Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
GEREZANI DAY 2022: GEREZANI IMEBADILI MAJINA YA MITAA KUWAENZI WAZEE WAO WALIOPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Leo WanaGerezani wameadhimisha siku yao ya familia kwa kuwarehemu masheikh, wazee wao na wenzao waliotangulia mbele ya haki.
Shughuli ilifanyika Shule ya Kisarawe na ilitanguliwa kwa khitma na kisha kupambwa na hotuba za viongozi wa serikali.
Furaha ilionekana waziwazi pale Salum Abdallah Matimbwa alipotangaza kuwa Gerezani imeamua kuhifadhi historia yake iliyotukuka ya kupigania uhuru wa Tanganyika isipotee kwa kuipa baadhi ya mitaa yake majina ya wazee wake waliokuwa mstari wa mbele dhidi ya ukoloni.
Mtaa wa Lindi sasa utajulikana kama Mtaa wa Bi. Tatu bint Mzee na Mtaa wa Congo utaitwa Mtaa wa Iddi Tulio.
Picha ya mwisho kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee akiwa na Bi. Titi Mohamed na Bi. Chiku bint Said Kisusa wakimsindikiza Rais wa TANU Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955.