikosa?"
"Hapana hiyo pesa kwa namna yoyote lazima ipatikane?"
"Unaipata wapi na pesa hauna"
"Hapo nitafanya jitihada yoyote au njia yoyote mpaka pesa ipatikane na ni lazima niipate"
"Hahahaha hahahaha ndugu mwandishi wa habari nafikiri nimekujibu swali lako tayari"
"Khaaaa kivipi tena mheshimiwa?"
"Si umesema lazima upate pesa kwa namna yoyote ile ili uokoe uhai wa mama?"
"Ndiyo"
"Sasa kama unaweza kufanya hivyo kwenye kuyapigania maisha yako unayo enda kuishi mwenyewe unashindwaje? Kumbe njia zipo na zinajulikana ila watu wanasubiri mpaka yakiwafika shingoni ndio huwa wanazikumbuka"
"Mhhhhhhhh mheshimiwa"
********************************
"Umaskini ni kama gonjwa ambalo athari zake zinajulikana sasa hizo athari zake kwenye kuzikabili ndo watu wanatofautiana, ni sawa na Leo unajua kwamba UKIMWI upo na unaua, njia zake za kuambukizwa unazijua, namna ya kujikinga bado zinajulikana kwanini sasa watu wanaendelea kuupata?. Umaskini ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine ambao unaua watu kinacho takiwa ni kujifunza namna ya kujikinga na athari zake na wale ambao hawana huo uwezo wa kuzikinga hizo athari zake basi ni wasaidiwe kama wana hao watu au kama hawana basi wahakikishe wanafanya maamuzi magumu sana kwenye kujikinga na gonjwa hilo. Ndugu mwandishi nadhani muda wangu wa kukaa hapa umetosha kwa leo ngoja nikalihangaikie tumbo langu nisije nikarudi kule ambako nilikuwepo zamani" mwanaume alimaliza maelezo yake ya kuvutia ambayo kila ambaye alikuwa anaangalia kipindi hicho alipiga makofi kwa furaha sana, ukiambiwa mwanaume huyo halijui darasa hata moja usingeweza kuamini kwa mambo ambayo alikuwa anayaongelea.
Huyu ndiye yule Kani rafiki wa zamani wa Alen kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite, maisha yalimuendea Kasi kwa sasa alikuwa anaheshimika sana ndani ya nchi hii kwa sababu ya kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho alikuwa anakimiliki, sio yule Kani wa kulilia shilingi elfu moja za kitanzania alikuwa ni Kani ambaye kwa sasa alikuwa anatembea na msafara wa magari ya kutosha.
Mwanaume alitoka kwenye kituo hicho kikubwa cha habari akaingia kwenye gari yake moja ya kifahari na kuondoka mahali hapo, msafara wa gari tatu ulitosha kuelezea namna mtu huyo alivyokuwa na ukwasi wa kutosha kwenye mifuko yake, akiwa ndani ya gari yake hiyo kuna meseji iliingia kwenye simu yake akaitoa na kuiangalia kwa muda kidogo kisha akamuagiza dereva wake gari aelekee nayo baharini. Kutoka Mwenge kuelekea mbezi beach ilikuwa ni Safari ya muda mfupi sana , alifika na kushuka kisha akaletewa kiti na kukaa akiwa anaivuta sigara yake.
"Sogeeni pembeni" aliongea bila hata kuangalia nyuma akimaanisha kwamba mtu aliyekuwa nyuma apewe nafasi ya kupita mpaka mbele, kweli nyuma walikuwepo wale wanaume watatu ambao muda fulani walionekana ndani ya hospitali ya mkoa ndani ya Arusha, alitumiwa meseji kwamba ndani ya msafara wake kuna gari limeongezeka kutoka kwa walinzi wake ambao walikuwa kwenye gari ya nyuma ndiyo sababu alihitaji kuwajua ni akina nani hao ambao walikuwa wakimfuatilia.
"Ni akina nani nyie na mnataka nini?" Aliongea bila hata kugeuka akilipiga funda lake la sigara akisindikizwa na upepo safi wa bahari, wala usingeamini kwamba ndiye yule Kani wa enzi zile.
"Wewe ndo Kani?" Baada ya kutajiwa jina lake alinyanyuka na kuiweka suti yake vizuri kisha akamsogelea mwanaume mweusi sana mwenye upara akiwa ameongozana na wenzake waarabu wawili.
"Mhhhhh ni nani wewe ambaye sikujui na wewe unanijua?
"Tumekuja kukuchukua tondoke wote"
"Hahahaha hahahaha hahahahahah" Kani alicheka sana tena sana, wanaume hao walipata hasira mno yule black alikishusha kibao chake ili amzabe nacho mwanaume huyo alikishusha wakati kinaelekea eneo la shavu alijikuta anapokea ngumi kama tano kwenye uso wake alishangaa kwa sababu aliambiwa Kani alikuwa dhaifu sana kweli alivyo mwangalia Kani alikuwa amesimama vile vile akiwa anavuta sigara yake kubwa huku mlinzi mmoja akiwa analifuta koti lake la suti.
Nini kimefanyika hapa, Kani ndiye kawa mtu hatari sana namna hii au kuna siri gani? 56 inafika mwisho
Bux the story teller
Chao
Sent from my TA-1053 using
JamiiForums mobile app