GEREZA NI SHULE YA UCHUMI
Gereza ni sehemu au makazi ambapo wakosefu wa sheria za nchi Fulani wamekua wakiishi kwa ulinzi na uangalizi mkali. Inafahamika kua gereza ni sehemu ya kuadhibu watu ambao wamekiuka maadili yaliyowekwa na jamii ya watu Fulani au nchi Fulani.
Katika Maisha ya kawaida wanadamu hutofautiana kitabia na maadilii pia hivyo hupelekea baadhi ya watu kua na maadili hasi na tamaa hali ambayo huwapelekea kua na tabia zisizokubalika katika jamii, hatimae kushutumiwa na kupelekwa gerezani kwa muda wa miezi au miaka kadhaa au kifungo cha Maisha.
Gereza linafahamika kua ni sehemu ya adhabu kwa mtu mkosefu ambaye alifanya kosa au makosa tofauti akiwa uraiani. Adhabu hii imewekwa ili kumfundisha mkosaji ya kwamba kosa alilolifanya lina ukubwa na halikubaliki kwa kiasi gani katika jamii.
Mbali na mfungwa kukosa uhuru wa kufanya shughuli zake za kiuchumi lakini pia mfungwa huyo hukosa uhuru pia wa huduma ya chakula kizuri, na malazi mazuri pia. Achilia mbali huduma zingine kama vile huduma za afya.
Nchini Tanzania tumekua na magereza mengi na makubwa mno kiasi ambacho yanamiliki watu wengi sana. Kutokana na hali hiyo magereza mengi nchini Tanzania yamekua yakimiliki nguvu kazi nyingi sana.
Wengi wa watu wanaojaa magerezani ni wale ambao makosa yao ni wizi, utapeli na dhuluma. Matatizo haya hamekua yakikithiri kwa kiasi kikubwa sana kutokana na wengi wa watu kua na hali duni ya kiuchumi na kushindwa kua na uvumbuzi wa kazi gani wafanye ili waweze kujipatia kipato halali.
Kukosekana kwa elimu ya ufundi ambayo vijana wangeweza kujiajiri au mtaji ambapo kijana angeweza kuanzisha biashara yake hupelekea kuingiwa na tamaa na kuchukua maamuzi hasi dhidi ya sheria iliyowekwa na nchi. Hali hiyo hupelekea vijana kufungwa gerezani na hatimaye kurudi tena uraiani wakiwa hawana dira wala muelekeo kiasi ambacho hupelekea kurudia tena kosa na kurudi tena gerezani.
Kutokana na kupoteza nguvu kazi nyingi sana katika jamii zetu, familia zetu zimekua zikiangamiza vijana megerezani ambao wangeweza kupambana vikali mtaani na kujipatia riziki halali kisha kusaidia familia na jamii zao.
Mbali na hayo sio familia tu au jamii inayomzunguka kijana huyo bali pia hata serikali hupata hasara kubwa mno kutengeneza magereza na kuwafunga hawa vijana.
Hasara ambayo serikali inapata sio tu gharama ya kujenga majengo na miundombinu ya magereza pia kuwalipa mishahara wasimamizi wa sekta hiyo yaani askari magereza, kikubwa Zaidi serikali hupata hasara kwa vijana wanaofungwa magerezani kwani hawawezi kufanya shughuli yeyote ya uzalishaji mali kiasi ambacho hupelekea wasichangie kunako pato la taifa na kusababisha kushuka kwa pato la taifa.
Nini kifanyike…
Serikali iandae mkakati yakinifu na madhubuti wa kuhakikisha kua wanaligeuza gereza kua shule ya mafunzo kwa kuwafundisha wakosefu jinsi gani wanapaswa kuishi badala ya kufanya kama sehemu ya kutolea adhabu kwa wakosefu wa sheria za nchi.
Serikali iandae gereza liwe kama sehemu ya kuchangia pato la taifa katika nchi badala ya gereza kutegemea pesa za serikali na kuendeshea shughuli zake hali ambayo husabaisha kupunguza pesa za serikali ambazo zingeweza kusimamia miradi mingine ya kimaendeleo.
Gereza ni shule…
Serikali itengeneze mazingira na miundombinu ya kuwezesha wafungwa gerezni wawe wanapata mafunzo ya ufundi ya muda mfupi Ambayo yanaweza kuwasaidia wafungwa hao kujiajiri mara baada ya kutoka kifungoni,
Mafunzo hayo yaambatane na mazingira halisi ambayo wafungwa hao wanatoka. Mafunzo kama vile kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, ufundi wa kushona nguo, ujasiliamali wa kutengeneza sabuni na vitu vingine hitajiki katika jamii, mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa.
Gereza liandae muda maalumu ndani ya kila wiki kuwe na vipindi na madarasa pia wapatikane walimu watakaotoa mafunzo hayo kwa wafungwa. Gereza pia liwe linafanya mafunzo kwa vitendo, yaani kama ni mafunzo ya ufigaji basi gereza liwe na mradi mkubwa wa ufugaji kuku au Wanyama na wafanyakazi husika wawe ni wafungwa.
Gereza pia litoe mafunzo kwa vitendo kama ni kilimo, basi wafungwa waandae mashamba wakiwa wanasimamiwa na mtaalam wa kilimo na waelekezwe kulima kisasa wakiwa na lengo la kutoa elimu na sio adhabu tena kwa wafungwa hao.
Gereza litoe elimu ya utengenezaji wa bidhaa ndogondogo hitajiki katika jamii ili kuweza kuwapa fursa wafungwa mara baada ya kutoka gerezani na kuweza kujiajiri.
Gereza ni pato la taifa…
Kutokana na uwekezaji mkubwa wa sekta ya magereza, sekta hiyo itaweza kujitengenezea pato lake lenyewe na kuchangia kunako pato la taifa. Gereza pia litaweza kujitegemea kutokana na uzalishaji mkubwa wa mali na uchumi kiujumla. Gereza litaweza kutumia jumla ya makusanyo yake na kusaidia kunako matumizi yanayohusu magereza mfano ununuzi wa magari na vifaa vya magereza, malipo ya mishahara ya Askar na wafanyakazi wote wa magereza yanaweza kusaidia kutatua mahitaji yote yanayohusu matumizi ya magereza.
Hivyo basi shughuli za kiuchumi katika sekta ya magereza zitawezesha kuchangia pia pato la taifa na kusaidia kukuza uchumi nchini.
Kutokana na hayo yote serikali itakuainatengeneza kuvu kazi mpya mara baada ya vizazi vinavyotoka gerezani kua vinazalisha mali na pia kusaidia kuingiza mapato mengi sana kutoka katika sekta hiyo ya magereza pia itaweza kupunguza matumizi mengi ya bajeti kwa mwaka wa fedha unaofuata na kusababisha kua na bajeti kubwa itayoweza kusaidia sekta nyingine kuimarika.

Upvote
1