Gerson Msigwa aipongeza MSD kwa kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba

Gerson Msigwa aipongeza MSD kwa kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba

Serikali wana uhakika wanaweza kuendesha viwanda vya madawa na vifaa tiba? nafikiri yanayofanyika ATCL kila mmoja wetu anayaona......nyie piganieni promo tu za kikanda na kikabila, naona wajanja wameshasoma mchezo hapo.......
 
Gerson Msigwa angemuuliza afande maswali yafuatayo;

1. Ni Bodi ipi ilipitisha huo mradi!

2. Report ya cost benefit analysis ya huo mradi iko wapi!

3. Huo mradi umeanzishwa kwa sheria ipi ya Bunge?, kwasababu MSD ilianzishwa kwa sheria namba 13 ya Bunge ya mwaka 1993 kwa kufanya; manunuzi, kuhifadhi na kusambaza dawa za binadamu, kazi ya uzalishaji haipo. Hatutaki kuwa na kiongozi ambae anajifanyia tu mambo kwa utashi wake utafikili yuko nyumbani kwake

4. Nani alipitisha kujenga kiwanda kwao Iringa, je kuna kuna report yoyote ya upembuzi yakinifu?

5. Je nani alipitisha kuanza uzalishaji wa hizo gloves badala ya dawa, maana MSD ina catalogue items ya dawa 385 ambazo zinahitajika hospitalini at any time T

6. Mkandarasi wa ujenzi alipatikanaje? Kulikuwa na ushindani? Maana inasemekana ilikuwa through single source ikiwa ni pamoja na materials za dawa

7.

8.

Hayo ndo maswali aliyotakiwa kuuliza Msigwa!
Inaongozwa kijeshi we unataka mamichakato yetu ya kifisadi ili mpige 10%
 
Msigwa naona anavuka sana mipaka ya utendaji kazi wake. Nani kamwambia awe anafanya haya majukumu? Nini kazi ya Waziri husika? Msigwa anapaswa kujua mwisho wa utendaji kazi wake. Huyu kwa hizi mbio za sifa anazofanya anatakiwa kukemewa.
 
Inaongozwa kijeshi we unataka mamichakato yetu ya kifisadi ili mpige 10%
Wewe vipi! Kwani huku ni jeshini? Huku hatutunzi maghala ya kuhifadhia mabomu, huku taasisi zinaendeshwa kwa sheria za utumishi wa umma. Na manunuzi yanafanyika kufuata sheria za manunuzi mbali ya hapo wewe ni fisadi

😆😆😆 nenda kawaulize suppliers waliokuwa wana-supply dawa na vifaa tiba pale Lugalo enzi za afande kilichokuwa kinafanyika utashangaa!!
 
Back
Top Bottom