German shepherd 8 wamezaliwa leo home kwangu naomba tips za kuwapa mafunzo hatua zake kwa ujumla

JITU LA MIRABA MINNE

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
726
Reaction score
476
Ninafurahi sana kupokea taarifa hizi toka home vigerman shepherd 8 vimezaliwa leo nataka nivipe mafunzo ya kikamanda na ulinzi naomba tips za namna ya kuwafundisha ulinzi ikiwezekana kila mmoja niweze kumpangia majukumu yake katika muundo wa nyumba
mm ni mpenzi na mbwa sana hadi shemeji yenu ana lalamika kwamba nampend mbwa kulik yeye
Karibuni mafriends wote




























Hao hapo juu makamanda wangu nilikua busy na safari wakulu wangu
 
Tupia kapicha mkuu
 
Kabla ya hizo tips......angalia uwezo wa kuwatunza hizi week mbili za mwanzo pamoja na dawa.
Secondly Mbwa nane ni wengi saana wapunguze wabaki wawili au watatu max.
Kama ni Arusha wapo dog trainners na vet clinics
 
Wawekee mazingira mazuri yenye joto na hakikisha mama yao ana chakula cha kutosha kwa ajili ya kutengeneza maziwa yake. Inashauriwa ungempatia chakula cha puppy pia huongeza maziwa.
Kuwatunza puppy ni changamoto, though GSD wapo vizuri kwenye uleaji.

Usipocheza na ishu ya mazingira utaambulia puppies wachache.

Mimi nilipata puppies saba and all wapo sawa. Wana 3 months now.

Otherwise hongera and wishing you all the best kuwatunza mkuu.
 
Kwa mahitaji ya chakula chao nione ninatengeneza chakula bora kabisa natafute kwa namba hii 0625606086
 
Wewe kama mimi. Napenda sana mbwa. Unauza bei gani?
 
Kama unafahamiana na askari Polisi kikosi cha mbwa na farasi jaribu kuwasiliana nao wanaweza kukusaidia kuwafundisha mbwa wako wakafikia mpaka kiwango cha kuweza kumtambua mwizi aliyekuibia hata kama atakuwa amejichimbia katikati ya kundi la watu atachomolewa tu,hata kama utataka kupigiwa paredi pamoja na kupigiwa salute utapigiwa.
 
Hiv wale wa police wanauzwaje
 
Nikiwa na kwangu nitafuga mbwa ila si wengi hivyo
 
Hiv wale wa police wanauzwaje
Sijui bei yao lakini ukiwa jirani nao wanaweza wakakufanyia mpango wa kukuuzia vimbwa vidogo ambavyo vinazalishwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya kiutendaji na vinaweza vikapatikana katika chuo cha mafunzo Moshi,Siku za nyuma nilikuwa na rafiki yangu alikuwa Mkuu wa mafunzo ya mbwa na farasi chuoni hapo kwa sasa ameacha kazi na sina mawasiriano naye.
 
Mkuuu msaada wa picha tuwaone hao mang'ang'a
 
Mkuu kama unauza naomba tuwasiliane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…