Gereza la Ukonga ni 'Maximum Security Prison'. Tuache upotoshaji. Masharti yake ni tofauti na gereza la kawaida kwa manufaa ya pande zote mbili

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,751
Kila nchi ina magereza yanayoitwa maximum security prisons. Magereza ya aina hiyo yanakuwa na ulinzi mkali na masharti tofauti kwa wanaoshikiliwa (inmates) humo ukilinganisha na kwenye magereza ya kawaida..

Hii ni kwa faida ya wanaoshikiliwa humo wasije wakadhuriwa na maadui wao wa nje wanaoenda kuwaona kuwaona gerezank kwa mfano kwa kulishwa sumu au kuchomwa na ncha kali. Watu wanaoshikiliwa humo wenginewao ni tishio kwa usalama wa nchi. Hawa kwa kushirikiana na rafiki zao wa nje wanaokuja kuwaona gerezani wanaweza kufanya mipango ya kuwatorosha gerezani au mipango mingine miovu dhidi ya nchi.

Hivyo katika magereza hayo ya maximum security prisons duniani kote, wote wanaoruhusiwa kuwaona hao inmates idadi yao huwa limited, mazungumuzo yao na mienendo yao wakiwa na inmate huwa closely monitored and recorded na maafisa wa magereza na kwa nyezo nyingine za kiusalama hususani makamera ya cctv etc. Hakuna mazungumuzo ya faragha ukiwa humo.

Hata kama askari magereza wakiwa hawamo kwenye hicho chumba cha inmate physically, wanakuona na kukurekodi kila kitu remotely kupitia teknolojia ya tehama. Utakuwa unajiganganya tu hata ukiongea kiingereza au kinyaturu haisaidii kitu.

Gereza letu la Ukonga ni mojawapo wa aina hiyo ya magereza duniani yenye maximum security. Huyu jamaa yetu ana rafiku zake wa karibu wengi wanaoishi ughaibuni ambao wangalipenda kumtoroshea huko kwa mbinu zo zote.zile.

Jamaa yetu huyu ana maadui wengi asiowajua na wengine anaamini ni marafiki zake kumbe sivyo. Hawa kwa ushawishi wa fedha au kwa chuki zao wanaweza kumudhuru kwa sumu au ncha kali au mbinh zingine akiwa kwenye chumba cha magereza. Ndiyo sababu ya kumuhamisha kutoka gereza la kawaida alilokuwa la Keko kwenda gereza la Ukonga Maximum Security Prison. Tuachane na upotoshaji.
 
1744456446209.jpg
 
Wakiwa wengine mnaona ni sawa, ni mpaka wahusika wakiwa wazazi au ndugu zenu
 
Wewe ni Mjinga
Jibu hoja acha matusi, hayasaidii. What's the definition of a maximum security prison? Achana na upotoshaji na ubwabajaji wa mawakili wenu akina Kibatala. Lengo lao ni ku prolong tu hiyo kesi ili hiyo hela mnayokusanya ya tone tone iishie kuwalipa hao mawakili lukuki wanaomtetea mwenyekiti wenu.
 
Nilikuja speed nikijua utaweka vifungu vya sheria.

Je, maximum security prison ni jina tu au ni taasisi iliyopo kisheria?? Na sheria zake ni zipi?

Naona ni kama umeleta tu story isiyokuwa na basis yoyote ki taaluma.

Rekebisha hayo makosa na u justify unachokisema, otherwise utakuwa hujalitendea haki jina lako
 
Inamaana Lissu ndo mahabusu wa kwanza kupelekwa gereza la Ukonga?
Pia Lissu hajakutwa na hatia hivyo siyo mfungwa ni mtuhumiwa bado yupo mahabusu. Sasa tupe hizo sheria za maximum prison.
 
Nadhani unajua maana ya inmates. Gereza hilo ni kwa ajili ya kuwalinda aina fulani ya inmates. Inmates ni watu wanaohifadhiwa magerezani. Wanaweza kuwa ni convicts au rumandees yaani waliohukumiwa na wale walio mahabusu.
 
