Siungi mkono uharibifu wa uwanja, lakini kwamba uwanja wa Mkapa umekarabitwa kwa mabilioni sidhani kama ni kweli. Nilienda hapo siku mbili kabla ya mechi ya Simba na Yanga. Kama mnaouita ukarabati mkubwa ndio ule basi Watanzania tuna matatizo ya akili. Sikuona CHOCHOTE kilichokarabatiwa au kubadilishwa. Viti chakavu uwanja mzima, sehemu za kupigwa rangi hazijapakwa rangi mpya, vyoo vichafu kama zamani na mengine mengi. Nakumbuka siku hiyo mvua ilinyesha, niliingia ofisi mojawapo hapo hapo uwanjani nikakuta inavuja mpaka wameweka ndoo katikati ya ofisi kukinga maji yanayovuja. Halafu tunaambiwa ukarabati wa mabilioni umefanyika. Kwa kweli nilijiuliza nchi hii ina matatizo gani?