Kila nchi ina magereza yanayoitwa maximum security prisons. Magereza ya aina hiyo yanakuwa na ulinzi mkali na masharti tofauti kwa wanaoshikiliwa (inmates) humo ukilinganisha na kwenye magereza ya kawaida..

Hii ni kwa faida ya wanaoshikiliwa humo wasije wakadhuriwa na maadui wao wa nje wanaoenda kuwaona kuwaona gerezank kwa mfano kwa kulishwa sumu au kuchomwa na ncha kali. Watu wanaoshikiliwa humo wenginewao ni tishio kwa usalama wa nchi. Hawa kwa kushirikiana na rafiki zao wa nje wanaokuja kuwaona gerezani wanaweza kufanya mipango ya kuwatorosha gerezani au mipango mingine miovu dhidi ya nchi.

Hivyo katika magereza hayo ya maximum security prisons duniani kote, wote wanaoruhusiwa kuwaona hao inmates idadi yao huwa limited, mazungumuzo yao na mienendo yao wakiwa na inmate huwa closely monitored and recorded na maafisa wa magereza na kwa nyezo nyingine za kiusalama hususani makamera ya cctv etc. Hakuna mazungumuzo ya faragha ukiwa humo.

Hata kama askari magereza wakiwa hawamo kwenye hicho chumba cha inmate physically, wanakuona na kukurekodi kila kitu remotely kupitia teknolojia ya tehama. Utakuwa unajiganganya tu hata ukiongea kiingereza au kinyaturu haisaidii kitu.

Gereza letu la Ukonga ni mojawapo wa aina hiyo ya magereza duniani yenye maximum security. Huyu jamaa yetu ana rafiku zake wa karibu wengi wanaoishi ughaibuni ambao wangalipenda kumtoroshea huko kwa mbinu zo zote.zile.

Jamaa yetu huyu ana maadui wengi asiowajua na wengine anaamini ni marafiki zake kumbe sivyo. Hawa kwa ushawishi wa fedha au kwa chuki zao wanaweza kumudhuru kwa sumu au ncha kali au mbinh zingine akiwa kwenye chumba cha magereza. Ndiyo sababu ya kumuhamisha kutoka gereza la kawaida alilokuwa la Keko kwenda gereza la Ukonga Maximum Security Prison. Tuachane na upotoshaji.
Malipo huwa ni hapa hapa Duniani..

Ipo siku ndugu yako wa damu, ata kamatwa kwa kesi ya mchongo, mkatazwe kuongea naye..
Kwa kisingizio cha security.

Nadhan hapo Akili zita kurejea
 
Ok hakikisheni Lissu afya yake ni njema msimamieni ale vizuri
...anaenda kugoma kula, na kama kawaida, CHADEMA kama ilivyokuwa "wakususa susa" na Laigwanaan Tundu chakula anasusa. -hiyo ni sera yao
na afanye mazoezi hasa ya kuruka kichura ili kujenga afya yake.
🔥😅😁😁😁😉 na atoke kile
kijasho cha kweli😂😂😂😂😂

🤯on the other side🤔mmmm naona psysiology alignment itaenda kutoka.

Wachange tone tone wampelekee wachuaji huko, manake hivi vichura chura na huku tunavyosikia atapoenda kugoma kula, Aikambe ...mwili hata ukiwa kama Shujaa Mkwawa utanyong'onyea.

Kwa kweli wahakikishe afya yake ni njema.
 
Nadhani unajua maana ya inmates. Gereza hilo ni kwa ajili ya kuwalinda aina fulani ya inmates. Inmates ni watu wanaohifadhiwa magerezani. Wanaweza kuwa ni convicts au rumandees yaani waliohukumiwa na wale walio mahabusu.
Sijakata Dr Akili ndiyo nilikua nakuomba utuelimishe zaidi kwa sheria za maximum prison ili tupate uelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom